Mtoto nje ya ndoa naomba ushauri

Mtoto nje ya ndoa naomba ushauri

mambo mengine mpaka yakukute ndio unajua ufanyaje.
 
Huyo mtoto kwa vile umemleta duniani ni wajibu wako kumtunza na ni haki ya mtoto kutunzwa bila kujali amezaliwa ndani ya ndoa au nje. Kwani ilibidi ujue matokeo ya kwenda nje ya ndoa kablwa ya kwenda, kwahiyo ushauri ndo huo.
 
Ni kweli alikuficha, lkn hata ukitaka kujua kwa nn alikuficha hakuna kinachobadilika, beba mtoto lea.
Usikute ww mwenyewe ni wa nje halafu unajipa mawazo haya, kama dada mmoja alipata bf husband material ila ana mtoto wa nje, mdada yy mwenyewe ni mtoto wa nje na tena sio wa nje tu bali hana makao maalum maana mama aliolewa na baba akaoa kwingine yy akalelewa na ndg kwa upendo kabisa. Cha ajabu akawa anadai yuko njia panda kisa huyo bf ana mtoto wa nje, akasahau yy ni wa wapi na amependwa kma alivyo.
It su.cks
 
labda kuna sababu ya kutokuambia mnaweza kuongea na kujua hizo sababu
je huyo mtoto kwa kipindi chote anaishi na nini.....baada ya kuongea mnaweza kumwacha mtoto huko anapolelewa maana inaonekana umeshaanza kuumia/ chuki isije kumdhuru mtoto
 
kutokusema tangu mwanzo kunaibua maswali kwa mwenzi wake, kwamba inawezekana mtu aliyenae si mwaminifu na ukiicha ilo la mtoto labda kuna mengine pia ambayo hakuelezwa tangu mwazo. UONGO HAUJAWAHI KUWA TABIA NJEMA, nakushauri msamehe ili muendelee kukaa pamoja na mlee watoto wenu na huyo mwanaume aonywe na wazee.
 
Hbr wana JF.
Upo na mumeo au mkeo kwa zaidi ya miaka 10 mkiishi kwa amani na furaha na mmebarikiwa kupata watoto 2. Siku mmeo/mkeo anakwambia ooh! Blaa blaaa blaaa unajua nilikuwaga na mtoto kabla hatujaoana sasa moyo unaniuma kuweka siri hii leo nimeona nikwambie. Kama ni wewe unafanyaje na kweli ukifwatilia unajua yupo na ni mkubwa kulingana na mlipofunga ndoa na kuna baadhi ya ndugu zake wanajua hili.

Ushauri jamani kama ni wewe unafanyaje?

Tatizo nini hapo pekundu?
Ulimkuta yuko bikira;
Au alishatumika.
Pokea mtoto wewe!

Bazazi!
 
hapo trust itavunjika


Mtu anayeweza kuficha mtoto wake kwa miaka 10 na zaidi ni hatari kuliko tindikali
 
That's my point...kama anataka kusamehewa mwambia aseme na mengine anayokuficha;

Inatisha ati...kuna uwezekano yuko mwingine na mwingine na mwingine...na kuna mengine na mengine na mengne...

Hakuna kitu kibaya na mtu mbaya kama msiri na muhongo...mwanamke kama anakupenda anakupenda; alidhani utamkataa ungejua kuwa ana mtoto? hiyo ni ushamba...wanaume wa kizamani ndio walikuwa wana hizo sana...wanaoa afu wanasubiri mke akizaa wamwambie kuna mtoto mwingine...kwa nini mtu asikupende jinsi ulivyo?

Na hiyo inachangia mama wa kambo kuwa na roho mbaya..hasira anamalizia kwa mtoto ambaye ni innocent sababu ya kosa la baba.

Na huyo mzazi mwenzie kwa nini alikubali kukaa kimya wakati wewe unaolewa...Kuna kitu hapo...more likely wanaendelea ndio maana ametulizwa asikwambie.


kutokusema tangu mwanzo kunaibua maswali kwa mwenzi wake, kwamba inawezekana mtu aliyenae si mwaminifu na ukiicha ilo la mtoto labda kuna mengine pia ambayo hakuelezwa tangu mwazo. UONGO HAUJAWAHI KUWA TABIA NJEMA, nakushauri msamehe ili muendelee kukaa pamoja na mlee watoto wenu na huyo mwanaume aonywe na wazee.
 
Mimi dada yangu alijua mumewe alizaaga nje baada ya mume kufa...ndio hivo tena mtoto hakuwa na chake although wadogo zake wamemkubali ingawa hakuna bond kivile...wanaume wengine sijuhi wakoje; na wanaozaa nao ndio sijuhi wakoje kabisaaa...unakubalije mtoto wako awe siri? wanajua side effect ya hizo siri...

Dada yangu kajisema well and good...huyu alikuwa baba yako?...haya hawa wadogo zako kwaheri...



mambo mengine mpaka yakukute ndio unajua ufanyaje.
 
Hakuna kitu kigumu kama kupokea kijiti cha malezi aisee. Bora mtoto umkute mdogo umgroom mwenyewe. Mbwa akizaliwa akakuta paka nyumbani wanaishi kwa amani. Ila akija mkubwa hapatatosha.

Rahisi sana kusema mchukue umlee. Kwa nini asiendelee kulelewa na mamake? Makuzi yako na aliyopewa yanaweza kuwa tafauti sana. Nimependa majadiliano ya BADILI TABIA na nyumba kubwa. Nyuma ya siri kuna siri kubwa zaidi
 
Last edited by a moderator:
Hbr wana JF.
Upo na mumeo au mkeo kwa zaidi ya miaka 10 mkiishi kwa amani na furaha na mmebarikiwa kupata watoto 2. Siku mmeo/mkeo anakwambia ooh! Blaa blaaa blaaa unajua nilikuwaga na mtoto kabla hatujaoana sasa moyo unaniuma kuweka siri hii leo nimeona nikwambie. Kama ni wewe unafanyaje na kweli ukifwatilia unajua yupo na ni mkubwa kulingana na mlipofunga ndoa na kuna baadhi ya ndugu zake wanajua hili.

Ushauri jamani kama ni wewe unafanyaje?

Jamani kina mama/baba hebu fikirieni kwa umakini. Mimi pia naweza kufa au kuachwa na mwanamke mwingine akalea wanangu lkn haya mambo yafanyike kwa utaratibu.
Nimeishi na mume kwa upendo zaidi ya miaka 10 kwa upendo na furaha alishindwa vipi kuniambia mke wangu nina mtoto nje? Tena ni mtoto aliyezaliwa kabla hajanioa? Kuna siri gani imejificha hapa? Cha ajabu ni nini? Leo hii zaidi ya 70% ya ndoa wanaishi na watoto wa nje kwanini yeye afiche????.
Eti baada ya kubwagwa na mzazi mwenzie kuondoka na kujua hata weza kumwona tena ndo aone umuhimu wa kuniambia mimi? Jiulize je asingeondoka? Je asingepata mpenzi mwingine? Angesema lini???. Maana kwasasa hawezi kuonana naye ndiyo maana kaamua kusema.
Kwakweli nakuwa na wakati mgumu sana kuamua hili.
 
Hili ni janga la kimaisha mabinti tunapaswa kuwa makini sana, kama halijakutokea ni vigumu kuelewa ila linaumiza watu wengi sana kwa kweli. Na akina kaka muwe wawazi mapema sisi wanawake ni waelewa sana ukistaarabika.
 
Back
Top Bottom