Mtoto wa miezi sita hajaanza kusimama!

Charliemic

JF-Expert Member
Feb 17, 2019
585
919
Wakuu habarini!

Naomba mnijuze, huyu mtoto ana miezi sita hajaanza kutambaa! Kinachonishangaza ni kuwa anajitahidi kutaka kusimama! Akijishikilia na kitu chochote basi anajitahidi asimame! Je hii ni jambo la kawaida!?
 
Wapo watoto wanaoanza kusimama kabla hata ya kutambaa so ni jambo la kawaidaa..!! Ingekuwa ukimuweka mahali hamove kabisaa ingekuwa dalili mbayaa
 
...Miezi sita siyo umri sahihi wakuanza kuhoji matukio ktk ukuaji wa mtoto msichojua hali hii huwasababishia wazazi wengi kuwatia vilema vya matege watoto wao pale wanapoanza kuwasimamisha kabla ya wakati wao.

Mtoto huanza kufanya mazoezi ya kujitegemea anapokuwa na miezi 7>7½ kuendelea na huanza kusimama au kutambaa akiwa na miezi 9/10 kwa baadhi 11 wapo wanaofikisha hata mwaka hawajaweza kusimama bila kujishikiza kitu, mwacheni mtoto mwili wake uamue mabadiliko unayoyataka muhimu mama yake akishamuogesha amnyooshe viungo,miguu mikono mgongoni na kwenye mapaja kwa mafuta ili hivi viungo viwe active mtoto atakapoanza mazoezi mbalimbali ya ukuaji wake.
 
...Miezi sita siyo umri sahihi wakuanza kuhoji matukio ktk ukuaji wa mtoto msichojua hali hii huwasababishia wazazi wengi kuwatia vilema vya matege watoto wao pale wanapoanza kuwasimamisha kabla ya wakati wao...
Sijui haujaelewa ama sijui upo kwenye lile kundi la much know au bush lawyer, anyway ukitaka kushauri andika bila kujitia ujuaji!

Nilichokisema huyu dogo hakuna anayemsimamisha bali akipata sehemu akajishika anastruggle kujiinua na kusimama!
 
Mleta mada huu ushauri wa mchangiaji usiubeze japo ni mgumu kuuelewa. Kitabibu haswa kiasili usiwe na hofu sana atakuja kutembea.. Kuwa na muda nae msaidie kutembea kwa mazoezi madogo na mafupi/Panga ratiba kila siku huko Tza mnahita Mama Cheza basi kwa uwezi wa Mwenyezi Mungu atatembea tuu..
 
Mkuu naomba urudie tena kusoma uzi kule juu
 
Wakuu habarini!

Naomba mnijuze, huyu mtoto ana miezi sita hajaanza kutambaa! Kinachonishangaza ni kuwa anajitahidi kutaka kusimama! Akijishikilia na kitu chochote basi anajitahidi asimame! Je hii ni jambo la kawaida!?
Ni kawaida sana. Kuna watoto wanaruka stages hasa wakiwa na afya nzuri bila kuuguaugua huwa wanasimama na kuondoka mazima kama gari. Huyo atatembea na miezi 8 au 9.
 
Yaani huyu atatembea haraka mno. Yeye hataki kukaa chini. Kuna mtoto wangu mmoja miaka hiyo hata baby walker hakuna. Alianza kutaka kuisimama mapema mno. Mama yake alikuwa akimbeba mkononi yeye anapambana kuisimamia. Alipofikisha miezi 5 akawa anasimamia stuli ndogo halafu anachezea na kurusha Mguu mmoja mmoja. Tulikuwa na hofu sana hasa kuanguka au kuwa matege. Hakika miezi 6 alianza kuhama stuli moja kwenda nyingine na kukamata meza.

Alidumu hivyo kwa mwezi mzima. Alipotimiza miezi 7 na wiki 1 siku tukiwa kazini tunarudi home tukaambiwa alitembea na kuanguka ila hakuumia. Basi mama yake akamchukua akamnyonyesha akamuweka chini akasimamia meza na akatembea kuja kwangu kama steps 5 bila kuanguks ila kwa speed. Tukamshangilia. Kesho yake motion ndogo ndogo na wiki akakimbia kama gari.

Hiyo ni Miezi 7.5. Wengine alitembea miezi 11, mwingine 11.5 na mmoja miezi 12 na wiki moja. Huyu alikuwa mnene kupitiliza ila mwepesi.
Sijui haujaelewa ama sijui upo kwenye lile kundi la much know au bush lawyer, anyway ukitaka kushauri andika bila kujitia ujuaji!

Nilichokisema huyu dogo hakuna anayemsimamisha bali akipata sehemu akajishika anastruggle kujiinua na kusimama!
 
Ni kawaida sana. Kuna watoto wanaruka stages hasa wakiwa na afya nzuri bila kuuguaugua huwa wanasimama na kuondoka mazima kama gari. Huyo atatembea na miezi 8 au 9.
Okwy, nilihofu maana kutambaa bado, ila akijishika popote tu anasimama sasa hv ana miezi 6.5
 
Yaani huyu atatembea haraka mno. Yeye hataki kukaa chini. Kuna mtoto wangu mmoja miaka hiyo hata baby walker hakuna. Alianza kutaka kuisimama mapema mno. Mama yake alikuwa akimbeba mkononi yeye anapambana kuisimamia. Alipofikisha miezi 5 akawa anasimamia stuli ndogo halafu anachezea na kurusha Mguu mmoja mmoja...
Itabidi nimtafutie baby walker mapema hii!
 
Sijui haujaelewa ama sijui upo kwenye lile kundi la much know au bush lawyer, anyway ukitaka kushauri andika bila kujitia ujuaji!

Ndugu mleta mada!

Kiutaratibu mtu anapotoa ushauri anatoa ushauri kulingana na experience ndogo au kubwa aliyo nayo ili anayeomba ushauri achanganye na zake lile analoomba ushauri lifanikiwe,sasa wewe unapotaka kutufunga wajumbe mikono kama ccm ili tuandike unachotaka wewe ilikuwa haina haja ku-post hapa kuomba ushauri mngekaa chumbani kama ni mkeo au mumeo mkashauriana la kufanya kuhusu mtoto wenu.

Hivi wewe kwa akili zako mtoto wa miezi sita anaweza akajiinua pale alipolazwa ili ashike kitu asimame nacho?huyo mtoto ni nyinyi wenyewe mnaomsimamisha!kwa umri huo anayajua kwanza manufaa ya kusimama kwake?unajua kadiri mtoto ubongo wake unavyokua ndivyo anapoona umuhimu wa yeye kufanya vitu kama kusimama,kutambaa na kuanza kusogelea vitu na mwisho anaona umuhimu zaidi kwenda kwa kutembea?obviously huyo mtoto kwako ni wa kwanza na unataka akue jinsi ulivyojitengenezea picha kichwani mwako kwamba akiwa na miezi 6 asimame 7 atambae tisa atembee kumi akimbie mwaka 1½ umtume dukani miaka miwili umpeleke boarding school.

Huyo siyo robot kwamba utam-program unavyotaka wewe huyo anao utashi wake atajifunza mwenyewe kwa msaada wenu mdogo sana na nakushauri nenda hata kwa doctors,wanakataza watoto kulazimishwa kukomazwa viungo vyao wakiwa wachanga watoto waachwe wajiamulie kadiri akili na miili yao inavyotaka itakuwa hatari pale tu mtoto atakaposhindwa kuvuka stage 1 ya ukuaji ambayo ni kukaa na kujigeuza mwenyewe akiwa na umri kuanzia miezi 7 au 8,mnashauriwa hamtaki nyie ndo mnaotuletea watoto wenye matege ukiwaangalia hujui kama wanacheza mpira au singeli.
 
Mimi niko nje kidogo ya mada, hivi mama mjamzito asipopata vile vidonge vya mwanzo kabisa kuna hatari yeyote ataipata wakati wa kujifungua au atajifungua mtoto mwenye shida?
 
Yaani huyu atatembea haraka mno. Yeye hataki kukaa chini. Kuna mtoto wangu mmoja miaka hiyo hata baby walker hakuna. Alianza kutaka kuisimama mapema mno. Mama yake alikuwa akimbeba mkononi yeye anapambana kuisimamia...
Good story teller
 
Mimi niko nje kidogo ya mada, hivi mama mjamzito asipopata vile vidonge vya mwanzo kabisa kuna hatari yeyote ataipata wakati wa kujifungua au atajifungua mtoto mwenye shida?
Unamaanisha vile vidonge vya supplement, kama Follic acid!?

Kama ndio wanasema vinakinga watoto dhidi ya vichwa vikubwa na mgogo wazi.

Kama mama anapata nutrients za kutosha kutoka kwenye vyakula hata asipotumia hizo dawa mtoto hatakuwa na shida
 
Usiogope wangu katimiza miezi mitatu juzi, ila anapenda kweli kusimama.Binafsi nimejifunza kitu baada ya kumwona Mama yake anakazania sana vyakula vya vitamin na vyenye virutubisho mhimu sana kwa mtoto zaidi sana humfanyika mazoezi ya miguuna mikono pamoja na masaji ya mwili mzima kabla ya kuoga. Hebu jaribu kufanya haya pia tuone.
 
Back
Top Bottom