Kitaalamu ni marufuku/haitakiwi kumpa chanjo mnyama baada ya kupata ugonjwa, kwa kufanya hivyo unakua unazidisha tatizo, tubadilike wafugaji jamani "CHANJO INA RATIBA YAKE" sio wameumwa ndio tunakumbuka chanjo. Kuhusu hao "waliobaki" niseme tu kwamba kama hao vifaranga walikua wanalala, kula na kushinda pamoja basi kuna hatari kubwa ya maambukizi kuwa yamesambaa (sio lazima wawe wote wanaonyesha dalili) japokua inawezekana pia kua wengine wakawa wazima. Cha kufanya watenge hao wagonjwa, tafuta msaada wa karibu (afisa mifugo wa karibu nawe) akija hapo atakupa msaada stahiki. (kuna vitu huwa tunaangalia ambavyo inakua ni vigumu kusema nikiwa mbali na kwa picha hiyo moja tu), hata kama hao vifaranga watakufa, lengo ni kuepusha dhahama kama hizi kesho na kesho kutwa. Asante.
"""Mbeya moyoni"""