tamimusalim
JF-Expert Member
- Jun 17, 2014
- 1,822
- 499
Jina lake halisi ni Mohamed Emwazi ni kijana wa umri 26 ni raia wa uwingereza aliekulia kuwait na kupata elimu yake ya shahada ya kompyuta uko kabla ya kurudi Uingereza, kwa mujibu wa majarida mbali mbali yamemtaja mtu huyu ndio katili zaidi duniani, akijulikana kama Jihad John. Ndani ya kundi la IS amekuwa akitekeleza mauaji kwa kuwakata vichwa mateka wa mataifa mabalimbali, hawa ni miongoni mwa mateka aliowakata vichwa kwa mkono wake
Akiwa huko alipopata elimu yake Kuwait, alikuwa mtoto mwenye nidhamu, mpole na uwezo wa akili sana darasani, kwa mujibu wa walimu na rafiki yake (class mate) ambae hakutaka jina lake litajwe.
Mama yake alipohojiwa kutoka nyumbani kwake alidai mtoto wake mara ya mwisho alimpigia simu 2013 kwamba alielekea Syria kujiunga na mashirika ya kujitolea ya kibinadamu.
Haya ni makazi ya familia ya Mohamedi Emwazi huko Uingereza
Mama yake aliongeza kuwa aligundua mwanae kajiunga na kundi hilo hatari duniani pale alipoigundua sauti yake katika video ya mateka iliotolewa na kundi hilo mwanzoni mwa mwaka 2014, mtu huyu anaetafutwa na mataifa makubwa hapa duniani, Marekani imetoa dau la US Dollar milioni mia 700 kwa ataefanikisha kukamwatwa kwa IS executioner huyu, pia inasemekana kwamba mwishoni mwa mwaka 2009 aliwahi kutembelea nchi mojawapo ya Afrika Mashariki kwa mujibu wa data za kiusalama
Katili huyu hajaoa, pia si muumini wa dini ya Uislam ingawa hupendelea kuvaa mavazi yake
Kwa munibu wa mama yake alipohojiwa kutoka makazi yake