Mtoto ni wangu au bado nadanganywa?

Mtoto ni wangu au bado nadanganywa?

jimmy jay jay

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
223
Reaction score
39
WanaJF,

Mimi mwaka 2009 nilimpata binti tukapendana badae kaniambia ana ujauzito. Mimi nikaamua kujitambulisha kwao na kutoa barua kwao, wakanijibu nitoe mahari. Kipindi nasubilia kupata hela ili nilipe mahari nikaona gari la baba yake limemleta nyumbani kwangu na nguo zake. Mimi nikaona poa nikamuambia mzee (kama baba yangu). Kaniambia nimpeleke nyumbani kwake nisubiri wiki moja wanipe baraka za wazazi halafu nikae nae, nilifanya hivyo.

Sasa nikawa namuita mwanamke nampa hela ili aanze kununua vifaa vya nyumbani, kama kesho yake ndo tunapewa baraka nimetoka kazini akaja nyumbani kwangu akawa amalala kitandani, nikachukua simu yake badae nikaona msg imeingia inasema hivi; ''Wewe kiumbe changu umeamua kumpa mtu mwingine''.

Mimi nikajifanya kama mwanamke nikawa nachati nae, nikagundua kwamba mimba inaweza isiwe yangu. Nikamuambia mzee tukawapigia kwao, demu karudi nyumbani kwao ila yeye kaendelea kusisitiza kwamba mtoto ni wangu.

Basi badae kajifungua kwao wakaniita eti nije kuangalia kama tunafanana, nikaenda ila sijaona hata kidogo kwamba tunafanana. Sasa mimi nikaamua kusafiri na kwenda mbali ili ni refresh mind yangu na nikapata kazi nyingine, basi nikaanza maisha mapya.

Juzi mwezi wa 12/2014 ndo mwanamke kanipigia kwamba sasa hivi amepanga, anaishi na mtoto na hana kazi yoyote na mtoto amefikisha umri wa kuanza shule. Mimi nikamuambia kwanini baba yake hakusaidii? Kaniambia baba yake ni wewe.

Mimi nikasafiri nikaja kuwaona, nikakuta kwenye cheti cha kuzaliwa ameandika kwamba baba yake ni mimi na mtoto ukimuuliza jina la baba anataja jina langu ila hanijui kamba ndo Mimi. Nikaona kweli inawezekana huyu mtoto ni wangu. Nikaomba samahani nikasafiri tena nikaaga kazini nikarudi ili niishi na mtoto wangu ambae hajakaa na baba kwa kipindi cha 5 years.

Nikafika mwanamke nikamfungulia duka la nguo na vinywaji. Sasa juzi kaniona naongea kwenye simu mda murefu kanipokonya simu. Mimi nikamuambia ungeniuliza kwamba naongea na nani kuliko kunipokonya simu wakati bado naongea.

Kiukweli nilikua naongea na rafiki yangu yupo Marekani. Tukafika nyumbani, rafiki yangu tena kanipigia, mwanamke kaanza tena maneno makali. Lakini kumbuka kwamba na yeye ana vifaa vyake nyumban maana niliongeza vitu vidogo kama Godoro, Fan, TV na vingine vichache ila vingine ni vyake.

Ndo kaanza, 'nenda kaongelee na mataira wako nje'. Mimi nikamuambia mimi nimeacha kazi na mambo mengine ili nije tujenge familia, sasa hivi unaniambia hivyo? Kanijibu, 'Kwani kuja hapa nilikuweka kamba?

Duuu hapo nikaishiwa pozi, nikamuambia basi niache, kanijibu, 'Nikuache Mimi, au wewe ndo wa kuniacha? Sasa hapo ndo nikaishiwa na nguvu kabisa, nikamuuliza, 'nikuache'? Kaniambia, 'uniache Mara ngapi'?

Basi mimi nikamuambia kwamba nashukuru na kesho kila mtu aendelee na maisha yake. Asubuhi nikaamka nikamuambia kwanzia leo kila mtu awe na maisha yake. Kaanza kuomba samahani na machozi mengi anasema eti hasira ndo sababu na wivu, kaniomba nimpe last chance. Lakini yeye anasema ataishi, je na yeye na mtoto? Maana yake kinachomuuma sio kwamba hatokuwa na mimi, ni kwamba ataishije?

NB: Halafu kila siku yeye ni mbishi hataki kunielewa. Nikienda kunywa soda ananiandikia ma msg eti tuna shida mpaka matakoni na wewe unaenda kunywa? Yeye hajasoma na nikimshahuri kitu anabisha wakati hana experience ya maisha.

Namuelekeza hataki mpaka sasa nimeanza kujuta na kuwaza kwamba mtoto anaweza asiwe wangu.

Mnishauri nifanye nini, maana sielewi niamuaje..
 
Mkuu pole sana kwa mapito unayopitia. Ila kwa jinsi nilivyoelewa huyo mtt siyo wako umepewa either mwenye mtt hana uwezo wa kutunza ama kuna mapungufu ya namna nyingine baina ya mkeo na aliyempa ujauzito

Kingine we kama mwanaume unatakiwa kuwa na msimamo thabiti usiyumbishwe kwa maneno ya kulialia na kutia huruma kwani kabla ya kukujua alikuwa akiishije :what:

In short huyo hakufai na kidogo kidogo anaanza kuvua ngozi yake ya ukondoo na kubaki na ya chui , Kama mtu hana elimu wala kumjua Mungu hilo ni bomu linaloweza lipuka anytime
 
Asante mkuu maana Ni shidaa najiuliza nikiamua kumuacha na mtoto akawa Ni wangu nitakua na amani kwer
 
DNA test ndio itakwambia ukweli kuhusu huyo mtoto.Alaf kwa jinsi nilivyoona ni kwamba kero za huyo mwanamke ndio zinakufanya huwe na hisia mbaya juu ya mtoto.
 
Dah is very difficult issue king chamsingi sana Hapo usipime hats DNA yaan vina saba maana ukikuta sio wako utaumia sana nduguu!! Wewe cool Fanya mtoto ni wako wala usitake kuchunguza sana kaka tulia mfanye mtoto akupende sana asisikilize neno lolote na kweli pia huyo mkeo anawivu sio kingine ndugu

Kuna jamaa wangu yeye alikuwa na mwanamke acha kabisa yani akipiga simu usiku ikakuta inatumika nmmh!! Analia mpaka basiiiiii sasa cha msingi wewe ishi maisha ya kibaba sasa ndugu
 
Wewe amini tu kwamba mtoto ni wako
Ukimchunguza bata..............!
 
Asante Mimi nimemuambia kwamba akiniambia maneno kama hao tena kila mtu ataishi maisha yake
 
Usipime dna ndg itakuathir sana ikzngatia mtoto anakujua wewe na hadi kwenye cheti..take easy lea mtoto
 
Naona tatizo la kuanza mapenzi ukubwani. Kosa ulifanya siku ya kwanza uliposoma ujumbe kuwa mimba ya jamaa mwingine palepale ungekinukisha vya kutosha. Ushalegea hata ikikaza sasa utachekesha watu tu.
Pima DNA kama mtoto wako mchukue uanze nae maisha wewe nae kama sio wako unajua cha kufanya.
Huyo mwanamke nae wa kupiga chini
 
Yaani kwa miaka mi 5 yote hajakutafuta, sasa ndo amekutafuta? Nahisi alikutafuta baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo, otherwise hii ni chai. Kama si chai, basi jitafakari.
 
Sikiza kijana, mimi pia ni mama. Huyo mtt sio wako ht km ni wako huyo mm kaa nae mbali sana. Atakuharibia maisha yako. Km anakosa ht staha na kuingilua mazungumzo kwenye simu kuna siku atahara kwa mdomk mbele ya wageni. Ondoka mahali hapo haraka.
 
Ebana acha upole usio na maana inaonekana dizaini flan kama hujiamini

Ndio maana huyo mwanamke anakuwa na maneno ya hovyo .

Hapo mwisho uliamua vizuri nashangaa ukarudi nyuma. ...mwanamke anatakiwa akutii sasa hayo maneno maneno anatoa wapi.

Piga chini mtu habebeki wa kazi gani
 
Brother brother, tatizo liko kwako, halafu si dogo. Uwezo wako wa kufikiri na kufanya maamuzi ni wasiwasi bro, no disrespect.
 
Back
Top Bottom