Mtoto huyu anaomba msaada wenu tafadhali

tondoli

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
207
51
Habari wanajamii, nakuja mbele yenu nikijaribu kumuombea msaada wa kumsomesha mtoto Swahila anaishi hapa Dar. Mtoto Swahila alifaulu kwenda secondary mwaka jana, kwa bahati mbaya mpaka sasa hajaanza shule. Kipindi cha mwanzo baba mtu alisema hali yake kifedha siyo nzuri akabidi amwanzishe mtoto wake huyu tuition akisubiri hali yake kifedha iweze kutengamaa, lakini cha ajabu majuzi amesema hawezi kumsomesha huyo mtoto kwakuwa kwa sasa anataka kujenga nyumba nyingine. Kati ya wazazi wawili mama anataka mtoto aende shule wakati baba anataka mtoto aolewe au amtafutie kazi ya kufanya na kwa bahati nzuri mtoto anapenda sana shule. Kumbuka huyu mtoto ndio kwanza ana miaka 14. Ombi langu kwenu ni kwamba kama kuna mtu yoyote au taasisi yoyote ambayo inaweza kumsaidia huyu mtoto tafadhali na imsaidie. Mimi ni msamalia mwema tu. Namba yangu ya simu ni 0756572287 au namba mama wa mtoto ni 0714 55 40 81. Au kama kuna mtu anayo namba ya mbunge wa Kisarawe ndg, Selemani Jafu naomba, nimeambiwa huyu mbunge anaweza kumsaidia.

ASANTENI SANA.
 
Back
Top Bottom