Mtoto kubemendwa hutokea hivi

Naomba kuuliza kuna uwezekano mtoto akabemendwa akabaki na afya yake mzuri ila akawa mlegevu na kushindwa kutembea na darasa hapo ndugu zangu.
 
wenyewe wanasema sayansi yote imetokana na kitabu kitakatifu kwani kila kitu kimeelezwa humo,labda ndiyo haya mkuu
Tena huyu jamaa angeshauriwa akomae na fani yake....
Huu ushauri awaachie watu waliosomea..
Na sio kupotosha umma namna hio
 
Hii mada inaleta maswali vikirishi zaidi badala ya kwenda kwenye hitimisho moja kwa moja .

Kuna kitu umeona hapo kwenye suali lako la kwanza point bado IPO hivyo ilivyo kwamba baba na mama wanaweza kuendelea kufanya tendo ila haitamuadhiri mtoto,lakini mama akitoka nje basi mtoto anadhurika .

Hicho kunachomdhuru mtoto ni nini ?tukiite Acid au kama kuna jina lingine la kisayansi liweke hapa Mkuu jamii tufahamu.

La pili umezungumzia viruses ni kweli hapo virus ni mpaka mhusika awe na maambukizi na hayo maambukizi ni ya maradhi yote ya zinaa .
Maana tukisema tu maambukizi wengi huelewa ni HIV/AIDs peke yake .
 
Naomba kuuliza kuna uwezekano mtoto akabemendwa akabaki na afya yake mzuri ila akawa mlegevu na kushindwa kutembea na darasa hapo ndugu zangu.
Mkuu kwanza naomba umpuuze mleta maada maana ni muongo...

Scientifically hio imani ya kubemenda ni uongo....mwanamke baada ya kuzaa anaruhusiwa kufanya mapenzi na hakuna njia ambayo manii zinaweza kumdhuru mtoto (never)
 
asante ndugu kwa darasa. Ila magonjwa mengi ya zinaa yanasababishwa na bacteria kasoro ukimwi peke yake ndio unasababishwa na virus na ndio maana ni ngumu kuutibu. Ila hayo magonjwa mengineo ya zinaa (STD) yanatibika kwa antibaotics.
Na pia nahisi maelezo yako umechanganya kati ya bactreria na virus. Bacteria ndio wanaoishi katika mwili wa binadamu na kutengeneza enzymes mbali mbali kwaajili ya kumsaidia binadamu. Ila virusi vina muingia binadamu kwenye chembe chembe hai za damu (blood cell) kwa lengo la kushambulia. Nadhani ulichotaka kumaanisha ni kwamba kuna antibody na antigen.

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hata kama mwanamke atafanya zinaa na mwanaume mwingine hakuna madhara ya kibaiolojia yanayoweza kumpata mtoto (
 
hapa ishu ni usafi ,hata kama ni mkeo unapiga mzigo na kumnyonyesha mtoto lazima ataharisha tu
 
Mkuu hata kama mwanamke atafanya zinaa na mwanaume mwingine hakuna madhara ya kibaiolojia yanayoweza kumpata mtoto (
ndugu nimeshawahi kuwa na mahisiano na mke wa mru mwenye mtoto wa miezi 5,alitembea akiwa na miezi 9 hakuna cha kubemenda wala nini.huo ni utapiamlo unaosababisha hali hiyo
 
ndugu nimeshawahi kuwa na mahisiano na mke wa mru mwenye mtoto wa miezi 5,alitembea akiwa na miezi 9 hakuna cha kubemenda wala nini.huo ni utapiamlo unaosababisha hali hiyo
Afadhal mkuu uwaelimishe.....
Kubemenda ni imani potofu..
Labda wazee wetu waliweka ili kuwafanya wanawake wawe waaminifu tu
 
Mada nzuri ila uongo mwingi hata sisi wa fundamental biology tumekushtukia matango yako
 
Mada nzuri ila uongo mwingi hata sisi wa fundamental biology tumekushtukia matango yako
Mkuu hapa ndio sehemu ya kupeana Elimu badala ya kuponda elezea unachojua kuhusu mada husika utakua umesaidia jamii kwa ujumla.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…