Mtoto na mpenzi

Mtoto na mpenzi

Simplelady

Member
Joined
Oct 26, 2009
Posts
44
Reaction score
22
Mama mmoja aliachana na mume wake muda kama miaka 12 hivi iliopita, baadae akapata bwana ambaye walikuwa wanakaa mbalimbali, ingawa alikuwa walikuwa wanatembeleana na mara nyingine analala hapo kwa mwanamke na mwanamke anaenda kwa bwana.
Sasa wameamua kufanya mipango ya kufunga ndoa ili waishi pamoja, ila mtoto wa huyu mama hataki na hampendi huyu bwana amuoe mama yake. Sasa mama yupo kwenye dilemma afanyeje kuhusu hili?
 
Hilo litoto linataka mama yake akamuliwe na nani?
Au anataka huyo mama aibue mmoja wa Serengeti boys ndio atie adabu?
 
Huyo mtoto hana akili, mapenzi ya mama yake yanamhusu nini? Anataka mama yake aanze kazi ya kubadilisha wanaume wa kumrithisa ndio afurahi?
 
Huu uzungu unatupeleka pabaya, yaani mtoto anaonyeshwa mpenzi wa mama!!
 
Ana sababu za msingi?
How old is mtoto?
Aombe mtu mwingine aongee na mtoto ili ajue kwanini mtoto hataki, huenda huyo mwanaume ni abusive.
 
Tofauti ya Africans na wazungu ipo kwenye thamani ya watoto. Mzungu mtoto/watoto wake ndo kila kitu kwenye maisha yake. Kama aliachana na mume wake, kwa walio wengi huwezi kumuoa hadi watoto wake waridhie.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
huwezi jua mtoto anafikira nini yawezekana umri wa mama yake ndo unaweza kua kikwazo au huyo mme anaye taka kumuo ni sawasawa na mwanae huwezi jua nini kinasababisha dogo akatae kuna umri mwingine wa mama kuolewa ni kutiana aibu ni bora aka2lia nyumbani
 
hivi hapo posa na mahari vinapelekwa kwa mtoto au???
 
Mama mmoja aliachana na mume wake muda kama miaka 12 hivi iliopita, baadae akapata bwana ambaye walikuwa wanakaa mbalimbali, ingawa alikuwa walikuwa wanatembeleana na mara nyingine analala hapo kwa mwanamke na mwanamke anaenda kwa bwana.
Sasa wameamua kufanya mipango ya kufunga ndoa ili waishi pamoja, ila mtoto wa huyu mama hataki na hampendi huyu bwana amuoe mama yake. Sasa mama yupo kwenye dilemma afanyeje kuhusu hili?

Halafu hujatuambia umri wala jinsia ya mtoto.
Ushauri wangu, asidharau tu mambo ya watoto; kama ni wadogo ni malaika wale, they can smell an evil person from far!
 
kweli kaunga, lamcingi afanye jitihada binafsi kujua maoni ya mtoto, ni lazima kubalance kati ya mume na watoto
 
Hiyo ndo tatizo la mizaz ya kiafrika
 
Sina hakika ni nani mbaya kati ya baba au mtoto ila ninavofahamu maranyingi mtoto hawezi kumchukia huyo baba bure, kids are angels, you love them, they love you back, ningekuwa mimi ni huyo mama ningechunguza zaid kwa nini mtoto hampendi baba mpya na ningefanyia kazi (if I love both my babies), labda mama kuna mambo anaongea kuhusu huyu baba you never know.... Lakini kwa kiasi kikubwa watoto hawasikilizi maneno kabisa, huwa watakupenda kutokana na unavyowatreat....Huwezi ingia kwenye ndoa ambayo tayari ina mgogoro, you will never find peace, Na huyo baba ana role kubwa ya kuplay, yeye ni mkubwa mtoto ni mtoto, ni time kwake kumuonyesha mapenzi mtoto wa mpenzi wake, akae nae ajue anapokosea, awe kama baba wa ukweli sio wa kambo, aongee nae vizuri acheze nae na ajenge tabia ya kumzawadia, kufuatilia maendeleo yake shuleni, kumuengage kwenye mazungumzo na maamuzi nk. to me if you dont love my kids, it means you dont love me, period, and if my kids dont love you, there is high possibility you are fake.
 
Mama mmoja aliachana na mume wake muda kama miaka 12 hivi iliopita, baadae akapata bwana ambaye walikuwa wanakaa mbalimbali, ingawa alikuwa walikuwa wanatembeleana na mara nyingine analala hapo kwa mwanamke na mwanamke anaenda kwa bwana.
Sasa wameamua kufanya mipango ya kufunga ndoa ili waishi pamoja, ila mtoto wa huyu mama hataki na hampendi huyu bwana amuoe mama yake. Sasa mama yupo kwenye dilemma afanyeje kuhusu hili?

dogo ana akili sana....hapana kukubali mama analeta ujinga ujinga hapa. wazazi wengine bwana...sasa wewe unadhani mtoto anajisikiaje kuona jamaa anakuja alala hapo anagegeda na kusepa alafu leo aje aoe...loh mama hana haya!?
 
Mtoto yuko sahihi!! Kisaikologia mtoto anaamini kuna mambo yatabadilika,anahic atateswa,hatapata upendo kama awali kutoka kwa mama ake!! BI MKUBWA amsikilize mwanaye!
 
Back
Top Bottom