Mtoto afanyiwa ukatili shuleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto afanyiwa ukatili shuleni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 23, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule moja ya msingi ya jijini Dar es Salaam, inayotoa elimu yake kwa lugha ya Kiingereza, amejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kuchapwa bakora akiwa uchi.

  Habari zilidai kuwa kitendo hicho dhidi ya mwanafunzi wa kike, kimefanywa na mhudumu wa usafi katika mabweni ya watoto.Inasemekana kuwa mtoto huyo alichapwa Juni 14 mwaka huu, baada ya kukataa kufua nguo yake ya ndani, aliyoikuta ikiwa imetapakaa kinyesi cha mtu ambaye hakufahamika.

  Kubainika kwa ukatili dhidi ya mtoto huyo, kumekuja baada ya mama yake mzazi, Teddy Salimwe, kuamua kumtembelea Juni 20 mwaka huu kwa lengo la kumjulia hali.Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Teddy alisema alipokutana na mtoto wake, aliamua kumpakata lakini mtoto alikuwa analia kwa maumivu makali yaliyotokana na majeraha.

  Alisema baadaye alimdadisi mtoto huyo, ili kujua kilichompata na kwamba katika maelezo yake, mtoto alidai kuwa alikuwa amechapwa bakora na mhudumu wa usafi.

  Alisema baada ya maelezo hayo, alimwendea Mwalimu mkuu ili kupata maelezo ya kina kuhusu sababu za mtoto kutendewa ukatili huo.Kwa mujibu wa Teddy, kiongozi huyo wa shule, alimwelekeza kwenda kwa msaidizi wake ambaye hata hivyo, alishindwa kutoa maelezo na badala yake, alimtaka kuondoka na mtoto kama alihisi kuwa adhabu aliyopewa hakustahili.


  Alisema kauli ya mwalimu huyo msaidizi, haikunifurahisha jambo lililomlazimisha kurudi kwa Mwalimu mkuu ili kupata ufafanuzi zaidi, lakini naye hakuonyesha ushirikiano.Teddy alisema kitendo hicho kilimsukuma kwenda polisi ambako alitoa taarifa na kupewa RB yenye namba STK/RB/8990/11.

  Akisimulia chanzo cha kuchapwa bakora, mtoto huyo alisema ni kukataa kufua nguo yangu ya ndani niliyoikuta ikiwa na kinyesi kitandani kwangu, sikumjua aliyeitumia kujifutia kinyesi chake."

  Alisema pamoja na jitihada zake za kujitetea, mhudumu wa usafi alimchapa kwa kutumia bakora maalumu kwa madai kuwa ni mjeuri.""Alinichapa kwa muda mrefu kwa kutumia fimbo ya 'Mr Bluu, nililia sana tena kwa sauti kubwa ambayo naamini wanafunzi wote walisikia nilivyokuwa nikichapwa huku nikiwa uchi,'' alidai mtoto huyo.

  Alidai kuwa baada ya kumchapa, mhudumu huyo alimtaka aisitoe kwa mtu yeyote, taarifa kuhusu kipigo hicho, jambo lililomfanya aendelee kulia kwa maumivu yaliyomfanya ashindwe kutembea wala kufanya chochote.

  Mwandishi wa habari hii alimtafuta Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Nashon Fanuel Rhobi na kumuuliza kuhusu tukio hilo.Katika majibu yake, kiongozi huyo wa shule alisema alikuwa hafahamu kama mtoto huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kiasi hicho.

  Ofisa Habari wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (WLAC), alisema chama hicho kimepokea taarifa kuhusu ukatili huo na kwamba inazifanyia kazi.
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  you put those brats of ur's ktk vi international vya uswaz watu wamepinda wamechoka watoto wanaleta kudeka deka my mum my dad cjui nini, watu wanawazibua alaaah
   
 3. A

  Aine JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  \
  Halafu wewe!!!!!!!!!! umenitia hasira hadi nashindwa niongeeje!
   
 4. A

  Aine JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza pole sana mama mwenzangu, pia nashauri amuahamishe mtoto huyo haraka kwani hao walimu hawana ushirikiano kabisa na hakikisha sheria inachukua mkondo wake hapo. Huyo mwalim mkuu hata kama hana taarifa si anatakiwa afuatilie ili ajue undani wa tukio hilo? tena angetakiwa amuite huyo mhudumu mbele ya huyo mama ili aseme kilichosababisha ampige mtoto hivyo!! yaani shule zingine ni after money basi!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Hizi shule yaani unalipa mamiliono mwanao anateseka
  na kuna vitendo vya kunajisiana kwa wavulana pia...
  Na shule zingine unakuta wanafunzi kwenye daladala
  na bado mzazi kalipia mamilioni...
  Ujinga mtupu
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tumezipokea hizi shule bila kujiandaa.
  Tumeachia watoto wetu walezi wasio kuwa na ujuzi wala wito wa kulea
  Watoto wanafanyiwa ukatili wanabakwa nk. kwa kwli ni balaa
   
 7. yatima

  yatima JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  tunaomba jina la shule - kwani kama mmiliki naye hawezi kuingilia kati basi hiyo SHULE IJULIKANE TUSIPELEKE WATOTO WETU - HAPO

  yaani huyo mhudumu ni mvuta bangi au????? na huyu mwalimu hana taarifa?????? sasa mama wa watu alipokuwa anamweleza alikuwa anapiga chenga za nini??? - HIYO SIYO SHULE - LABDA NI KITUO CHA MASHETANI - imeniuma sana sana na kuniumiza - PLEASE LET THE NAME OF THIS SCHOOL MADE PUBLIC FOR EVERYBODY TO KNOW IT
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Huyu mzazi pumbafu zake....
  Unampeleka mtoto wa umri kama huo shule ya bweni....
  Bora angecha kuzaa....pumbafu kabisa....! Huyu mama (na baba wa mtoto) hakustahili kuwa wazazi.....
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mbaya sana hii!
  Wazazi wa huyo mtoto wapo?...Kama wapo wanatakiwa kudai demages za kufa mtu, na mtoto ahame fasta!
  Kuna shule nyingi za jamii hiyo nzuri mno!
   
 10. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono unakuta mzazi yupo hapa lakini anasukumia mzigo wa malezi kwa watu wengine tena kwenye umri huo.

   
 11. m

  mancy Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umekosea kidogo Huyo muhudumu ulitakiwa kwanza umpe kichapo cha nguvu kwa mikono yako, vichwa, na mateke alafu akueleze kama amezaa na kama amezaa mwanae angefanyiwa hivyo angefurahi? Hana akili kabisa tupe jina la shule na la huyo mkuu wa shule tulifanyie kazi . Unalipa na siyo bure.
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kamishina wa ustawi wa jamii kawa bongolala nadhani anachofaidi pale wizarani ni posho tuu,sijasikia hat siku moja akikemea huu unyanyasaji wa watoto katika maeneo mbalimbali mara huyu kalawitiwa,kabakwa,kachomwa moto,kachunwa ngozi,kakatwa kiungo,kauawa,yeye yuko kimyaaaaaaaaaaa,hjui hili ni janga la kitaifa mpaka NGos waseme jamani nchi hii mimi nashindwa kabisa kuilewa hii serikali
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,963
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  Maadili hamna kwenye shule hizi zinazoibuka kama uyoga.
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,471
  Trophy Points: 280
  Nilijua ni avatar yako lakini naamini kwa majibu yako ni kweli unapuliza.
   
 15. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,471
  Trophy Points: 280
  Inawezekana hilo ni moja kati ya mambo mengi wanayotendewa hawa malaika huko kwenye hizo shule za kiingilish.
   
Loading...