The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 828
- 2,108
GEORGE Stinney Jr, angekuwa na umri wa miaka 90 sasa kama Mungu angemuweka hai. Aliuawa akiwa mtoto mwenye umri wa miaka 14.
Ilikuwa siku kama ya leo, Juni 16, 1944, George alisingiziwa kuua mabinti wawili wa Kizungu ambao walikutwa wamekufa. George alikamatwa, kwa madai kuwa ndiye alionekana nao kwa mara mwisho. Akalazimishwa kukiri kosa.
Jopo la majaji Wazungu (all-white jury), walijifungia na kumhukumu George, bila hata utetezi. Hakuwekewa wakili wa kumtetea. Akahukumiwa kuuawa kwa shoti ya kiti cha umeme.
George alikuwa mtoto, na aliweka rekodi ya kuwa mtoto mdogo zaidi kuuawa kwa adhabu hiyo ya kiti cha umeme. Yalikuwa mateso makali mno kwa George. Alipasuka mpaka kichwa, maana kiti kile cha umeme hakikutengenezwa kwa ajili ya watoto. Kililazimishwa kutumika kumuua George.
Mwaka 2014, yaani miaka 70 baada ya kifo ya George kuuawa, Mahakama Kuu Marekani, ilitoa hukumu ya kukosoa hukumu ya mwaka 1944 (conviction vacated), kwamba George alionewa. Ikaamriwa familia yake ilipwe fidia.
Mwaka 2004, mwandishi Mmarekani ambaye ni mbobezi wa historia, George Frierson, ndiye aliyeibua kila kitu. Baada ya kufanya marejeo na rekodi mbalimbali, kesi ilirudishwa mahakamani na hukumu tofauti ilitolewa.
George ni mtoto wa Afrika. Na aliuawa pasipo haki Siku ya Mtoto wa Afrika.
Ndimi Luqman MALOTO