Mtuhumiwa kesi ya Dk. Ulimboka atoa siri nzito...

Mtuhumiwa kesi ya Dk. Ulimboka atoa siri nzito...

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi Makao Makuu na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa kauli tata kuhusu uchunguzi wa tukio la kutekwa, kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, mtuhumiwa pekee katika kesi hiyo hadi sasa, raia wa Kenya, Joshua Mulundi, ameibuka na kutoa kauli na siri nzito ya tukio hilo.

Mtuhumiwa huyo ambaye yuko mahabusu, ameliambia gazeti hili kuwa anataka upelelezi wa kesi yake ukamilike haraka ili atendewe haki, lakini kubwa kuliko yote ameitaka serikali imlete Dk. Ulimboka mahakamani ili aweze kumtambua.

Akizungumza kwa kificho kwa njia ya simu kutoka ndani ya Gereza la Keko alikohifadhiwa, raia huyo wa Kenya alisema ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kusoma taarifa ya gazeti hili juzi ilikionesha polisi wakirushiana mpira na kutoa kauli zinazopingana kuhusu tukio la Dk. Ulimboka.

Alisema hadi sasa haoni maendeleo ya kesi hiyo kwani kila ikifika mahakamani, upande wa mashitaka hutoa hoja ya kutaka iahirishwe kwa madai kuwa upelelezi haujakamilika.

“Kila ninapoenda mahakamani naiomba mahakama imlete Dk. Ulimboka anitambue, nahoji kwanini upelelezi haujakamilika. Kwa bahati mbaya sana siku hizi kesi hii inapokuja mahakamani, hata vyombo vya habari havijulishwi. Nashukuru Mungu nimepata namba zenu za simu kutoka kwenye gazeti lenu ili nitoe ya moyoni...

“Naomba Dk. Ulimboka aletwe mahakamani ili anitambue, kama atasema mimi ndiye niliyemteka na kumtesa, basi kesi iendelee na sheria ichukue mkondo wake, kama atasema sikuhusika, basi kesi iishe maana sioni sababu ya mimi kuteseka hapa gerezani kwa kusubiri upelelezi ambao haujulikani utaisha mwaka gani,” alisema Mulundi.

Kwa mujibu wa mtuhumiwa huyo, amepata kutoa malalamiko kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akiiomba serikali imlete mbele yake, Dk. Ulimboka ili amtambue na kuhakikisha upelelezi wa kesi hiyo unafikia tamati.

Mbali ya maombi hayo, mtuhumiwa huyo wa kesi inayovuta hisia za wengi ndani na nje ya nchi, pia alisema aliwaomba viongozi hao wamsaidie kupata dhamana kwani kesi inayomkabili inaruhusu dhamana na hana wakili wa kumtetea.

“Dk. Nchimbi alipokuja hapa gerezani nilimwambia, lakini aliniangalia tu bila kujibu kitu. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Kairuki nimemwambia, DPP nimemwandikia barua na hata Balozi wa Kenya nchini Tanzania nimemwandikia, hajanijibu wala hakuna msaada ninaopata. Naomba serikali, jamii inisaidie kesi hii imalizeke haraka,” alisema mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alitoa siri nzito ya kile alichokieleza kuwa, ukweli kuhusu Dk. Ulimboka, jinsi alivyokamatwa, kuhojiwa na kufikishwa mahakamani katika mazingira aliyodai tatanishi, ambayo gazeti hili kwa sasa haliwezi kuripoti kwani kufanya hivyo ni kuingilia mwenendo wa kesi iliyopo mahakamani.

Wakati Dk. Ulimboka alitekwa Juni 26 mwaka jana na watu wasiojulikana, mtuhumiwa huyo alikamatwa Julai 3 na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kitusu, Dar es Salaam Julai 13.

Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari uliotikisa nchini katika nyakati tofauti mwaka jana, alitekwa, kuteswa, kupigwa hadi kung’olewa meno na kucha na kisha kutupwa katika msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alitangaza kuunda tume ya wataalam kutoka ndani ya jeshi hilo, iliyoongozwa na ACP Ahmed Msangi.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Dk. Ulimboka mwenyewe kuwataja baadhi ya watu aliodai kuwa ndio walihusika kumteka na kumtesa, lakini hadi sasa Mulundi, ndiye mtuhumiwa pekee aliyekamatwa.

Hata hivyo, tume hiyo haijawahi kutoa ripoti yake kama Kova alivyoahidi pamoja na kwamba hata majeruhi mwenyewe, Dk. Ulimboka hajawahi kuhojiwa, huku vigogo wa jeshi hilo wakitupiana mpira kuhusiana na sakata hilo.

Katika hatua ya kushangaza, juzi jeshi hilo kupitia kwa msemaji wake, Advera Senso, limekanusha kuwepo kwa tume hiyo likisema kuwa walioteuliwa ni polisi ambao watafanya kazi za kiuchunguzi kwa taratibu za polisi.

Kauli ya Senso ilipingana na ile ya Kova, ambaye juzi alikiri kuwepo kwa tume hiyo, lakini akasema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa vile taarifa zake alishazipeleka kwa wakubwa wake makao makuu baada ya kukamilisha wajibu wake.

“Hili suala lipo mahakamani kwanza, na kuhusu kuhojiwa au kutokuhojiwa kwa Dk. Ulimboka hilo lipo kwa mkubwa wangu, sasa unataka mimi niseme kama amehojiwa au la wakati sijui kinachoendelea huko?” alisema Kova.

Lakini Senso alisema kuwa, hakukuwepo na tume hiyo na kwamba walioteuliwa ni polisi ambao walifanya kazi za kiuchunguzi kwa taratibu za jeshi hilo.

Alisema Jeshi la Polisi lisingeweza kuunda tume katika suala la Dk. Ulimboka kwa kuwa kilichotokea ni uhalifu kama mwingine na litashughulikiwa kwa mujibu wa jeshi hilo.

“Kwanza hilo ni suala la mwaka jana na sisi ripoti za mwaka huo tumeshafunga, labda nianze kufuatilia sasa hivi kujua limefikia wapi,” alisema Senso.

Wakati vigogo hao wakisigana katika kulifafanua sakata hilo, Dk. Ulimboka mara kadhaa amekuwa akieleza kuwa yupo tayari kutoa maelezo yake kama kutakuwa na tume huru ambayo si hiyo iliyoundwa na polisi.

Katika tamko lake mwishoni mwa mwaka jana lililosomwa kwa niaba yake na wakili wa kujitegemea, Nanyoro Kicheere, akimwakilisha mwanasheria wake, Dk. Ulimboka alisema wapo watu ambao hawatapenda kusikia siri iliyojificha katika tukio zima la kutekwa kwake na kwamba hana jinsi zaidi ya kueleza ukweli.

Alisema kuwa tukio la kutekwa kwake, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno, na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande, lilitokea wakati akiwa kikao na ofisa aliyetambulishwa kwake ni ofisa wa Ikulu, Ramadhani Abeid Ighondu.
 
Yatajulikana tu! Nchemba atakuwa na mkanda wa ikulu wakipanga mauaji.
 
hivi huyo raia wa Kenya wanamtesa bure kwasababu gani na wakati Ramadhani Ighondu yupo anavuta hewa bure?
 
polis CCM inabambikia watu kesi waziwazi. polisi force ni crime gang ambalo yapaswa wananchi tuchukuwe hatua kali dhidi yao. waliomtesa Ulimboka wapo wana-enjoy mitaani halafu mtu innocent anaozea keko. ajabu sana nchi hii. nimegundua watu wenye free minds ni wachache sana. anyway yatakayo tokea yote yalishatabiriwa. maskini Mtanzania..
 
Inchi hii viongozi wana 2tawala kwa mkono wa chuma, hawafuati utawala bola kam wanavyo pigia kelele.chengine nyie mnaejiita wanaharakati wa haki za kibinaa dam mkowapi? Msaidieni jamaa huyo ( alie gerezani ) apate haki yake!
 
Je,kiusalama inaruhusiwa mtuhumiwa kumiliki simu gerezani na kwa mazingira gani? Anyway,liwalo na liwe!
 
Ramadhani Inghondu bado yupo magogoni ama anaendelea kula kuku sauzi?
 
kwa upande wa sirikali na vyombo vyake vya usalama (police,usalama,dpp etc) hawako tayari kuingia aibu kwa uhusika wao kwenye hii issue, kamwe hawatakuwa tayari kusikia ukweli wa kilichotokea na waliohusika kuanikwa hadharani
 
Jee, wewe unavuta hewa kwa kuinunuwa? Ukimaliza hilo unganisha hii picha: dokta wa kannoni silaa ana ardhi huko pande, ni mchungaji kondoo aliyepotea na ana uhusiano na kanisa, mkenya ni kondoo aliyepotea na amekamatwa taarifa zikitokea kanisani. Hapo sasa!

Badala ya kumshambulia mtu asiye kwenye mada au mamlaka, nilitegemea angalau, kama huhusiki na utekaji, ujibu hoja moja tu...kwa nini mpk sasa mtuhumiwa alokamatwa ni mmoja tu!!!? Si unajua polisi wa inji hii walivyo wepesi kwa kukamata mtu wakisikia tu harufu yako ilikuwepo wakati wa tukio"!!??
 
Hii singo imepitwa na wakati, nasikia dokta slaa ana ardhi msitu wa pande, jee, kuna uhusiano hapo? Vitu vimejificha.

Kumbe upo?
Nilidhani nawe ulikuwa mahabusu na dhamana yako imekataliwa.

Heri ya mwaka mpya. HAKIIIII
 
Laiti kama ningekuwa Ulimboka ....
Ban on Duty
 
Hayo yanayofanywa polisi, mahakama na Waziri mwenye dhamani yanazidi kudhihirisha kuwa Ikulu chini ya utawala wa ccm inafahamu kitu na ndiyo maana wateule wa rais wanapata shida kufuata sheria badala yake bora wakiuke. Kwanini hawataki kumhusisha Dr. Ulimboka wakati anawafahamu waliomteka na kumtesa lakini serikali chini ya utawala dhalimu wa ccm inampuuza kana kwamba amekufa. Shame on my Country.
 
Back
Top Bottom