Mtoto mnene kuliko wote dunia apungua kilo 191 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto mnene kuliko wote dunia apungua kilo 191

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Billy Robins Friday, January 16, 2009 1:52 AM
  Mtoto mnene kuliko wote duniani aliyekuwa na kilo 381 amefanikiwa kupunguza nusu ya kilo za mwili wake baada ya madaktari kumfanyia upasuaji kuondoa mafuta kwenye mwili wake. Billy Robbins (19),kutoka Houston, Texas ambaye mwanzoni alikuwa na kilo 381 alionywa na madaktari kuwa akiendelea kula sana moyo wake utasimama kufanya kazi zake.

  Madaktari walimfanyia upasuaji Billy na kufanikiwa kuondoa kilo kadhaa za mafuta kutoka kwenye tumbo lake.

  Mtoto huyo hivi sasa ana kilo 190 zikiwa ni nusu ya kilo alizokuwa nazo mwanzo. Mama wa mtoto huyo alilaumiwa kutokana na matatizo ya unene yaliyompata mwanawe.

  Baada ya kumpoteza mtoto wake wa kwanza kutokana na kansa ya ubongo mama huyo alihamisha mapenzi yake yote kwa Billy kwa kumlisha vyakula mbali mbali zaidi ya uwezo wa mtoto huyo.

  Bila ya kujua kwamba alikuwa akimuua mtoto wake bila kujua, mama huyo alisema Billy alikuwa akipenda sana kula pizza, chipsi na hamburger.

  Billy alifanikiwa kupoteza kilo 31 punde tu baada ya upasuaji wa mwanzo kumalizika.

  Kwa sasa Billy anaendelea na matibabu yake ya kupunguza uzito.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=808798&&Cat=5
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  du hii hatari, dogo amenipita kama kilo 120
   
Loading...