Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama, lakini naona kwao ni tofauti

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Mimi nilifikiri ile methali kwao wangeitumia lakini bado wanakufa kisabuni maana methali inasema mtu mzima akivuliwa nguo uchutama lakini naona kwao ni tofauti kabisa maana ni watu wazima lakini suruari imeshushwa hadi chini, boxer pia ipo chini ya vidole vya miguu lakini wanaendelea kuning'iniza tu. jamani.

Jamani hiyo CHADEMA ndiyo baibai kama ilivyokuwa NCCR Mageuzi na CUF hata CDM nayo itakuwa zilipendwa, nendeni mkakae chini mtafakari hili mje kivingine kwa sasa mnajirisha upepo, maana kujifariji kwenu pia kwa ajabu hii ni nchi ambayo ilipata uhuru 9 Dec 1961 ni soveriini steti ina mahakama, Rais, Bunge, Bendera, Ngao na zana zote yaani haiingiliwi kama mnavyofikiri yaani ni kweli mtapata taabu sana kwa kuupenda urofa na ubora wake.

Ni bora mkakubali kuwa jamaa amewazidi kwa kila kitu maana imeonekana wani kila mliposogeza ugoko jamaa amekuwaana tupia jiwe la kilo 90 na sasa hamna miguu na maumivu ni makalisani, jisalimisheni, huu mziki si wa kitoto ndiyo maana mlipewa taarika mapema na Jakaya Mrisho Kikwete alisema kuwa sasa imetosha nawaletea 'chuma'.
 

IMG_20201102_182800.jpg
 
😁😁😁 Kwahiyo mlijua mmeua upinzani? Hapo ndipo mlipofeli, upinzani ni fikra na kamwe hauwezi kufa maana fikra kinzani zitaendelea kuwepo!

Pole sana kama ulitegemea kutuona mitandaoni tukiendeleza harakati, jiandae kisaikolojia maana mwendo ni huu huu kwa miaka hii 5 na baada ya hapo!
 
Amewazidi Chadema kwa lipi?,kukiuka misingi ya demokrasia?mauaji ya wasiojurikana?usijifanye wewe ni sawa na wao,wewe utasomesha shule ya kata,hakuna hata waziri atapereka mtoto wake shule ya kata.

Hana uchuma wowote,alipokea fedha za korona kiujanja,waliozitoa wanesema,Kama ni Mwamba kweli azirudishe tuone,yeye si anakusanya nyingi.
 
Hahaha huu ni mgogoro wa CCM sio mgogoro wa Tanzania kama wanavyotaka kutuaminisha wananchi.

Sasa wanatoa kauli za jumla jumla ohoo heshima na utu wetu. Hapana ccm msituingize wananchi kwenye mgogoro wenu.

Kabudi na Magufuli ni ccm, sisi ni watanzania please muelewe hivyo.
 
😁😁😁 Kwahiyo mlijua mmeua upinzani? Hapo ndipo mlipofeli, upinzani ni fikra na kamwe hauwezi kufa maana fikra kinzani zitaendelea kuwepo!

Pole sana kama ulitegemea kutuona mitandaoni tukiendeleza harakati, jiandae kisaikolojia maana mwendo ni huu huu kwa miaka hii 5 na baada ya hapo!
Lazima utofautishe upinzani na chama katika fikra zako. Chadema inaweza kufa lakini si upinzani. Like wise chadema inaweza kushika dola na ccm itakuwa ni chama cha upinzani. Ni muhali kutofautisha vyama na dhana ya upinzani
 
Lazima utofautishe upinzani na chama katika fikra zako. Chadema inaweza kufa lakini si upinzani. Like wise chadema inaweza kushika dola na ccm itakuwa ni chama cha upinzani. Ni muhali kutofautisha vyama na dhana ya upinzani
Ndio hivyo,huyu JPM na serikali yake tutaendelea kumkosoa na kumdhoofisha mfululizo mpaka muda wake utakapokwisha!
 
Zile ajira milioni 8 mlizoahidi ndo hizi za kukejeli upinzani mtandaoni siyo?
 
Tanzania ni mali ya watanzania, hii nchi sio mali ya Pombe na CCM yake, uamuzi wa kutumia nguvu za dora kuwatisha wananchi na udikteta uchwara una mwisho wake

Kazi kwenu CCM wakoloni weusi pambaneni na EU mrudishe hela yao pimbi nyie
 
Ni upumbavu kumuona MTU anaandika Uzi kama huu wakati nchi inadidimia kwa kauli zinazo onyesha wazi nchi kama nchi inaangamia na kupoteza heshima huku mkiufanya uendeshaji wa nchi kama ushindani wa Simba na Yanga
 
Tangu uchaguzi umeisha Chadema hawajafanya press conference zaidi ya mbili.Tumeambiwa humu ndani kuwa Makao Makuu yao yapo kimya na hata nyasi zimeanza kuota mlangoni.Ulitaka wafanye kitu gani hasa???
 
Back
Top Bottom