Sitaki kufurahishwa mrembo, bali nataka UKWELI kama ulivyo.Hayo mambo ya kuthibitisha unyani ni ya kisayansi na wala kwa akili yangu siwezi kuthibitisha hilo mdada. Ila kwa upeo wangu mfupi nimeandika comment nyingine chini labda itakufurahisha hyo.
Pili, mambo ya Kisayansi yapo bila shaka umeyasoma, ila kama uliyasikie bila kujua hakika yake, huku ni kuikosea heshima ELIMU. Hutakiwi kuwa shabiki katika mambk ya kielimu wala hutakiwi kuwa "Bendera fata Upepo".wala "Kichwa Mchunga". Kabla hujaandika jambo hakikisha una ELIMU nalo kama huna awla kukaa kimya au kuuliza.