Mtoto wa mjini Ndiye Mshamba wa mwisho mjini

Mtoto wa mjini Ndiye Mshamba wa mwisho mjini

Kuna ubaya gani mtu aliyezaliwa kirumba pale akijisifia na mwanza yake,mtu aliyezaliwa mbeya akijivunia mbeya yake au mchaga akijisifu na moshi town yake sasa ulitaka ajisifie wapi wakati huko kwingine hajawah hata kufika tatizo akijisifia mtoto wa dar ohh mbona huna kitu jaman kupata majaliwa mbona drogba kawa tajiri london na kuna borntown wa pale wanafagia barabara tu,ila seriously asilimia kubwa ya waliokuja mjini ukubwani hata awe na hela au elimu vp kuna kaushamba fulani hakiwatoki
 
mi nimelishuhudia kwa wazazi wangu baba alitokea kijijini haswa ila mama wa town sasa unakuta wanavyobehave ni tofauti mzee sasa hivi anazo kidogo basi unakuta anamiliki hata simu 5 kwa mpigo anaenda kula bata kwenye mahotel utamsikia anasema nilipata shida sana acha niwe navipiga na mimi lakini mama hata hana tyme ukimuuliza vipi anakwambia mi disco sijui hotel nimeenda sana kwenye ujana wangu tena la kuaga wazazi kabisa sio kama mzee ilikuwa ni zambi kwa babu yetu asikie mwanae kaenda disco basi leo mzee mungu kamjalia vijicent tabu tupu
 
Back
Top Bottom