Mtoto mchanga 'azaliwa' mara mbili baada ya upasuaji

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,908
Mtoto mchanga wa kike kutoka Lewisville, Texas, 'amezaliwa' mara mbili baada ya kutolewa katika kizazi cha mama yake kwa dakika 20 ili kufanyiwa upasuaji.

Akiwa miezi minne mja mzito, Margaret Hawkins Boemer aligundua kuwa binti yake, Lynlee Hope, ana uvimbe katika uti wake wa mgongo. Uvimbe huo unoajulikana kama sacrococcygeal teratoma, ulikuwa unasukuma damu kutoka kwa mtoto huo - jambo lililoongeza hatari ya moyo wa mtoto huyo kutofanya kazi.Baby Lynlee alikuwana uzito wa chini ya kilo moja wakati wapasuaji walipomtoa kwenye uzao wa mamake.

Bi Boemer awali alikuwa amebeba mimba ya pacha, lakini alimpoteza mtoto mmoja kabla ya kumaliza miezi mitatu ya kwanza. Awali alishauriwa kuitoa mimba hiyo kabla ya madakatari wa wa hospitali ya watoto ya Texas Children's Fetal Center kumpndekezea upasuaji huo wa hatari.

Uzito wa uvimbe huo na ule wa mtoto ulikuwa karibu sawa wakati upasuaji ulipofanywa. Aliarifiwa kuwa mwanawe Lynlee ana asilimia 50 ya kufanikiwa kuishi. Bi Boemer aliambia CNN: " nikiwa na miezi mitano, uvimbe huo ulikuwa unasitisha moyo wake kufanya kazi, kwahivyo ilikuwa ni uamuzi baina ya kuruhusu uvimbe huo ummalize au kumpa nafasi ya kuishi.

"Ulikuwa uamuzi wa rahisi kwetu: Tulikuwa tunataka kumpa maisha."
'Moyo wake ulisiti kupiga 'Lynlee Boemer alitolewa kutoka uzao wa mamake kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha yake kabla ya miezi mitatu baadaye kuzaliwa kupitia upasuaji. Lynlee Boemer alitolewa kutoka uzao wa mamake kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha yake kabla ya miezi mitatu baadaye kuzaliwa kupitia upasuaji.

Daktari Darrell Cass wa Texas Children's Fetal Centre nimojawapo ya matabibu waliotekeleza upasuaji huo. Amesema uvimbe huo ulikuwa mkubwa, kiasi cha kuhitaji upasuaji mkubwa kuufikia, jambo lililohatarisha maisha ya mtoto huyo.

Moyo wa Lynlee nusra usite kupiga wakati wa upasuaji huo lakini mtaalamu wa moyo alimsaidia kuendelea kuishi wakati uvimbe huo ulipakuwa unatolea, aliongeza.Madaktari hao baadaye walimrudisha katika uzao wa mamake na kuufunga uzao kwa kuushona.

Bi Boemer alisalia kitandani kwa wiki 12 zilizofuata, na Lynlee alizaliwa kwa mara ya pili mnamo Juni 6. Alizaliwa kwa upasuaji akiwa aribu kutumiza miezi tisa tumbano, na alikuwa na karibu kilo mbili na nusu.

Lynlee alipofikisha siku nane baada ya kuzaliwa, alifanyiwa upasuaji mwingine kutoa uvimbe uliosalia katika uti wake wa mgongo.Dr Cass anasema mtoto huyo sasa amerudi nyumbani na anaendelea vizuri. "Bado ni mchanga lakini anaendelea vizuri," amethibitisha.

Sacrococcygeal teratoma ni uvimbe usiojitokeza sana na huwapata watoto 30,000 kati ya 70,000 wanaozaliwa. Haijulikani husababishwa na nini lakini watoto wa kike huathirika mara nne zaidi kuliko wavulana.
 
daaaah.. ingekua bongo ndio ile kusema mtoto kafia tumbon na mama nae anaweza kuaga
 
daaaah.. ingekua bongo ndio ile kusema mtoto kafia tumbon na mama nae anaweza kuaga
Ni kweli kabisa kama ingetokea huku kwetu maisha ya mtoto na mama yake yangekuwa hatarini sana. Nchi yetu bado haijakuwa na waalamu na vifaa vya kutosha kuweza kuendesha operations kama hizo. Si mchezo; kwanza uwe na mazingira supportive kwa hiko kiumbe kuendelea kupumua wakati muda wa kuzaliwa bado, pili viungo vyake bado vilaini sana kuweza kuhimili upasuaji tatu hali ya mama huku akiwa na mimba changa kama hiyo. Huku kwetu na uwakika wangerahisisha kwa kusema "mama ili wewe upone hii mimba inatakiwa itolewe" na hakuna jinsi wengi wanakubali na mchezo unaishia hapo.
 
Back
Top Bottom