Mtoto Mdogo wa kiume alimuuliza Mama yake

Halfan Hamisi

New Member
Sep 11, 2021
4
7
Mtoto Mdogo wakiume alimuuliza Mama yake kwa upole: "Unalia nini Mama?"

Mama yake akajibu: "Kwasababu Mimi ni mwanamke!"

Sijakuelewa Mama.

"Sijakuelewa Mama!?"

Mama yake akamtazama kidogo, kisha akasema: "Na kamwe hutoelewa"

Basi Mtoto hakulizika, ivyo akamfuata Baba yake nakumuuliza swali lile lile:
"Baba kwanini Mama ulia bila ata sababu?"

Baba yake akajibu:
"Wanawake wote ulia tu bila sababu, kwaiyo usimshangae Mama yako!"

Basi yule Mtoto akaendelea kukua mpaka akawa mtu mzima, lakini kwakuwa yeye ni mwanaume bado alikuwa hajui kwanini wanawake wanalia.

Basi mwisho akaamua kupiga magoti nakuanza kuwasiliana na MUNGU kupitia Simu ya maombi vocha IMANI yake. MUNGU alipopokea tu Simu akamuuliza haraka haraka.

"Bwana MUNGU, kwanini wanawake ulia haraka haraka bila sababu?"

MUNGU akajibu:
"Siku namuumba mwanamke ilikuwa ni siku maharumu.

Niliyafanya mabega yake imara vyakutosha ili yabebe uzito wa duniani, bado kubeba siri na matatizo ya mume wake.

Nilimpa nguvu yakujifungua nakulea Mtoto wake, pia nikampa moyo wauvumilivu pindi Mtoto wake atakapokua Mkubwa nakuanza kumdharau nakumtelekeza, amsamehe tu.

Pia nimempa moyo mgumu, ambao yeye usonga mbele ata Kama mume wake amekata tamaa. Pia nmempa moyo wakumpenda Mtoto wake ata Kama kamuumiza kiasi gani.

Pia nimempa nguvu yakubeba matatizo ya mume wake, kwakuwa yeye ni ubavu wake.

Pia nimempa hekina yakumtambua kuwa mume bora hawezi kumuumiza mkewe ila kuna wakati Shetani uingia tu.

MWISHO KABISA:
Nimempa machozi ili ayatumie kulia pindi tu aumiapo au kuchukizwa na mtu. Na akisha lia usamehe na maisha yanaendelea. Bila kumpa machozi mwanamke angekuwa ni hatari zaidi ya chui na Simba.

"Umeona mwanangu?" MUNGU alisema, kisha akaendelea kusema:
"Uzuri wa mwanamke haupo kwenye namna avaavyo, au umbo alilo nalo au Mtindo wa nywere zake.

Uzuri wa mwanamke utauona machoni mwake, kwasababu macho ndio mlango wa njia ya kujua moyo wake. Mahali ambapo kaweka mambo yote.

Kijana akajibu:

"Asante MUNGU, sasa nimeelewa naomba unijalie nipate mke mzuri wakunifaa, pia mjalie uyu mwanamke au mwanaume aliye soma ujumbe huu apate mume au mke wakumfaa..Kama sio yeye ndugu yake rafiki yake ata Mtoto wake AMENI"

Wewe uliye barikiwa na ujumbe huu, sema AMENI, kisha share kwenye vikundi 5 na MUNGU
akubariki sana AMENI.
 
Back
Top Bottom