Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 431
- 433
Mtoto wa mzalendo wa mchezo wa riadha mzee John Stephen Akhwari aitwaye Rogath John Stephen ajitosa kuwania urais wa shirikisho la riadha Taifa (RT), ni kocha wa riadha wa jeshi la polisi kwa mkoa wa Arusha.
Mzee John stephen akhwari ni nani? ni yule mzalendo wa Tanzania aliyekimbia mbio za riadha za kilomita 42 huko Moscow mwaka 1968 akawa mwisho baada ya kuumia mguu, ila alitibiwa na kuendelea kukimbia hadi mwisho.
alipoulizwa kwa nini umeendelea kukimbia na maumivu ya mguu akasema " Nchi yangu haikunituma kuja kuanza mbio ila kumaliza"