Mtu anayeharisha anaweza kutumia soda?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,323
12,878
Habarini wakuu. Kumekuwa na imani potofu kuwa mtu anayeharisha hatakiwi kutumia vitu kama soda na juisi. Utasikia, "Usimpe soda huyo anaharisha."

Ukweli ni kinyume chake. Mtu anayeharisha anapoteza madini nw maji mengi sana. Na mara nyingi hii ndiyo hupelekea kufa, hasa kwa watoto. Kwa hiyo mtu anayeharisha anatakiwa kurudishiwa maji na chumvi anazopoteza kwa njia yoyote ile. Kama ni "Oral", juisi, soda nk nk.

Kwa hiyo basi, mtu anayeharisha inashauriwa apewe soda. Na si kumkataza kama ilivyozoeleka.
 
Habari!
Katika aina za kuharisha, kuna aina moja inaitwa "Osmotic diarrhea".

Wakati mtu ana shida ya kuharisha hasa watoto, huwa kuna shida ya mfumo wa tumbo kufyonza kwa ukamilifu viinilishe ikiwemi sukari.

Hii huweza kutokana na uharibifu mwenye mfumo wa tumbo pamoja na transient period/muda unaochukua chakula kusafiri toka mwanzo mpaka mwisho wa njia ya chakula kuwa mfupi. Hivyo material mengi ikiwemo sukari huwa ni rahisi kupitiliza mpaka kwenye eneo la mwisho la njia ya chakula.

Hapo mwili hichukua jukumu la kulinganisha kilichoko kwenye mwili dhidi ya kilichoko kwenye material yaliyoko kwenye njia ya chakula.

Kwa kuwa kutakuwa na uwezekano wa kuwa na sukari nyingi/concentration gradient basi maji huvutwa kutoka mwilini na kuingia kwenye mfumo wa chakula na kusababisha maji kuwa mengi "Osmotic diarrhoea."

Hii ndo huleta sababu husika na Oral Rehydration Salts (ORS), kuwa na kiasi tajwa cha chumvi na sukari.

Hivyo, agizo hilo huwa ni sahihi.
 
Back
Top Bottom