Mtoto Jela Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto Mwenzake

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MTOTO James [14] mkazi wa kijiji cha Senani Wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kumlawiti mtoto mwenzie mwenye umri wa miaka mitano.
Sambamba na hukumu hiyo pia amepewa adhabu ya kuchapwa viboko vipatavyo sita akiwa ndani ya gereza .

Hukumu hiyo imetolewa jana katika mahakama ya wilaya na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Maswa, Tamphon Mtani na upande wa Mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Kidwadi Kalinga.

Hakimu huyo aliieleza mahakama kuwa ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi na mshitakiwa mwenyewe kukiri kufanya na kutenda kosa hilo mbele ya mahakama.

Ilidaiwa kuwa Mei 15, mwaka huu, majira ya saa 10 jioni, mtoto huyo akiwa ndani ya nyumba anamoishi alimwita mtoto mwenzie (jina limehifadhiwa) aingie ndani alimokuwepo wakati mtoto huyo alikuwa anacheza na wenzake jirani na nyumba hiyo.

Ilidaiwa alimwomba mtoto huyo aingie ndani ili ampatie pipi na alipoingia alianza kumwingilia sehemu zake za siri mbele na za nyuma na mtoto huyo kuanza kupiga kelele na kusikika na watu waliokuwa karibu na eneo la tukio.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa James alikimbia kwa kutumia baiskeli kutokana na hofu ya kukamatwa aliyokuwa nayo lakini alikamatwa baadae baada ya watu kumuona akiwa kama amechanganyikiwa.

Watu walipoingia ndani kwake walikuta mtoto aliyelawitiwa akiwa na hali mbaya na anavuja damu katika maeneo yote aliyoingiliwa.

James alifikishwa kituo cha polisi na kufunguliwa mashtaka ya kubaka wakati mtoto aliyelawitiwa aliwahishwa hospitali.
 
Viboko sita mbona vichache jamani? Kangetakiwa kufukuzwa kwenye mbigili au kafungiwe nyuma ya gari afu kaburuzwe kwenye lami.
 
kabaka na kulawiti..... huu ni unyama usiomithilika,kama kungekuwa na adhabu zaidi hiyo aliyopewa nafikiri ingefaa zaidi
 
wangekanyonga kabisa, shetani mkubwa huyo!!

Huyu sio mtoto ni jitu zima, miaka ilikosewa kuwa recorded correctly huko usukumani, mob justice should have taken course to get rid of such devil in the society at an earlystage. Nina uhakika jitu hilo likiomba rufani litashinda kwe kadri prosecution zinavyofanyika huko mawilayani. Kuna law technicalities nyingi kwenye hayo mambo in such a way prosecution side isipokuwa makini jitu hilo litashinda huko mbele
 
Back
Top Bottom