Jamani kwani hamjui hiyo ndiyo motive number moja ya wadada, Ila siyo wote lasivyo nitauwawa hapa na nitakuwa nakosea wale ambao hawako hivyo. Nimewahi kuwa na girl friend huu...unajua maana ya kila siku anaomaba hela. Samahani wadada mtaona kama nawasema vibaya lkn huyo alizidi. Mnajua maana ya kila siku..ukimpa leo kesho anakuja na excuses nyingine na sio elfu kumi. Atakupa tatizo kuanzia hamsini, laki etc Nilishindwa kwa kweli. Nikawa najiuliza ana matatizo gani? Mwisho nilijua hakuna upendo yeye anachojua ni pesa tuu. Nilimwambia ukweli kuwa hapana imekuwa too much hizo hela anataka kila siku anapeleka wapi???? aliuchuna kama siku mbili hivi ya tatu kaanza tena. Hapo ndipo nilipomwambia basi siwezi nikamtosheleza na pesa nilizo nazo. Akabaki kuwa rafiki wa kwenye internet tuu basi. Ila hajaacha siku mojamoja ananichomekeaga, najifanya kama sijaona hiyo message.