Mtoto wa Rais Banda afungwa jela

Mtoto wa Rais Banda afungwa jela

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
andrew_banda.jpg

​


Lusaka. Mtoto wa Rais wa zamani wa Zambia, Andrew Banda amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kutiwa hatiani katika makosa ya kuhusika na rushwa.

Andrew (53), mtoto wa aliyekuwa Rais Rupiah Banda pia aliwahi kuwa mwanadiplomasia, alikamatwa mwaka 2012 akidaiwa kupokea rushwa kutoka kwa Kampuni ya Fratelli Locci ya Italia iliyopewa zabuni ya ujenzi wa barabara.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Joshua Banda alisema kwamba amezingatia maelezo yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka kwamba mtuhumiwa huyo ndiye mhusika mkuu katika kosa hilo la kudai na kupokea rushwa, lakini ni mara yake ya kwanza kutiwa nguvuni.

Alisema kutokana na hali hiyo, ameona ni vyema kuangalia namna ya kumpunguzia adhabu na hivyo kumhukumu kifungo cha miezi 24 jela, lakini pia akipewa haki yake ya msingi ya kukata rufaa.

Mahakama pia ilimtia hatiani kwa kushindwa kueleza kuhusu namna alivyozipata zaidi ya Dola 63,000 zilizokuwa kwenye akaunti yake, ambazo zinadhaniwa zilipatikana kwa njia zisizokuwa halali.

Banda, naibu balozi wa zamani wa nchi hiyo nchini India na aliyewahi kuwa katibu mkuu wa ubalozi wa Zambia nchini Italia ni mmoja miongoni mwa maofisa wengi kutoka katika utawala wa baba yake walioshtakiwa kwa kujihusisha na rushwa baada ya kampeni maalumu ya kupambana na rushwa inayoongozwa na Rais wa sasa, Michael Sata.

Chanzo: Mwanachi
 
Ridhimoko na yeye yu mbioni pamoja na deal zake za madawa ya kulevya na mambo na kuihujumu nchi kwa miradi ya gas hii.
 
wacha wakamatwe wanadhani kwa kuwa baba zao wana mamlaka basi wapo juu ya sheria
 
cc Ritz

ukiona mwenzio ananyolewa kavukavu wewe tia maji fasta.
 
Last edited by a moderator:
Da safi sana na sisi Tz inabidi tumpate Rais mwenye sifa kama za sata ili awawajibishe watu kama ridhiwani Pamoja na baba yake
 
Lusaka, Sunday. Zambian ex-diplomat and son of former president Rupiah Banda was on Friday sentenced to two years in prison after being found guilty of corruption.


Andrew Banda, 53, was arrested in 2012 on charges of soliciting a kickback from Italian company Fratelli Locci, which was awarded a contract to build roads.

In passing the sentence, Magistrate Joshua Banda said he had considered mitigation presented by the defence that the accused was a first time offender.

But he said a “custodial sentence” was necessary and “therefore I sentence the accused to 24 months effective today, but both parties are at liberty to appeal.”

The court also found him guilty of failing to account for 360,000 kwacha, about 63,000 dollars/46,000 euros, found in his possession, which is suspected to have been proceeds of criminal activities.

Banda, a former deputy high commissioner to India and former first secretary at Zambia’s mission in Italy, is one of the many officials from Banda’s administration charged with graft, in a massive clean-up campaign launched by President Michael Sata after he came to power in 2011.

His father, the former president, is also facing corruption charges.


The Sata administration had also tried to implicate another of ex-president Banda’s sons, Henry.

It had reported Henry, who is based in South Africa, to Interpol, but it was unclear why
 
Back
Top Bottom