Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,403
- 1,241
Yale makuu mliyo hisia kuhusu huyu mtoto yamewadia:
MTOTO aliyemuhoji swali Waziri Mkuu Edward Lowassa, Aron Wambura Shera anadaiwa kuandamwa na maofisa usalama wa taifa wakimhoji kila mara kuhusiana na swali alilouliza.
Habari kutoka kwa ndugu wa karibu wa kijana huyo, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Pius Msekwa kidato cha kwanza, zimedai kuwa maofisa hao siku hiyo ya mkutano walimfuata mwalimu wake na kumtaka amweleze historia ya kijana huyo.
Akiwa wilayani Ukerewe katika ziara, mwanafunzi huyo alimuuliza swali Waziri Mkuu kuwa viongozi wamekuwa wakiwaambia kuwa mshika mawili moja humponyoka na kuwa vijana ni taifa la kesho, wasome ili kulitumikia taifa vipi wao wamekuwa wakirundikiana vyeo zaidi ya kimoja na kutoa mfano uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk Alex James Msekela kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa ilhali ni mbunge.
Swali hili halikujibiwa na Waziri Mkuu baada ya kujibu maswali mengine na kumaliza hotuba yake bila ya kujibu hatua ambayo iliwafanya wananchi katika mkutano huo kumkumbusha kujibu na yeye kuwaeleza kuwa atarudi siku nyingine.
"Tangu siku hiyo katika mkutano alifuatwa na watu wakijitambulisha kuwa wao ni maofisa toka usalama wa taifa na kumtaka awaeleze juu ya swali hilo iwapo kafundishwa na mtu hatua ambayo ilimshangaza kijana na kushindwa kuwajibu," alieleza kwa simu mmoja wa ndugu na jamaa wa kijana huyo ambaye aliomba asitajwe jina gazetini.
Alisema kuwa kutokana na kijana kushindwa kuwajibu vyema walikwenda kuuliza kwa wanafunzi wengine ili kujua anasoma kidato cha ngapi na kuomba majina ya walimu wa kidato cha kwanza kwa lengo na nia ambayo haijajulikana hatua ambayo imewatia woga.
Alisema ndugu huyo kuwa kutokana na hatua hiyo wanahofu huenda haki na uhuru wa kujieleza kwa kijana huyo huenda ikamtumbukia nyogo hata akapoteza masomo au walimu wake wakapoteza kazi.
Chanzo: Mwananchi
SteveD.