Mtu anaishi baada ya kufa?

Mnyazi Mungu anaowachukia ghalfa vifo manake hawapendi?
Na je wasioenda church au hawajui habari hizi za Jesus nafasi yao ikoje kwa hili?
Kama kila mtu angekua akiumwa anajua atattubu kwa ivo afanye maovu tu duniani?
 
Mnyazi Mungu anaowachukia ghalfa vifo manake hawapendi?
Na je wasioenda church au hawajui habari hizi za Jesus nafasi yao ikoje kwa hili?
Kama kila mtu angekua akiumwa anajua atattubu kwa ivo afanye maovu tu duniani?
Usipo mjua Yesu mbingu anza kujenga yako tena mjiunge kakikundi kabisa.. Ila ukimuamini Basi mbingu yakwako..hushauriwi kuwa mwovu ila ukiwamwisho Wa uhai ukatubu na kukiri Yesu Basi umeponea chupuchupu kuingia motoni ila nje ya hapo kwny msiba waasie amini itabidi wachungaji au mapadre wadanganye sana wakialikwa mazishini hapo
 
Mnyazi Mungu anaowachukia ghalfa vifo manake hawapendi?
Na je wasioenda church au hawajui habari hizi za Jesus nafasi yao ikoje kwa hili?
Kama kila mtu angekua akiumwa anajua atattubu kwa ivo afanye maovu tu duniani?
Mkuu swala la wokovu ni tofauti kabisa na fikra za kibinadamu ni tofaut kabisa na kuhudhiria kanisan ama msikitini ni tofaut kabisa na kuwa kiongozi wa dini , ni mahusiano yako na Mungu ndani kabisa ya Moyo wako boss, kinachoangaliwa ni Nia ya dhati ya toba basi, na sio toba ya juu juu , toba ya that ya Moyo na kusikitikia maovu .... Kwa sababu moyo ( hapa nazungumzia mindset sio Moyo nyama inayodunda) ndo unaotamka hvyo huwez kudanganya .....

Mkuu ukianza kusema fulan aliua , sjui fulan alifanya hivi ...yaan hata wewe hapo Mungu angekuwa na Akli kama zetu usingekuwepo ,mana umefanya maovu mengi sema Tu Kwa vile hauna popularity ndo mana wanazengo hatuhajui na hata tukiyajua hayawezi kutupotezea mda .....

Nakupa mfano mmoja wa kwenye biblia ndo ujue sasa calculation za Mungu ni amazing.... Mfalme Manase ni moja ya wafalme waovu kuwahi kutokea , inasemekana jamaa alifikia hatua ya kufanya uzinzi kwenye hekalu , anaanzisha ibada ya mashetani , nabii isaya alipomkemea mfalme manase alimkamata na kumuua , .... Na jamaa akatawala mda mrefu kuliko hata mfalme mwema Daudi , zaidi ya miaka 50 jamaa lipo Ikulu na maovu yake ....

Mwisho ufalme ukashambuliwa na maadui mshikaji akakamatwa i , akateswa Sana...akiwa gerezani akamrudia Mungu , jamaa akaomba aisee , biblia inatamaka wazi kabisa kwamba Mungu akamsikia .... Manase alikufa akiwa na Tumaini la wokovu , jiulize sasa mtu aliyefanya maovu vile but with in a second anarudi kwenye mstari....

Tuachane na huyo Yule mwizi msalabani , dk ya mwisho kabisa jamaa anasepa .....
 
Unakua malaika na kama kuna maombi uliyapeleka katika idara yao ya uajiri unaweza kufikiriwa.
 
Umenena yananiingia kwa mbali!
 
Nafsi = Roho , nimeelewa hivo

Nafsi haifi, ndio maana huwa tuna sema Mwili wa ..........., hapo inatajwa nafsi ake aliyetutoka kimwili,

Roho iiradhi lkn mwili hauko tayari !!!

Je
1. Ni kweli Roho =/= Nafsi ?

2. Roho = Nafsi ?

Kwa mujibu wa Mleta maada nimeelewa kwamba Nafsi ni Roho.
 
Mambo ya hukumu mwachieni mwenye kutoa hukumu.

Suala la nani ataenda mbinguni na nani hataenda si lako.

Ww hubiri usitoe hongo ya mbingu na kutishia watu moto ili wawe upande wako.

Dunia ina watu b7 au 8b na wote wana miongozo tofauti ya namna ya kwenda mbinguni na wanavitabu vitakatifu.
 
Nimesema ukweli hata sija hukumu. Wala sijatishia ila nilichosema nikweli. Kuamini niuamuzi wako MTU binafsi nakama unadhani mtuakisema ukishika moto utaungua kama utahisi nivitisho wewe shika hapa lazima ukweli tuambiane bila haya
 
Unaruhusa kamili ya kuchangia maoni yako ila sio umuelekeze MTU Fulani na nimetoa mada hiyo kuwa eleza ukweli ulivyo kuepukka false doctrine za wapotoshaji..
Sawa vipi kama hoja yako ndio false doctrine?
 
Jf nowdays....

Ume uliza swali au umetoa conclusion?

Nilidhani unakaribisha watu kwenye mjadala wa kujibu swali lako

Ungepata mchango mzuri Wenda kuliko hicho ulichoandika hapo
Nimeshindwa Hata kuendelea kuisoma article yake'
 
Sawa vipi kama hoja yako ndio false doctrine?
Leta hoja yako kama umeshindwa Basi..maana najua watu wajamii yako mpo wengi sana nanafahamu huwa mnaongea nini kwenye hoja zenu maana hamna point zamaana ila mnakawaida ya kuegemea kwenye dini zenu na ndio maana niliandika kwa mfumo wakuzuia watu kama wewe na kundi lako
 
Nimeshindwa Hata kuendelea kuisoma article yake'
Kwasababu haiendani na false doctrine uliyokwisha mezeshwa na hutaki kusikia zaidi kalili ghost boss usisome maandiko yangu wala Ku reply
 
Haraka ya Nini kwa kuwa kifo ni kitu ambacho hakiepukiki, Sote tutakufa siku moja na tutakuwa na majibu sahihi kabisa...
Majadiliano hayabadilishi nadhalia ya uhalisia wa Kifo, Ila kikubwa Ni kuweka uhusiano mzuri na MUNGU, Kutenda mema, Kuwa na mahusiano mazuri na Binadamu wenzako, upendo husio na unafki na kuwajali maskini...!!!
 
Kwahy roho za wanyama znaendaga wp
 
Nini tofauti kati ya roho na nafsi mkuu?
 
Sheria ipo hivi ili usamehewe ni lazima utubu hadharani mbele za hao uliowafanyia dhambi ili zisafishwe kabla hujaitwa rasmi na islael mtoa roho... huwezi kujifungia ndani ukamwita paroko eti unatubu - hiyo haipo..

Refer Mfalme Daudi baada ya kumuua askari mtiifu kisa tu eti amwoe mkewe nini alikifanya ili kupata msahama wa dhambi..

Sheria bado ni zilezile hazijabadilika... Jiulize ni wangapi wanalia kwa mabaya aliyowafanyia mwendazake tena bila ya hatia...
 
Yeye amepata bahati na upendeleo wa Mungu kwa kweli.....

Mara Paap tuliobaki tunakufa halafu unamkuta mlangoni yeye ndio anakuonyesha pa kukaa πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
Hapo kinakuwa kimeumana..🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…