Ngongoseke
JF-Expert Member
- Jan 1, 2012
- 3,202
- 1,464
Hawa Chadema ni kuokoteza watoto wa vigogo tu sasa
wanaomfahmu zaidi tujuzeni maana lisije kuwa pandikizi tu
Ni mtoto wa Tyson Wasira huyu?
Nawasubiri rafiki zangu Ridhiwani Kikwete, Januari Makamba, Wiliam Malecela nk. Salama yao ni kuokoka mapema, ukombozi u mbele yao tu.
Historia inatuambia kuwa Wassira aliwahi kujinga na chama cha upinzani (NCCR MAGEUZI).Pengine siku za mwisho za CCM zikikaribia anaweza kuwa mwanachama wa CHADEMA.
Stephen Wassira hafai kwa lolote. Hata akisafishwa, hasafishiki. Siku akiingia CDM, na akakubaliwa, ndipo nitakapojiridhisha kuwa CDM tumekuwa vilaza wa kufikiri. HIVI WASIRA AKIJA CHADEMA, TUTAMPA KAZI GANI?
Kwa jinsi Wasira anavyochukia upinzani sidhani kama hakuna mchezo mchafu unaotaka kuchezwa hapo. Kumbuka hata baba yake aliwahi kutumika kama mamluki ili akavuruge upinzani
Unamkumbuka Madaraka Nyerere ambaye ni kifungua mimba alipoenda kuwa mwanachama na mbunge kupitia chama cha upinzani wakati Nyerere babake akiwa hai. Madaraka Nyerere alikuwa mbunge huko Arusha kama sijachanganya kupitia NCCR Mageuzi wakati mzee wa Kiraracha (nji hii) aka Lyatonga Mrema alipoiteka Tanzania na kuitetemesha CCM kutokana na kosa la Mwinyi kumwengu kwa sababu ya kutowajibika pamoja kwa malengo ya kulindana.
mkuu .... correction .... alikuwa ni Makongoro Nyerere .... ambaye sasa ni ubunge wa East Africa legislative assembly
May be huyo ndo katumwaa kuja kukakamilisha kale ka mradi ka kuisambaratisha CDM before mwaka kuisha.
Si sahihi kumhukumu kijana huyu na hata wengine watakaojitokeza kujiunga na CHADEMA kwa makosa ya wazazi au wanafamilia zao. Steven Wassira anafahamika kwa political opportunist behavior yake na kinachomuweka CCM sasa hivi ni mkate anaopata kutokana na cheo alichohongwa na kina Makamba ili abaki huko. Hana msimamo na ni Political harlot ambaye bei yake huamuliwa na njaa yake. Wanaojidanganya ana mapenzi ya kweli na CCM wajaribu wamuengue kwenye shibe waone rangi yake halisi.Historia inatuambia kuwa Wassira aliwahi kujinga na chama cha upinzani (NCCR MAGEUZI).Pengine siku za mwisho za CCM zikikaribia anaweza kuwa mwanachama wa CHADEMA.
Ni mtoto wa Tyson Wasira huyu?
Zaidi ya kuwa mtoto wa Wasira sidhani kama ana nguvu kwenye chama kilichomtuma kwani kama baba yake anaaminika na ana nguvu kwenye chama chake sidhani kama mtoto ana nguvu kivile (kwa kesi hii MTOTO WA NYOKA SI NYOKA)