Mtu na kujitambua

Mtu na kujitambua

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
MTU NA KUJITAMBUA.

Watu wengi siku za Leo,wamekuja na shauku ya kutaka kujitambua,je twajua au hatujui maana yake?.

Utambuzi wa mtu upo wa Namna nyingi sana.
Kuna kujitambua kifikra,Kuna kujitambua kiroho ,Kuna kujitambua kiakili,Kuna kujitambua kimwili nk nk.

Sasa ninachotaka kuongelea ni utambuzi wa kujijua wewe ni nani.

Utambuzi ni kujijua ndani mwako,kurudi ndani mwako ,kurudi kwenye asili,Sasa hapo ndipo ilipo kazi,wengi tunajua tunapo Rudi kuitambikia Mizimu ndiko kujitambua,wengine tunajua pale tunapoielezea historia ya Afrika saana ndiko kujitambua,Wengine wanajua pale tunapokataa Dini na madhehebu yake kisa yamekuja na wakoloni ni kujitambua nk ,Lahasha tunafeli ,kuabudu mizimu,Kumiliki majini na Negativity zingine zifananazo vyote hivyo ni mitetemo ya chini sana.

Asili ni Ile mwanzo ,Ile iliyokuwako ,iliyoumba Kila kitu,iliyokuumba na mwili wako,hiyo ndio LIGHT AND SOUND, ambayo Leo hii ipo ndani mwako,hiyo ndio asili ambayo ni mitetemo ya juu sana,ipo katika mwendo wa Ajabu mno,ndio maana haifi milele yote, hayupo mchawi ,Wala jini ,Wala mizimu Wala Mganga,,Wala chochote kiwezavyo kushindana nayo.

Asili Iko ndani mwako,jishushe na kimwili Kako hako nawe utaishuhudia,na itakutendea mambo makubwa na ya Ajabu mno.
 
Mwanga na Sauti.

Hivi vitu viwili viliumbwa kwa Neno.

Neno ndie Mwanzo na Mwanzo ndie Mungu mwenyewe(Utupu)nothingness.

Neno lilitoka kwenye Utupu na kusema(Sauti ),(nguvu ke) ,na iwe Nuru ,kumbuka Sauti ndio ilisikika kutoka kwenye Utupu na iwe Nuru ,ilipotokea Nuru(nguvu me), zikaungana zote kuwa kitu kimoja vinavyotembea pamoja,au tunasema mwili mmoja kwa maana hizi Mwanga na Sauti ziliingia katika maumbile, maana ndio waumbaji wa Kila kitu.

Hata sisi wanadamu na viumbe vyote na vitu vyote tunazo nguvu hii ya light and sound ambayo ipo ndani mwetu,inaumba na KUUA Kila Leo.

Nguvu hii ipo katika mwendo mkali sana na WA Ajabu na katika layer NDOGO mno ,ambapo huwezi kuiona kwa macho ya kawaida,pale inapoingia katika maumbile haiwezi kuonekana mpaka kufanya mazoezi maalumu ya kutafakari.

Unapofanya mazoezi ya kutafakari ,nguvu hii huanza kujidhihirisha kwako na kukufanya kuwa sehemu yake.

Nguvu hii hapo Mwanzo ilikuwa imetulia pamoja na Mungu ,lakini baadae iliamua kujitenga na Mungu ili kusambaratisha Maumbile yote Ulimwenguni/kuumba maumbile yote ulimwenguni.
Ambapo Leo tuna Kila aina ya maumbile kama Sayari,Nyota ,Galaxies,magimba mbalimbali,watu,wanyama,mimea,madini nk,hii yote ni matokeo ya Mwanga na Sauti.

Nguvu hii ndio inayokushikilia wew katika mwili wako huu,Leo unapojiona upo hai ni kwa sababu ya nguvu hii ,ndio inayoleta uzima kwako .
 
Back
Top Bottom