Mtu wa Kanda ya Ziwa kutokujua kuogelea ni ujinga wa hali ya juu

Vyombo vya majini vina taratibu zake za ku-handle na wanajua kabisa maana huruhusiwi kuingia bila ticket na ikiwezekana orodha ya raia ibaki nchi kavu (of course kwa kivuko kwa kuwa ni huduma ya kuvuka angalau idadi ya abiria nchi kavu ijulikane lakini pale tumeambiwa idadi haijulikani kwani mkata ticket nae alikuwa ni sehemu ya waliokufa).
Ila vivuko hawaangaliagi idadi ya watu hata MV magogoni, na kigamboni watu wanakata tiketi mnaingia bila idadi ni wewe tu kuamua basi kiukweli ni hatari sana
 
Ni uzembe sana kwa watu wanaokaa karibu na airport kushindwa kuendesha ndege
 
Ila vivuko hawaangaliagi idadi ya watu hata MV magogoni, na kigamboni watu wanakata tiketi mnaingia bila idadi ni wewe tu kuamua basi kiukweli ni hatari sana
Wanafanya assumption kwa kukadiria abiria kulinganisha na magari yaliyoingia na kuona bado kinaweza kula nyomi, matokeo yake unakula nyomi alafu inaingia gari moja tu imebeba mzigo wa nguvu ukijumlisha na wananchi unakuta umezidisha (ifike mahala wabebe raia wanaopaswa kubeba yaani raia wawe sambamba na life jacket kwa idadi - msingi wa kuwa na kivuko ni kutoa huduma na kurudisha gharama za matengenezo ikiwezekana na kulipa wafanyakazi lakini vingi vinatumika kwa ajili ya ku-maximize profit na wanaoendesha pia wapige chao
 
Yani inabidi sasa hivi wanaoshindwa kuvisimamia wafungwe tu basi maana magari huingia bila kuangaliwa uzito plus abiria mi ni kipanda kivuko huwa nawaza sana maana ni hatari, na kikikaribia mwisho abiria wote huamia mbele
 
Licha ya ajali kutokuwa na fundi vingine vinaepukika imagine watu wangevaa life jackets zingesaidia licha ya kufunikwa tusisingizie ajali haina fundi vingine tunaweza punguza athari yake watu 100 ni wengi hafu kila siku changamoto za vivuko hazifanyiwi kazi, uzembe unapoteza watu wasio na hatia
Uzembe wa wahusika hapo nakuunga mkono lakini kulaumu kwanini hawajui kuogelea hapana asee!
 
Kkkkkkkk watu Wa Dar wafundishwe kuvuka barabara! Kipindi nilipoenda kusoma Ujerumani somo la kuogeleaa lilikuwa ni LAZIMA kama hujui na hataki kujifunza kuogelea rudi kwenu hawakubembelezi na walikuwa wakiwashangaa sana watu ambao wanatoka sehemu ambayo kuna bahari/mto/ziwa halafu hujui kuogelea
Nalog off
 
Uzembe ni tatizo ila waliojirusha kwa Maji walipona kuna mama mjamzito alijirusha kapona naye
Tukio lilikua ghafla mno that’s why wale waliokua ndani hawakupata chance ya kuchomoka kirahisi, majority ya waliopona ni wale waliokua nje nadhani
 
Mkuu sema wengi hujifunza sehemu tofauti tofauti, sasa mtu aliyekulia kwenye ziwa kufa bila Ku fight hafu karibu na nchi kavu inasikitisha sana bora watoto.

Una fight vp mama?hivi kuna binadamu yupi au kiumbe hai kipi kinachoona hatari mbele yake kisichukue hatua yoyote?
Unafikiri waliofariki,walikuwa wamekaa tu wakisubili mauti?
Kumbuka kivuko pia kilibeba mizigo mingi yakiwemo magari,na naamini wengi walikandamizwa na haya magari wakati kinapinduka,na wengine walizamishwa zaidi kwenye maji baada ya kujaribu kuishika mizigo hii isiyoweza kuelea ndani ya maji.
Jana nilimsikia mtaalam mmoja akiwa anahojiwa kwenye radio,alisema kwa mujibu wa mmoja wa wahanga,kuwa baada ya kivuko kukaribia kufika,nahodha alikata kona ya ghafla,kutokana na kuelemewa na uzito kivuko kilipinduka kwa ubavuni.
Point yangu ni kwamba,unaweza kuwa unajua kuogelela,lkn kutokana na msongamano mkubwa wa watu na mizigo, chombo kinapopoteza balance,watu hulaliana na hata kukandamizwa na mizigo,na hata wengine kujeruhiwa,hapo kujiokoa huwa ni mtihani.
 
Back
Top Bottom