Mtu kama huyu, wewe utamjibu vipi?

Mtu kama huyu, wewe utamjibu vipi?

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
19,370
Reaction score
14,522
Hivi mambo mengine ya ajabu kwelikweli, unakuta mtu anakupigia simu usiku wa manane halafu anakuuliza, hivi umelala? Mimi huwa nawajibu hapana, nipo nje ninaota jua.

Sijui wewe utamjibu au huwa unamjibu vipi mtu wa namna hiyo?
 
Hapana kuna mjinga mmoja namsoma jamiiforums
 
Kumbe hujaenda shule bhana!! Vingine muwe mnauliza maana yake sio unakurupuka kuleta ujinga ujinga hapa
Kasome kiswahili form 3 na utajua hiyo ni mini
Tashtiti,takriri.....utajua huko
Unakutana na mtu njiani anakuuliza aaah upo ndugu yangu? Na anakuona hapo.

Sasa wewe hapo utaona ajabu kumbe kawaida tu ndio kiswahili hicho
 
Mkuu nashukuru kwa majibu yako mazuri!,lkn mkuu wewe kumwelekeza mtu pasipo kumtukana huwezi?.
 
Jibu lako sahihi kama wewe sio mlinzi wa zamu
 
Back
Top Bottom