Mtu 1 afariki dunia huku 30 wakijeruhiwa kwenye vurugu uwanja wa mkapa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Taarifa ya Awali Kuhusu Majeruhi Mkapa Stadium DSM. Hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea Majeruhi 30 ambapo 1 amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40.

20230528_144039.jpg

Majeruhi wengi wanaendelea vizuri wana majereha madogomadogo, wanaendelea na vipimo. Aidha timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa DSM ipo uwanjani, inafuatilia kwa karibu kuangalia kama kuna majeruhi wengine.

Timu ya Wataalam wa Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa Temeke na wapo standby kupokea na Kuwahudumia.

Majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi.

Pia, Soma: Mashabiki wavunja mageti uwanja wa Benjamin Mkapa
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu @ummymwalimu ametoa taarifa ya awali kuhusu majeruhi Mkapa Stadium Dar es salaam ambapo amesema hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea majeruhi 30 ambapo Mwanaume mmoja mwenye umri wa takribani miaka 40 amefariki.

Ummy amesema “Majeruhi wengi wanaendelea vizuri wana majereha madogomadogo, wanaendelea na vipimo, aidha Timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ipo uwanjani, inafuatilia kwa karibu kuangalia kama kuna majeruhi wengine”

Japokuwa Wizara ya Afya haijasema Mtu huyo alifariki katika mazingira yapi, baadhi ya Mashabiki leo kabla ya mechi kuanza walionekana wakiruka fensi kuingia uwanjani hapo huku wengine wakiingia kwa kusukumana kupitia moja ya mageti ya Uwanja huo. #
 
Inawezekana kuna watu wengi zaidi wamefariki..
Hakika uongozi wa uwanja Una kesi ya kujibu
 
UMMY MWALIMU : MMOJA AFARIKI KWA MKAPA , MAJERUHI 30 =Siasa kwenye mpira.​

Back
Top Bottom