Mtoto wa Wassira ajiunga Chadema

Huyo sio mtoto wa Steven Wasira. Kalaga baho.

Mtoto wa kaka yake bila shaka? maana si unajua tena mtu anataka ajinadi kupitia jina maana huwa watu wanateleza kwa kuchagua jina la ukoo bila kuangalia uwezo wa kuongoza
 
Karibu sana kamanda. Chadema mwendo mdundo, maamuzi yako ni ya hekima sana. Vua gamba vaa gwanda.
 
Mtoto wa kaka yake bila shaka? maana si unajua tena mtu anataka ajinadi kupitia jina maana huwa watu wanateleza kwa kuchagua jina la ukoo bila kuangalia uwezo wa kuongoza

Kijana amejiunga CDM kachukua tu kadi kawa mwanachama ni haki yake ya kikatiba.
 

Mfano mzuri kabisa kwani hamuwezi wote mkawa manafanana mawazo na ukiona hivyo ujue kuna mtu kai azima akili kwa mwenzake yaani kwa yule mwenye wazo. Mwenye mawazo independent ni mtu ambaye anajitambua na anaweza fika kule Mungu alikopanga afike kwani si tegemezi kwa mwanadamu mwenzake.

Mungu mwenyewe katuumba hatufanani vipi wewe uwe unakubali kila unachoambiwa bila kuangalia ni vipi hicho kinaendana na vision yako katika maisha?
 
Historia inatuambia kuwa Wassira aliwahi kujinga na chama cha upinzani (NCCR MAGEUZI).Pengine siku za mwisho za CCM zikikaribia anaweza kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Mkuu kwa kuweka tu kumbukumbu sahihi ni kwamba wasira amesha wahi kuwa mwanachama wa chadema na ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho ambao wako wenye list ya waasisi. Kama utakumbuka kamanda Mbowe alimtaja kwenye msiba wa Bob Makani baada ya katibu wa magamba kuleta uzushi kuhusu uongozi wa chadema.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Nimefurahi sana kwani baada ya kusoma thread hii nimegundua vijana w CDM ni makini sana wanahofu sana juu ya uasi.
 

Mkuu, hapa hujaweka kumbukumbu sawa! Ndio kwanza umeziapotosha. Kumbukumbu zinaonesha kwamba mmoja wa waasisi wa cdm ni George Wassira na si vinginevyo!
 
Usikute katumwa.....hhahaaha
hata kama katumwa CHADEMA ipo imara kila idara angalia inavyo washughulikia madiwani wake ndumila kuwili

jambo la msingi mi naona ni bora tumpe muda tusimhukumu mapema kwa dhamana ya babaye
 
Kama si mpango mkakati basi saa hii wasira kapandwa na pressure
 
Huyo sio mtoto wa Steven Wasira. Kalaga baho.
Kama si mtoto wa Wassira ni mtoto wa nani? Ukweli unasimama ni mtoto wa Wassira na ndugu zake wote watavua magamba pia
 
Hawa Chadema ni kuokoteza watoto wa vigogo tu sasa

Ukitaka na wewe unajitokeza kama una sifa na uwezo wa kukabiliana na mikiki ya siasa hakuna mashaka. Kwa watanzania wa sasa wala hawana mashaka na mtu kuwa mtoto wa kigogo kwani wanaufahamu wa kutosha na bado watafahamishwa zaidi, kujiunga kwake haimaanishi ndiyo mambo mswano, ataendelea kuwa subject to public trust mpaka ajijengee jina na sifa ya kuwa mzalendo wa kweli pamoja ansomeshwa kwa kodi yangu huko marekani.:frusty:
 
Hawa watu hawaaminiki. Baba yake alikuwa NCCR-Mageuzi, leo yuko wapi? Makongoro Nyerere alikuwa NCCR-Mageuzi, leo yuko wapi? Tuwe makini ni watu hawa.
 
Huenda huyu mtoto akagombea ubunge wa Bunda kwa tiketi ya CDM. Kila la heri Wassira Jr. Kumbuka mzee alishawahi kuwa NCCR-MAGEUZI
 

Wassira mwenyewe alikuwa CHADEMA au mmesahau?

Huyo mwache huko akikuwa ataacha. "Mtoto akililia wembe"
 
Si kujiunga tu, alikuwa mbunge kupitia NCCR Mageuzi, alimbwaga mzee wa tume ya katiba Warioba aliyegombea kupitia CCM
Wasira ni moja ya waasisi wa chadema, badaye alihamia NCCR na kugombea ubunge, alishindwa na Warioba akafdungua kesi wakambwaga, njaa ilipozidi kahamia CCM na kugombea ubunge na kuwa mbunge hadi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…