Mtoto amepotea

Tracy, tafadhali weka maelezo zaidi:
  1. Recent photographs of the baby
  2. Alionekana wapi mara ya mwisho (be as specific as possible)
  3. Alionekana lini mara ya mwisho (time and date)
  4. Alikua na nguo gani alipo onekana mara ya mwisho
  5. Alipotea katika circumstances gani (mnahisi kaibiwa au kapotea tu)
  6. Anajua kusema?
  7. Akipatikana apelekwe wapi? kuna number ya sim?
  8. Kamakuna vitu kama ugonjwa wa mtoto/alegry etc bora utaje ili atakae mpata asiweke maisha yake hatarini.
Poleni sana, be strong. Atapatikana safe, Insh'allah.
 
Inshaallah Mungu amjaalie apatikane salama, safe and sound
Poleni sn, any inf usiache kutujuza, we pray for the little boy
 
Tukio hili limenikumbusha mwaka juzi nikiwa na shida zangu binafsi nilifika kituo kimoja cha polisi nikakuta watoto wa kati ya miaka kumi na mbili wamekaleta kituoni katoto ka miaka kama mitatu hivi ka kike wakidai wamekaokota.

Kitendo cha mimi kuingia pale mapokezi nikaongea na askari mmoja na kuondoka si kale katoto kakaanza kunifuata huku kananililia nikitaka kuondoka tena kanalia kanasema kananitaka mimi. Ilibidi OCS achukue jukumu la kunikabidhi katoto kale, kwa kuwa nilikuwa nafahamika pale kituoni niliambiwa we nenda nako atakapokuja mzazi wake tutamuelekeza kwako aje amchukue mwanae.

Niliondoka naye mpaka nyumbani nikamwambia wife katoto haka kamepotea nimekapata kituo cha polisi kamenililia sana hivyo nimekabidhiwa nikae nako hadi hapo mzazi wake atakapopatikana.Kweli namshukuru sana wife si kama baadhi ya wanawake wengine hakuonyesha kumchukia mtoto yule alikaogesha kwa kuwa tulikuwa na mtoto wa umri ule alichukua nguo za mwanetu akakavisha.

Tulikaa nae kwa siku tatu ndipo mzazi wake alipokuja kumchukua. Mzazi wake (mamake) alipomwona alitokwa na machozi ya furaha.
 
Let's just hope little Collins finds a host as kind as you...
 
pole Tracy tunategemea utakapo kuja tena utakuwa na habari njema
 
Tracy, what happens to the Katoto please? We are all worried!! Tell us kama kamepatikana.
 
Tracy tuwekee taarifa za polisi kama mtoto bado hajapatikana
 
thank you for all the support Jf members, mtoto bado hajapatikana.



he last time alikuwa nyumbani and kwa bahati mbaya gate lilikuwa wazi, that's when he went missing.
 

Attachments

  • 308453_184879914932503_100002314871960_362240_666831632_n.jpg
    25.1 KB · Views: 487
mods thank you kwa kueka kwa sticky.samahani sikuweza kueka the picture earlier but thats the baby who is missing,kwa yeyote ataemuona.

Please help, mbarikiwe wote.
 
thank you for all the support Jf members, mtoto bado hajapatikana.



he last time alikuwa nyumbani and kwa bahati mbaya gate lilikuwa wazi, that's when he went missing.
Oh God, the boy is cute. Mungu muwekee ulinzi wa malaika wako mpaka wazazi wake wampate.
 
hili tatizo la kupotea watoto kwa sasa ni kubwa sana
hata jirani yangu amepotelewa na mtoto wake
japo wanafanya siri na sijajua hiyo siri imetoka wapi.
 
Kwa imani Collin atapatikana tu kwani Mungu ni mkuu. Ila matangazo yapelekwe hata kwenye nyumba za ibada itasaidia pia kwani watz hatuna utamaduni wa kusoma mbao za matangazo wala vipeperushi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…