Mtoto amepotea

Shakazulu

JF-Expert Member
Feb 23, 2007
957
281


Samwel Prosper Nyoni.jpg

Jina:
Samwel Prosper Nyoni

Umri: Miaka 10

Shule: Olimpio



Mtoto huyu amepotea. Alikuwa anaishi mabibo na huko ndiko alionekana mara ya mwisho. Alikuwa amevaa t-shirt ya kijivu na kaptula ya dark blue ambayo kwa nyuma ina maandishi ya kaki ya namba 19 and 26. Miguuni alikuwa amevaa yeboyebo za blue. Kichwani anaugonjwa wa ngozi unaosababisha aonekana kama ana mvi.


Baba yake anasema kuna watu walimuona ubungo terminal akiwa ameshikwa mkono na msichana amabye ni mkubwa kidogo kwake ambaye ndiyo anamuongoza.


Tafadhali atakayemwona anaombwa awasiliane na baba yake kwa namba 0773197550
 
Aisee! In sha Allah M'Mungu atawaongoza! Wizi wa watoto umerudi sasa! Naona kila siku wanatangaziwa ktk ITV saa 12 jioni
 
Tunawashukuru wote kwa sala na dua zenu. Mtoto Samwel amepatikana na kurudishwa salama kwa wazazi wake. Alipatikana Jumapili usiku maeneo ya uwanja wa Karume. Asanteni sana.
 
Baada ya Asante zako hembu tuambie alipotea katika mazingira gani na alipatikana vipi.
Ili kama kuna uzembe wengine tujifunze humu,maana tunawatoto
Haya tupe ushuhuda

Mtoto alikuwa anacheza nje na wenzake ndipo alipokuja dada mtu mzima na kumchukua as if anamjua maana alimshika mkono wakawa wanaongea huku wakikata mitaa na kutokomea kusikojulikana. Kuhusu kupatikana kwake ni kuwa kuna askari wa kituo cha Msimbazi alisaidia katika upelelzi ndipo walipomkuta akirandaranda maeneo ya Uwanja wa Karume. Mtoto mwenyewe haelezi kiundani what happened kwa hiyo inakuwa ngumu kujua huyo aliyemchukua alimpeleka wapi na kumfanya nini.

All in all tunamshukuru Mungu kuwa amepatikana akiwa mzima.
 
Asante sana kwa Taarifa.
Ila kama ni Muislam basi huyo mtoto mumsomee kisomo cha rukhiya na kama ni Mkristo basi mpeleke kwenye maombi maalum kabla ya kuchanganyika na wenzake.

Kimtizamo tu ni kwamba kuna kitu kinaweza kuwa kilifanyika,maana mtoto ni mkubwa na uwezo wa kujieleza lazima awenao,ila kuna hali inaweza kuwa inamfanya awe hivyo.

Kupatikana akiwa mzima wa mwili ni suala la kumshkuru mungu,ila suala la uzima wa akili na utata lazima kumpe mungu amsafishe mtoto huyo kwa maombi maalum,ili kama kuna mambo ya kishetani au kichawi yaweze kumtoka na kumkwepa.Dunia imebadilika saana siku hizi

Bwana Mungu Asifiwe
 
Back
Top Bottom