Pamoja na kwamba ni mtoto ajabu kwa kumuangali lakini ni hali ya kawaida kuzaa mtoto kama huyo na hapa tanzania watoto kama hao wanazaliwa...
Huyo mtoto ni congenital abnormality anajulikana kama anancephaly ambapo anakuwa hana ubongo wa mbele, fuvu linalofunika ubongo(skull) pamoja scalp ...tatizo hutokea pale neuro tube zinaposhindwa kuungana wakati wa ukuaji wa mtoto nikama siku ya23 na 25 baada ya mimba kutungwa. kuna baadhi ya dawa zinazochangia kutokea kwa tatizo hilo ni kama dawa za kifafa, pia kuna magonjwa kama kisukali na sababu zingine ni za urithi wa gene.
..wamama wajawazito wanashauriwa kwenda kliniki ili wakapewe dawa za folic acid ambazo huweza kupunguza tatizo
Kwahiyo jamani tufute kauli ya kusema ni mtoto wa ajabu huyo ni kilema kama vilema wengine; isipokuwa mtoto kama huyo hawezi kuishi .....ana uwezo wa kuishi kwa muda si zaidi ya masasa 24 anakufa