Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,193
Ana miaka 30 kwa sasa, ni kijana mtanashati na mwenye bidii ya kazi. Nilikuwa na ahadi ya kukutana nae kwa shughuli fulani, mkoa mmojawapo hapa nchini. Wakati tunajadiliana nae kuhusu yale yaliyotukutanisha nae, alifika Mzee wa miaka 60 hivii, Mzee yule aliingilia maongezi yetu na kuanza kumshauri rafiki Yangu huyu aoe. Ghafla rafiki yangu akamkatisha yule Mzee na kumwambia ''ondoka hapa, ndio wale wale'' Mzee akaondoka
Rafiki yangu huyu, akaniambia hafikirii kuoa kwa sababu wazee wa siku hizi hawana tofauti na vijana. Akaniuliza unamkumbuka yule mchumba wangu wa kijijini? Nikasema, ndiyo!!
Naam, alikuwa binti mzuri sana, mpole yeye, mkarimu yeye, wa kupigiwa mfano yeye. Wawili hawa walipendana sana. Upendo wao uliongezwa kasi na baba yake ambae alitaka wafunge ndoa upesi. Binti nae akachachamaa wafunge ndoa maana anampenda.
Lakini rafiki yangu huyu hakuwa tayari kwa sababu biashara ilikuwa haimuendei vizuri. Binti nae kakubali ila kamwambia basi waendelee kukutana kimwili ili penzi lao lisichuje.
Anasema, Msichana ndiye bingwa wa kukataa mapenzi bila kinga, lakini siku moja ulizuka ugomvi baina yao baada ya mdada kusema anamechoka na kinga. Ugomvi huo ulisababisha siku ile wakatawanyika bila kuagana.Siku nzima iliyofuata hawakuwasiliana kwa simu wala ana kwa ana. Ilipofika usiku wa saa mbili usiku alimpigia simu mchumba wake huyo lakini alikata, kapiga tena na tena lakini ilikuwa inakatwa.
Aliamua kwenda kuyamaliza akaelekea kwao msichana. Wakati anaelekea kwao msichana alipigiwa simu na mtu mwingine ambae alimwambia aende kwenye jengo fulani ambalo lilikuwa halijakamilika akaone mchumba wake anayoyafanya. Upesi akaenda.
Lahaula lakwata, mchumba wake alikuwa na baba yake mzazi, gizani. Baba anamwambia binti /mkwe mtarajiwa wake asitoe mimba aliyonayo maana hataki damu yake ipotee bure na kuwa atamlazimisha kijana wake amuoe.
Rafiki Yangu huyu aliamua kuwamulika tochi, akawaambia amesikia kila kitu na kuwa hataoa. Kesho yake akasafiri, mpaka nakutana nae ana miaka miwili hajarudi kwao.
Sasa ikiwa baba na Mtoto, wanaumwa ugonjwa mmoja, Mtabiri wa kazi gani kutuambia, maadili yameisha? Kwamba hata wazee, viongozi wetu na wale tuwaaminio sana, baadhi yao hutushauri mambo kwa maslahi yao?
Ndiyo, ugonjwa umeingia.. Nani alaumiwe kwa kupoteza ufunguo wa UKWELI na UAMINIFU ?