Mtoto wa Dikteta wa zamani kushinda Urais wa Philippines ni mfano wa gharama ya demokrasia dhaifu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,350
Ferdinand "Bongbong Marcos" Jr. ameshinda urais wa Philippines kwa zaidi ya asilimia 50 za kura huku mpinzani wake wa karibu akiwa na wastani wa 30%.

Baba yake Dikteta Ferdinand Marcos aliitawala Philipines kwa miaka 21, mwaka 1965 hadi 1986, chini ya utawala wa mkono wa chuma huku muda mrefu zaidi akiitawala kwa amri ya kijeshi" martial law" na amri za kawaida "decree" baada mahakama kumzuia kugombea kwa muhula wa tatu mwaka 1972.

Utawala wake ulikuwa muovu sana, wa kifisadi, wapinzani wake waliuwawa na kupotea. Hadi anaondolewa madarakani mwaka 1986 inakadiriwa alikuwa ameiba billion 10 dola za kimarekani. Mke wake alikuwa na hobby kubwa ya viatu, inakadiriwa alikuwa akimiliki pair 3000 za viatu hadi wakati wanaondolewa madarakani.

Hatimaye wapiga kura wa Philippines wameamua kuirudisha familia hiyo ya Marcos madarakani kupitia mtoto pekee wa familia hiyo. Marcos Jr. ataitawala nchi hiyo kwa kipindi cha muhula mmoja wa miaka 7 kama hatabadilisha katiba ya nchi hiyo.

Demokrasia wakati mwingine ina mitanziko na matokeo ya kushangaza.
 
Mtoto wa kiongozi mbaya nae ni lazima awe mbaya? Basi kina lizmomko na mama ake hawatakiwi bungeni, japo wao ni team fisadi kweli kweli.

Hoja yako itakuwa na nguvu kama utaeleza sparks za uovu wa huyu wa sasa kama vile hawa pale juu wanavosifikakwa biashara za china, uwezo mdogo nk,
 
Inaonekana serikari za nchi nyingi zinaweka madikteta ni fashion ya tawala nyingi hasa nchi zinapopita ktk tahadhari za kivita, hii ilitokea sana kwa viongozi wa kwanza wa mataifa mengi ya Afrika ni effects za vita ya pili ya dunia za kipindi kile
 
Back
Top Bottom