Mtu wa Kanda ya Ziwa kutokujua kuogelea ni ujinga wa hali ya juu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Heshima kwenu wakuu,

Nakumbuka kule Nungwi watu waliogelea kilometa tano hadi wakaogelea. Eti hawa Wasukuma wanajiita wanaume wa mkoani wanashindwa kuogelea mita 50.

Wapemba wanaogelea kwenye bahari ambayo maji ni ya chumvi na hawafumbi macho.

Ni uzembe mtu unakaa Ukara eti hujui kuogelea hata mita mia moja.

Nmesikitika sana na wameniaibisha sana.

Mtaalam wa kuogelea angeweza kuokoa watu 50 kwa wakati mmoja, anawavuta na wengine kuwabeba mgongoni.

Hii ajali ya MV nyerere itupe fundisho. Tujifunze kuogelea.

Wapemba pale Msimbazi wanaogelea tu. Hutasikia Mpemba kafa maji kizembe.

Hongera kwa Serikali ya Zanzibar kwa kuwawezesha kila raia mkazi ajue kuogelea.
d802429474b6599b15861299daa54351.jpg

Yaani hapa na pale Mwanaume wa Mkoani kashindwa kuogelea!?

Serikali ianze kutoa elimu mashuleni kulingana na mazingira. Watu wa Pwani na Ziwani wafundishwe kuogelea. Watu wa polini wafundishe kupambana na wanyama wakali, watu wa dar wafundishwe kuvuka barabara. nk. Watu wa mikoani wafundishwe kulima pia

Injinia Cherehani kutoka akiwa mzima baada ya kukaa majini siku mbili, ni kielelezo kwamba wananchi wangepewa elimu ya kuogelea na kuishi majini kwa muda mrefu ikiwemo mbinu ya kujipaka oil, wengi wangeokoka.
 
Heshima kwenu wakuu,

Nakumbuka kule Nungwi watu waliogelea kilometa tano hadi wakaogelea. Eti hawa Wasukuma wanajiita wanaume wa mkoani wanashindwa kuogelea mita 50.

Wapemba wanaogelea kwenye bahari ambayo maji ni ya chumvi na hawafumbi macho.

Ni uzembe mtu unakaa Ukara eti hujui kuogelea hata mita mia moja.

Nmesikitika sana na wameniaibisha sana.

Mtaalam wa kuogelea angeweza kuokoa watu 50 kwa wakati mmoja, anawavuta na wengine kuwabeba mgongoni.

Hii ajali ya MV nyerere itupe fundisho. Tujifunze kuogelea.

Wapemba pale Msimbazi wanaogelea tu. Hutasikia Mpemba kafa maji kizembe.

Hongera kwa Serikali ya Zanzibar kwa kuwawezesha kila raia mkazi ajue kuogelea.
Wa kanda ya kaskazini tunawashinda daaah hatari, huku kaskazini haswa klm kila raia anajua kuogelea 😂😂😂
 
Umewakosea heshima wana kanda ya ziwa.
Hivi umeona kile kivuko kilivyokaa, kimegeuka juu chini. Kwa waliokuwa ndani ya kivuko sehemu zile za kukaa kutoka si rahisi. Mizigo,magari na wingi wa watu kutoka ni ngumu.
Nadhani wengi waliopona ni wale waliokuwa juu .
 
Hata Mimi nimeshangaa MTU unakulia ziwani hujui kuogelea what a shame hafu kivuko hakikuwa mbali na nchi kavu aisee, wajifunze kuogelea, mfano wangekuwa wanajua kuogelea maafa yasingekuwa makubwa
wa
Wewe mjinga kweli kaskazini kuna ziwa msipende kujilinganisha na watu wengine
😂😂😂😂 lipo mkuu ziwa manyara,babati,mito IPO kama yote so kuogelea tunajua sana tyu
 
. Eti hawa Wasukuma wanajiita wanaume wa mkoani wanashindwa kuogelea mita 50..

Sio wote waliokuwa ndani ya Ferry ile ni Wasukuma. Sio wote ni wakazi wa kule. Unaweza kukuta wengine walikuwa wageni wameenda kule kikazi tu kwa muda mfupi. Tusidhihaki mambo haya, especially pale ambapo maisha ya wengi yamekatizwa ghafla.

Mimi na team kutoka Wizara ya Afya nilishawahi kupanda kivuko hicho kwenda Ukara last year wakati wa Cholera outbreak. Hali niliyoiona nilijua tu ipo siku haya mambo yatatokea. Tungepatwa na hii dhahama tungelaumiwa pia "kwa uzembe wetu wa kutokujua kuogelea". RIP marehemu wote
 
Umewakosea heshima wana kanda ya ziwa.
Hivi umeona kile kivuko kilivyokaa, kimegeuka juu chini. Kwa waliokuwa ndani ya kivuko sehemu zile za kukaa kutoka si rahisi. Mizigo,magari na wingi wa watu kutoka ni ngumu.
Nadhani wengi waliopona ni wale waliokuwa juu .
Mtu unaruka. Ukiwa mtu wa kuogelea, lazima ujue dalili ya meli itakayozama.
 
Vitu vingine tunaweza kuviepuka wenyewe tu kwa kujifunza mi hii ajali imenishangaza mno, ukulie ziwani hafu ufe Maji kizembe, kuna haja ya kuongeza mitaala ya jinsi ya kujiokoa kwenye elimu yetu
Vitu vingi tu huwezi kuviepuka.. utaelewa vizuri siku yako ya kufa.huwezi kuamini kitakachokuua ni kitu kidogo sana.mabaya kwa mwanadamu yanatokea popote muda wowote.kifo Ni mtego
 
Vitu vingine tunaweza kuviepuka wenyewe tu kwa kujifunza mi hii ajali imenishangaza mno, ukulie ziwani hafu ufe Maji kizembe, kuna haja ya kuongeza mitaala ya jinsi ya kujiokoa kwenye elimu yetu
Jamani jipeni mda wa kuwasikiliza wahanga wa ajari hiyo,

Nasikia kuna wengine walikua ndani, hawa walifunikwa ghafla,

Waliopona ni Wale wachache waliokua kwa nje

Ndg zangu ajari haina fundi.
 
Back
Top Bottom