Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia asafirisha Mwewe 80 katika Ndege

Ambacho sikielewi hawa ndege haswa huwa wanapatikana wapi,? Na kile kama kikamba kinachofungwa kichwani ni kwa ajili gani
 
Mkuu upuuzi wao uko wapi? Kusafirisha hao "hawks" kwa njia ya ndege? Ulitaka wasafirishwe kwa njia ipi kamanda wangu? Kama ni wazungu wamefanya ivo je tungesema wapuuzi?

Kila mmoja anafanya alichojaaliwa na Mungu.pesa anazo za kumwaga azipeleke wapi! Angekua anasafirisha malaya au kilevi cha aina yeyote ningemuona mjinga flani hivi asiejitambua..ni hayo tu kamanda wangu
Kuna ndege za mizigo sio kuwalipia seat

Sent from my SM-G313F using JamiiForums mobile app
 
Umejenga hoja ila umesahau huyo ni Mtoto wa Mfalme anaishi kwa kodi za Wananchi ,alipaswa kutumia njia mmbadala na sio kufuja Mali za Uma namna hiyo..
Mkuu saudi arabia ni nchi tajiri sana sidhani kama kwao hilo ni bonge la tatizo.
Inawezekana hiyo ndiyo ilikuwa njia sahihi ya kusafirisha hao ndege kwa haraka sana.
hujawahi kuona mtu anapakia kuku kwenye prado mpya badala ya kuwapakiza kwenye fusso.
That is Saudi Arabia Royal family wana mapesa mengi sana and wanayatumia kweli kweli na uzuri wananchi Saudi Arabia citzens hawana shida kama zetu za kuchangia madawati na kukosa dawa hospitalini
 
uthamani wao unakuwaje katika mafugo yao....mkuu.. naomba kufamu..!!...
Hawa ndege wanatumiwa zaidi na familia za wafalme wa Gulf States na matajiri wakubwa kwa kuwindia.
Na huwa kuna hunting season ambapo huwa wanaenda jangwa la Iraq na Saudia na kukutana huko kwa mawindo.

Siku hizi wanashindanisha na kuona yupi ni mzuri kwa kuwinda na mshindi hupata zawadi nono.

"Jewels with wings" ndio utajua hilo neno lina maana gani, kwa mfano wale Lanner Falcon wanafika bei hao wafalme wa Qatar mpaka $275,000 kwa mmoja, ni ufahari kuwa nao na jeuri pia ya pesa au tuseme pia traditional yao kuwa na ndege hao.

Peregrine Falcon ni wa pili kwa thamani.
Wapo watu kazi yao kila msimu huenda kuwasaka na wakiwakamata wanaenda kuwauza kwa matajiri hao kuanzia $70000-110000
 
Mafuta yanawapa jeuri sana hawa
Wewe una gesi, mlima, mbuga za wanyama, bahari, mito, maziwa, madini ya kila aina na mengine hayapatikani duniani mfano tanzanite , uranium, na mafuta sasa wewe Mungu akupe nini ?
 
Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia asafirisha Mwewe 80 katika Ndege
Maajabu ya dunia kabisa, Syria, Yemen, Iraq hata Palestine, hao waarabu huko wanapata shida mno, mno, ila huyu mwenzetu kaona kusafirisha ndege ni muhimu kuliko kusaidia waarabu wenzake, ile kuchukuwa wahamiaji tu nchi zote za kiarabu zimekataa, sio ajabu Bw. Trump kuwapiga ban hawa waarabu na wana Imani ya kiislamu, kuna mambo mengine kama haya sio ya kushabikia kabisa, Mwl. Nyerere angempa neno huyu mpuuzi asingesahau maishani kwake...
 
Kamanda Hapo kwenye colour..Umejuwaje kama hawasaidii hao jamaa? Kuna matajiri wengine wanatoa bila kujua mkono kushoto nini kinaendelea, sio lazima mtu akitoa kumsadia fulani basi dunia yote eti ifahamu.alafu huyo nyerere amekua nani? Yeye alikua anaangalia na watu wa saizi yake, sio kila mmoja amtolee neno baya.
 
Kiafya kwa wanadamu waliopanda kwenye hiyo ndege inakuwaje?Manake inakuwa sawa na watu waliopanda gari LA kusafirisha ng'ombe,kuku au mbuzi!
 
Mkuu saudi arabia ni nchi tajiri sana sidhani kama kwao hilo ni bonge la tatizo.
Inawezekana hiyo ndiyo ilikuwa njia sahihi ya kusafirisha hao ndege kwa haraka sana.
hujawahi kuona mtu anapakia kuku kwenye prado mpya badala ya kuwapakiza kwenye fusso.
That is Saudi Arabia Royal family wana mapesa mengi sana and wanayatumia kweli kweli na uzuri wananchi Saudi Arabia citzens hawana shida kama zetu za kuchangia madawati na kukosa dawa hospitalini

Asante kwa ufafanuzi mzuri Mkuu ,nimekuelewa nilishindwa kutofautisha kati ya 'wao' na akina 'sie'.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri Mkuu ,nimekuelewa nilishindwa kutofautisha kati ya 'wao' na akina 'sie'.
Nimekukubari kwa kukubari challenge.
Mfalme wa Saud Arabia kuna kipindi alienda likizo huko ufaransa na familia na wafanyakazi na ulinzi mkubwa.
Vyombo walivyokuwa wanatumia kipindi wako huko vilikuwa baada ya chakula havitumiki tena wanatumia vipya.
Beach ilifungwa kwa ajili yao tu alikuwa ana watu 1,000 tena wamefikia kwenye mahotel ghali zaidi.
jisomee hapa
King Salman's French holiday: A throne, motorcades and a lift to the beach - BBC News
Hawa wana ela sana kwasababu ya mafuta
Saudi king brings 1,000-person entourage on French holiday
 
PRINCE.png

Kutoka Saudi Arabia mtoto wa mfalme wa nchi hiyo Prince Mohammed Bin Salmanambaye pia ni waziri wa ulinzi ndio aliemiliki vichwa vya habari.

Uamuzi wake wa kusafiri na Ndege jamii ya Mwewe wapatao 80 kwenye ndege ya abiria ndio umekua gumzo ambapo ndege hiyo inatajwa kuwa ya shirika la Qatar Aiways.

Kikawaida ni jambo gumu kuwasafirisha ndege ndani ya ndege tena wanaofikia 80 labda tu uwe mtoto wa mfalmee kama ambavyo Prince Mohamed amefanya hivi karibuni baada ya kuamua kuwalipia nauli mwewe 80 kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 ili kupata siti za ndege hao.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Prince Mohamed inaelezwa kuwa ni kweli kitu hicho kimefanyika na waliwafunga mabawa Mwewe wote ili wasiruke wakati ndege ikiwa safarini.

3CACA88F00000578-0-image-a-8_1485821661428.jpg

3CAD23E800000578-0-image-a-9_1485821756177.jpg

Inaelezwa kuwa sio jambo geni kusafirisha wanyama au ndege lakini hawatakiwi kuzidi 6 tu, sasa ili upate ruhusa ya kusafirisha idadi kubwa lazima ulipe fedha nyingi au uwe na kibali maalumu cha viongozi wakuu wa nchi kama ilivyokuwa kwa mtoto wa mfalme.
 
Back
Top Bottom