Mtu mwenye akili akikushauri jambo la kijinga ukakubali atakudharau

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Wanabodi salamu!

Siku za hivi karibuni kumekuwa na watu wengi wakienda Ikulu kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhesimiwa JPM jinsi ya kuendesha serikali yake. Ni jambo jema, lakini baadhi ya watu wanao kwenda kumshauri wanakosa sifa za kuwa washauri wazuri.wanaweza kuwa na ajenda za kibinafsi zaidi kuliko masilahi ya Nchi.Wanaweza kumshauri Rais mambo ya kijinga na akikubaliana nao baadae watamdharau ingawa ajenda zao zitakuwa zimetimia.

Kipimo kizuri cha utendaji wa serikali ya Mheshimiwa Magufuli ni wananchi. Wananchi walio wengi anamkubali sasa zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika tasinia ya siasa.Kwa mtazamo wangu, akitaka kujua hilo, leo hii akiitisha mkutano wa siasa popote pale ili kufafanua mambo mbalimbali atakuwa mwanasiasa wa kwanza wa CHAMA CHA MAPINDUZI kujaza watu lukuki bila kuwasomba na malori katika zama hizi za vyama vingi.wanao wanao mshauri awasikilize lakini wenye ushauri unao kinzana na matarajio ya wananchi awapuuze

Wananchi wanataka katiba mpya ile ya Warioba, wanataka miji iliyo pangiliwa vizuri, wanataka uwajibikaji serikalini, wanataka huduma bora za afya na elimu, wanataka utawala wa sheria! it is now or never!
 
Magu tangu aingie ikulu hakuna hata moja alilofanikiwa, kuanzia shitukiza yake hadi matamko, nashindwa kuelewa wakati ana tia nia sijui alijipangaje, naona bla bla blah tu
 
sidhani kama amejiandaa kuikomboa hii nchi alijitamba na mabadiriko ya kweli ameshindwa sasa wapambe wake mumeanza kukata tama munasingizia wapambe wanamshauri vibaya si ana executive power
 
kuna
Magu tangu aingie ikulu hakuna hata moja alilofanikiwa, kuanzia shitukiza yake hadi matamko, nashindwa kuelewa wakati ana tia nia sijui alijipangaje, naona bla bla blah tu
watu dunia kamwe hawezi kukubali jambo analo fanya mtu mwingine kuwa ni jema. Huyu Magufuli wazungu watu wa viwango wamemvulia kofia halafu wewe hata kuandika jina lote la Magufuli unaona uvivu unaweza ukasimamia jambo likafanikiwa? haiwezekani.
 
Magu tangu aingie ikulu hakuna hata moja alilofanikiwa, kuanzia shitukiza yake hadi matamko, nashindwa kuelewa wakati ana tia nia sijui alijipangaje, naona bla bla blah tu
Si bure, itakuwa ulichezewa na jirani yenu ulipokuwa mdogo.
 
kuna

watu dunia kamwe hawezi kukubali jambo analo fanya mtu mwingine kuwa ni jema. Huyu Magufuli wazungu watu wa viwango wamemvulia kofia halafu wewe hata kuandika jina lote la Magufuli unaona uvivu unaweza ukasimamia jambo likafanikiwa? haiwezekani.
siwezi, eti wazungu wamemvulia kofia! nani kakudanganya??? Wazungu ni wanafiki tu kwa Magu, hapo anaandaliwa kisaikolojia kupigwa mizinga mitakatifu, chekea wazungu nyie mtalala nje
 
siwezi, eti wazungu wamemvulia kofia! nani kakudanganya??? Wazungu ni wanafiki tu kwa Magu, hapo anaandaliwa kisaikolojia kupigwa mizinga mitakatifu, chekea wazungu nyie mtalala nje
Hata me nawashangaa eti kipimo cha uwajibikaji ni wazungu looh ina maana serikal sio ya Watanzania bali ni ya wazungu
Akumbuke sisi wana UKAWA tutaanza kuyaamini mabadiliko chini ya magufuli endapo tu ataanza kushughulikia waizi wa ESCROW MEREMETA EPA bila kumsahau fisadi wetu mkuu LOWASA na lirichmond lake
Ovaaaa
 
Tupo pamoja, Na hawezi angekuwa Na nia ya kufanya hivyo SAA hiz tungekuwa twaongea mengine
 
Tupo pamoja, Na hawezi angekuwa Na nia ya kufanya hivyo SAA hiz tungekuwa twaongea mengine
Walituaminisha kuwa Lowasa fisadi tunataka kuona basi wakimshughulikia waache siasa na utoto kama Nape yupo serikalini na huku analalamikia mafisadi sasa je si raia tufanyaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom