Mtoto albino awafukuza waliokata mkono wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto albino awafukuza waliokata mkono wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 24, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MLEMAVU wa ngozi aliyekatwa mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana, Kulwa Lusana (16), amesimulia alivyojikuta akiwafukuza wavamizi hao, huku akilia na kuwaomba wamrudishie mkono wake.

  Kulwa ametoa maelezo hyao Polisi jana na kuongeza kuwa juhudi hizo za kudai kurudishiwa mkono wake, hazikuzaa matunda, kwani wakataji hao walizidi kutokomea gizani na kumuacha akitapatapa.

  Baada ya kupoteza matumaini ya kuupata mkono wake, Kulwa alisimulia kwamba akiwa anagugumia kwa maumivu makali, alikimbilia kwenye nyumba ya baba yake ambapo aligongana naye mlangoni na wote kuanguka chini.

  Mlemavu huo alifanyiwa unyama huo juzi saa 7 usiku katika Kijiji cha Mbizi, Kata ya Segese wilayani Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani alisema watuhumiwa hao walivunja mlango na kuingia ndani kwa albino huyo na kuanza kumshambulia na kumjeruhi sikio na baadaye wakakata mkono wake wa kulia na kuondoka nao.

  Kwa mujibu wa Kamanda Athumani, albino huyo alipiga kelele ya kuomba msaada kwa baba yake, Lusana Nkola ambaye hata hivyo wakati akitoka katika harakati za kumuokoa mtoto wake huyo, alipigwa jiwe kichwani akaanguka chini.

  Alisema baada ya kufanyiwa unyama huo, watu hao waliufunga mkono huo kwenye mfuko na kuanza kukimbia nao na kutokomea pasipo julikana na kumuacha albino huyo akigugumia kwa maumivu makali.

  Kutokana na tukio hilo, Polisi inamshikilia Petro Nkola mkazi wa kijiji cha Mtukula Runzewe wilayani Bukombe ambaye ni baba mdogo wa mlemavu wa ngozi, Kulwa Lusana (16).

  Hata hivyo, Kamanda Athumani hakutaka kueleza kwa undani sababu za kumshikilia baba huyo zaidi ya kufafanua kuwa ni kwa mahojiano zaidi na uwezekano wa kuwapata watuhumiwa wengine waliotoroka na mkono wa mlemavu huyo.

  Kulwa kwa sasa yupo katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama akiuguza jeraha lake na hali yake inaendelea vizuri.

  Kamanda Athumani aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watu wote watakaowadhani kuwa ni washiriki wa tukio hilo la kinyama alilofanyiwa mtoto huyo.

  Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tu baada ya mlemavu mwingine wa ngozi, Adam Robert (14) kujeruhiwa kwa kukatwa na sime mkono wa kushoto na kunyofolewa vidole vya mkono wa kulia huko katika Kijiji cha Nyaruguguna wilayani Geita, mkoani Mwanza.

  Katika tukio hilo la Geita, baba mzazi na mama wa kambo wa mtoto huyo, wanashikiliwa kwa tuhuma hizo.
   
 2. B

  Bijou JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145


  hivi watanzania, hii aibu ya kuua albino itaisha lini??????????????????????????? hivi inaingia akilini kweli??????????????????? shame on you all wenye mawazo ya kishirikina. Bwana na awafunue akili zenu
   
 3. M

  Msanya Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Waganga wa kienyeji wanajulikana na wanatumiwa na baadhi ya wenye uchu wa mali na baadhi ya wenye uchu wa madaraka.
   
 4. l

  lumimwandelile Senior Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  inasikitisha sana, nani ataikomesha hii hali?
   
 5. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hii kitu inanichefua sana na cjui nini hatma yake
   
 6. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hivi zile kesi za walio ua albino zilizo kuwa zinendelea wkt ule
  ziliishia wapi?? au ndio ziliishia juujuu tu???
  ingetolewa adhabu kali kwa wanao fanya uhalifu huo labda ingesaidia
  kukomesha vitendo hivi.
   
 7. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Inauma kweli,huo ni ukatili kwa upuuzi wa imani za kijinga
   
 8. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu walipata adhabu ya kifungo cha maisha,lakini wa2 hawakomi na hawana huruma.
   
 9. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  ni aibu kweli, kule kenya jokes za albino huwa wanaambiwa kuwa watapelekwa tanganyika!
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kuna walakini ktk uhusika wa wakubwa ktk hili
  ngekuwa jaji nawahukumu kuuwa kwa kupigwa mawe
  tena mbele ya halaiki bila kusubiri JK kusaini hati ya kifo
  inakera na kuuma kwauamini ushirikina
   
 11. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  adhabu itayo simamisha hi unyama.ni KUNYONGA TU.alafu waone kama wataendelea
   
 12. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  inatisha jmn na inasikitisha Mungu awarehemu nakuwafungua fahamu zao hawa watu mweee!
   
 13. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,744
  Trophy Points: 280
  Haina haja ya kuwapeleka huko
  mahakamani na nyie mnamkata kiungo kimoja baada ya kingine ndo wajue maumiv wanayoyapata wenzao pumbav kabisa!
  Ni kama wale wanaopiga wenzao nondo yaani ushirikina ni jambo la hovyo sana.na hawa waganga nao ua kabisa ndo chanzo cha uhayawani huu
   
 14. l

  lupaso Member

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii mijitu ya kanda ya ziwa (shinyanga na mwanza) ilifaa wayahamishe yote wapelekwe either kwa alshabab maana inatutia aibu ya karne wabongo au serikali wahamishe watu wa kusini na kaskazini na kuwapeleka huko na wao kuwapunguza mikoa mingine ili kudilute tabia zao za hovyohovyo
   
 15. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,744
  Trophy Points: 280
  masaburi yao hawa si ndo wanauaga
  vikongwe wenye macho mekundu!
  Hivi huyu kijana anaeuwa!!
  Anakumbuka kuwa nayeye anaelekea ukikongwe?so nayeye
  huko mbele auwawe??
  Pmbav kabisa alaaaa.
   
 16. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  labda ni dawa za kumaliza kesi za mafisadi maana hukumu inasusua sana na adhabu ni ndogo, dawa ni kuwapiga mawe hadi kufa
   
Loading...