Mtu kuonekana mzee kuliko umri wake halisi

Tricker

Member
Nov 26, 2010
96
25
Habari zenu waungwana!
Naomba mnaojua sababu zinazomfanya mtu aonekane mzee kuliko umri wake na jinsi ya kuzitatua,
Kwa mfano najua moja ni kunywa pombe kulikokithiri na solution ni kuacha au kupunguza pombe.Sasa wale wenye sababu nyingine ukiacha hii nilioitoa naomba mnijuze.
Mbarikiwe.
 
Kula natural food, bila mafuta mengi, kufanya mazoezi mara kwa mara. Kunywa maji mengi kwa siku
 
Jitahdi kufanya mazoezi sana tena sana,na ujitahdi kula vyakula vyenye virutubisho mwilini.
 
Acha misigara na GANJA (kama unatumia) Pia MASANGA kupita kiasi lazima UZEEKE SURA kuliko umri wako
 
kutopumzisha mwili - nyakati za usiku - kukosa usingizi - kunazeesha

kuruhusu minyama uzembe - mafuta mengi mwilini - kutofanya mazoezi

kuwa na mawazo mengi - stress - kukosa amani moyoni

kuwa na uchungu moyoni - unajitokeza nje - na inazeesha sana
 
kutopumzisha mwili - nyakati za usiku - kukosa usingizi - kunazeesha

kuruhusu minyama uzembe - mafuta mengi mwilini - kutofanya mazoezi

kuwa na mawazo mengi - stress - kukosa amani moyoni

kuwa na uchungu moyoni - unajitokeza nje - na inazeesha sana

Nalala sana usiku,ofcourse manyama uzembe yapo asante kwa kunijuza husababisha uzee,stress nikawaida kwa mtz sema naomba unipe mbinu ya kuzikwepa,hiyo ya uchungu moyoni ndo sijaielewa kabisa ndo nini?
 
Mara nyingi na maumbile tu ya mtu (ndion sa zingine utasikia mtu anaambiwa 'udongo' wake mzuri...ikiwa na maana hazeeki upesi!).

Huu ugonjwa wa kisasa pia unafanya mtu aonekane mzee kuliko umri wake!
 
Punguza uzinifu. Unapofanya mapenzi na wanawake wengi/tofauti tofauti.. unajipunguzia afya ndio maana wazinzi wanachakaa sana kabla ya muda.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom