Mtoto kufa baada ya saa 3 toka kuzaliwa

Field Marshal

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
414
280
Habari wakuu

Kuna binti kajifungua salama kwa njia ya kawaida leo saa 10 alfajiri akaruhusiwa kurudi nyumbani punde tu baada ya kujifungua.

Aliporudi nyumbani akapumzika kwa kulala yeye na mtoto kwa uchovu wa uzazi. Saa 1 asubuhi akaamka na alipojaribu kumuamsha mtoto alikuta ameshafariki.

Swali langu ni je, kitu gani kinaweza kuwa sababu ya mtoto kufariki? Huyu binti ni mdogo wangu nahitaji kujua Ili nijifunze kupitia hilo.
 
Yawezekana alimziba pumuzi mtoto kutokana na usingizi mzito wa mama Mzazi.
Pengine mtoto alilazwa vibaya.

Sababu ziko nyingi.
Angalia rangi ya mtoto ikoje kwanza.
 
Nadhani kabla ya kumzika ungempeleka kwa dr. akafanya uchunguzi kujua Zaidi, sina uhakika kama hospitali zetu baada ya mtoto kuzaliwa wanamfanyia uchunguzi wa kila kitu. Dr. atakupa jibu sahihi.
 
Mtu kajifungua saa 10 saa 1 kashafika nyumbani na kulala sio sahihi..

Ila pole mkuu
Uko sahihi sikuliona hilo. Kuna mambo mengi sana yanatokea ndani ya masaa 12 ya kuzaliwa mtoto.
Sasa kukimbilia home ni hatari sana kwa wote wawili. Mama na mtoto.
O
 
Yawezekana alimziba pumuzi mtoto kutokana na usingizi mzito wa mama Mzazi.
Pengine mtoto alilazwa vibaya.

Sababu ziko nyingi.
Angalia rangi ya mtoto ikoje kwanza.
hili ndilo la kwanza la kuwaza
mtoto mdogo nir ahisi sana kuzibwa pumz na mama yake wakati wamelala. ndio mana inashauriwa mama mzazi alale pembeni kidogo na mtt asikae karibu nae
 
Hilo ni ngum mana ilikuwaje akaruhusiwa kwa mda mfupi namna hiyo,anatakiwa akae hata masaa 24,kabla ya kuruhusiwa
 
Back
Top Bottom