Mtoto wa rais anaswa akipima 'ngoma'

Mtoto wa rais anaswa akipima 'ngoma'

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
ngomanoma.jpg

  • Posted by GLOBAL on February 20, 2014 at 7:30am
  • View Blog

mtotowarais1.jpg

Na Issa Mnally

MTOTO wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Salmin Amour aitwaye Amini Salmin, Februari 14 mwaka huu alinaswa akipima Ugonjwa wa Ukimwi ‘ngoma' katika kituo cha ushauri nasaa cha AMREF Makao Makuu kilichopo Upanga, jijini Dar, Amani linakujuza.

mtotowarais2.jpg
Mwandishi wetu alimshuhudia Amini akiwa katika kituo hicho kupima ugonjwa huo katika siku hiyo ambayo huadhimishwa kama Siku ya Wapendanao ‘Valentine's Day' ili kutaka kujua afya yake na kuwa tayari majibu yake yawekwe hadharani.

mtotowarais4.jpg

Hata hivyo, baada ya vipimo na kutakiwa kusubiri majibu, Amini alionekana kuwa mnyonge na mwenye mawazo mengi ingawaje aliweza kujifariji kwa kuangalia runinga iliyopo katika chumba cha kusubiria majibu.

mtotowarais6.jpg

Alipoitwa kwenda kupatiwa majibu yake alijikuta akijikwaa zaidi ya mara tatu na alipoingia chumba cha majibu, nusura adondoke baada ya kujikwaa tena katika kizingiti cha mlango wa kuingia kwa daktari.

mtotowarais8.jpg

Mara baada ya kupewa majibu yake, Amin alisema amechukua uamuzi wa kuijua afya yake siku hiyo kwa sababu vijana wengi huitumia kwa ajili ya kufanya ngono katika nyumba za kulala wageni.
mtotowarais8.jpg
"Nimeamua kupima Ukimwi leo kwa sababu vijana wengi wamepanga kukutana na mpenzi wao kwa lengo la kufanya ngono," alisema Amini ambaye alionekana kuwa na furaha baada ya kupata majibu mazuri.
mtotowarais7.jpg

Kipi kitu cha ajabu hapa? Kupima H.I.V kwa mtoto wa rais au nini?
Unaposema kabambwa yaani ni kama vile una maanisha kuna kundi maalum la watu wao kupima ndo halali wengine si halali.
 
Mkuu ndo udaku huo kama ulikuwa hujui.
 
Huyu jamaa alishapima kimya kimya jana yake, then akawaita waandishi waje wampige picha wakati wa kupima (siasa hizi)!

Hizi picha zinaoneka ni za kuarifiana, kwa sababu pia vyumba viko closed, mtu hawezi kupiga picha kimya kimya bila kuonekana.
 
kwa hiyo kupima ukimwi kwani ni tatizo ni moja wa kujua afya yako alafu mwandishi utafikiri alialikwa kwenda kupiga picha watanzania tumekalia ujinga tu lakini nijuavyo kupima ni siri ya mtu
 
Haya magazeti na mitandao uchwara bana...
 
Huyu jamaa alishapima kimya kimya jana yake, then akawaita waandishi waje wampige picha wakati wa kupima (siasa hizi)!

Hizi picha zinaoneka ni za kuarifiana, kwa sababu pia vyumba viko closed, mtu hawezi kupiga picha kimya kimya bila kuonekana.

umeona eeeeh
 
Huyo mama hapo pembeni nae ameomba coverage? Mtashtakiwa mshindwe kulipa nyie wauza maneno!
 
View attachment 142661

  • Posted by GLOBAL on February 20, 2014 at 7:30am
  • View Blog

View attachment 142662

Na Issa Mnally

MTOTO wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Salmin Amour aitwaye Amini Salmin, Februari 14 mwaka huu alinaswa akipima Ugonjwa wa Ukimwi ‘ngoma' katika kituo cha ushauri nasaa cha AMREF Makao Makuu kilichopo Upanga, jijini Dar, Amani linakujuza.

View attachment 142663
Mwandishi wetu alimshuhudia Amini akiwa katika kituo hicho kupima ugonjwa huo katika siku hiyo ambayo huadhimishwa kama Siku ya Wapendanao ‘Valentine's Day' ili kutaka kujua afya yake na kuwa tayari majibu yake yawekwe hadharani.

View attachment 142664

Hata hivyo, baada ya vipimo na kutakiwa kusubiri majibu, Amini alionekana kuwa mnyonge na mwenye mawazo mengi ingawaje aliweza kujifariji kwa kuangalia runinga iliyopo katika chumba cha kusubiria majibu.

View attachment 142665

Alipoitwa kwenda kupatiwa majibu yake alijikuta akijikwaa zaidi ya mara tatu na alipoingia chumba cha majibu, nusura adondoke baada ya kujikwaa tena katika kizingiti cha mlango wa kuingia kwa daktari.

View attachment 142666

Mara baada ya kupewa majibu yake, Amin alisema amechukua uamuzi wa kuijua afya yake siku hiyo kwa sababu vijana wengi huitumia kwa ajili ya kufanya ngono katika nyumba za kulala wageni.
mtotowarais8.jpg
"Nimeamua kupima Ukimwi leo kwa sababu vijana wengi wamepanga kukutana na mpenzi wao kwa lengo la kufanya ngono," alisema Amini ambaye alionekana kuwa na furaha baada ya kupata majibu mazuri.
mtotowarais7.jpg

Hii nayo ni habari?
 
Huu ni upuuzi,kanaswa au anajitangaza kuwa kapima ngoma??!! AMREFU pale unapewa huduma kwenye chumba peke yako/partner wako chenye privacy ya kutosha sasa haya mapicha na maneno ya kubambwa ni upuuzi na upumbavu tu!!
 
Tatizo liko wapi? Hivi vijarida ndio vinafanya takwimu sahihi zikosekane, kwa watu kuhofia kuonwa.....Sasa tatizo liko wapi hapo? Si bora huyo, je mwandishi wa habari hii yeye kapata ujasiri wa kupima?
 
Huu ni umbea! So ukitaka asipime au? Nyinyi kila kitu mnabwata, akienda kupimia nje ya nchi unalalama tena wasipopima utadai hauoneshwi mfano. Haya mambo peleka huko huko global publ., na sio hapa umbea stop!
 
Back
Top Bottom