Mto wa Magole wawatesa ma ENGNEER

ally ndunda

Member
Jun 2, 2013
23
3
Mto huu Wa magole uliopo mkoa wa morogoro ni mto wenye historia ndefu ambayo huongoza kuhama hama sana. Mto huu umetokea katka vijiji mbalimbali vikiwemo mkundi na vingine.

Mto huu wa Magole kwa sasa unaathiriwa na mchanga mwingi unatokana na maji madogo na mengi yanayotoka mitaani na vijito vidogo.

Mto huu wa Magole umekatisha barabara ya kwenda Dodoma na Morogoro. Pembeni ya mto huu kuna barabara inayokwenda Turiani.
Daraja la mto huu lilikua na kina kirefu sana lakini kwa sasa kina hicho kimepungua sana toka mita 20 mpaka 7. Hali ambayo maji yanayopita ktk daraja hilo husabisha kupita kwa shida na kutafuta njia mpya kupita.

Mto huu wa MAGOLE kwa sasa umetanuka sana kwa kua hauna kingo zilizojengewa pale unapoingia darajani. Kutanuka kwa mto huu kumefanya mashamba yaliopo jirani kupata mchanga mwingi na kushindwa kulima mazao kama mahindi.

Kuzuiwa kuchimba mchanga kwa wananch ktk mto huu kumeendelea kupata mtanuko unaoendelea kila siku kwa kua hauna kingo za kuzuia maji yasisambae.


Serikali kuzuia maji kwa matuta ya mchanga ni kupoteza pesa za walipa kodi bure. Leo ukipita ktk mto huo utaona serikali ilivyopoteza pesa nyingi kwa kuweka matuta ya mchanga, na kusambazwa na maji yanakuja kutokana na mvua ilioanza kunyesha hivi sasa.


Hivi sasa Serikali ianze kujenga ukuta mkubwa walau mita 2000 toka usawa wa daraja. Lakin pia waruhusu mchanga huo sasa kuchimbwa ili kutengeneza kina cha maji.
Kutoruhusu kuchimbwa mchanga ktk mto huo na darajani hapo MAGOLE kutaendelea kujaa mchanga na kusababisha maji hayo hayo kutanua mto na kupita juu kwa maji hayo.

Ndugu zetu Wasomi Ma ENGNEAR TUNAJUA mnaelimu kubwa lakin ktk hili haliitaji Elim ya chuo kikuu. Kaeni na wadau wananchi wanaoishi maeneo haya wawasaidie mawazo.

ELIM YANGU NDOGO INATOSHA KUSEMA HAYA.


AHSANTENI
 
Engineer hajawahi kushindwa..utakuwa ni mchimba mchanga yule wa pale Flomi..
 
Back
Top Bottom