Wa Mjengoni
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 480
- 128
Napenda wenye ufahamu wanisaidie kuhusu hili.
Nina mke wangu wa ndoa ambaye kabla sijamuoa nilimkuta na mtoto wa kiume wa miaka mitatu, mtoto huyo sasa hivi mkubwa na ameingia form one sekondari.
Mtoto huyu ana baba yake ambaye ni mtu mwenye uwezo mkubwa tu, lakini kutokana na jeuri ya mama yake (mke wangu) hataki kumshirikisha mtoto upande wa babake kwa jambo lolote, yaani hataki hata mtoto ajue kuna babake. Ada ya shule silipi mimi ila mjomba wa mtoto yaani kaka wa mke wangu.
Chakula, mavazi, uniform, nauli ya kwenda shule ya boarding na matumizi ya shule vyote natoa mimi.
Katika kukorofishana baada ya yeye kukataa kunipigia pasi nguo zangu kwa madai kupiga pasi ni option tu hufanyika akipenda yeye sio lazima na mimi nikamjibu ku supply education materials kwa mwanao ni option tu sio lazima kwani mtoto huyo ana baba yake aliye hai , labda asingekuwa naye (amekufa) ndo ingekuwa lazima!
Niliongeza kuwa wajibu wangu kwa mtoto wake huyo ni kumpa chakula ale na kumpa malazi alale tu na sio vitu vingine.
Swali langu sheria inasemaje kuhusu wajibu wetu kwetu sisi akina baba wenye watoto wa aina hii?