Mtizamo wa Bloga: Uamuzi wa CHADEMA Kususia Hotuba ya Kikwete Bungeni

Evarist Chahali

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,758
Suala ambalo limetawala maongezi ya Watanzania wengi kwenye social media kwa leo ni kitendo cha wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati anazindua Bunge jipya mjini Dodoma.Kwanza niweke wazi msimamo wangu kuwa naunga mkono uamuzi huo wa Chadema.Sifanyi hivyo kwa minajiki ya kukipenda chama hicho bali ni katika kuzingatia ukweli kuwa Chadema wametumia HAKI yao ya Kikatiba na kidemokrasia kuonyesha upinzani wak kwa vitendo.Nimeandika HAKI kwa herufi kubwa kwa vile neno hilo ni muhimu katika "kuwahukumu" Chadema.

Baadhi ya wenzetu wamekishutumu vikali kitendo hicho huku wengine wakikiita "utovu wa nidhamu wa hali ya juu".Lakini wakati wenzetu hao wanatumia HAKI zao za Kikatiba na kidemokrasia kuwalaumu Chadema,hawataki kutafakari japo kidogo kuhusu HAKI kama hizo kwa chama hicho,yaani HAKI yao ku-protest kwa amani dhidi ya mwenendo mzima wa uchaguzi uliopelekea Jakaya Kikwete kuwa Rais tena.

Inawezekana tukio hilo linaonekana sio la kawaida kwa vile ni mara ya kwanza kutokea nchini.Lakini kwa wanaojishughulisha kufahamu kinachoendelea sehemu nyingine duniani watafahaku kuwa hali hiyo imeshatokea kwenye mabunge mbalimbali,kwa mfano nchini Afrika Kusini,Gambia,Sudan, India,Pakistan na Iraki,to mention only a few.

Kwa namna moja au nyingine,vipengere dhalimu vya Katiba yetu vimewaacha Chadema na alternatives chache zaidi ya hatua kama hiyo ya leo kwa vile Katiba yetu inanyima uhuru wa kupinga matokeo ya ushindi wa Rais mahakamani hata kama ushindi huo umepatikana kwa njia zisizo halali.Leo mapungufu hayo makubwa kwenye Katiba yetu yanaweza kuonekana kama jambo dogo.Lakini yayumkinika kuamini kuwa inaweza tokea tukapata Rais dikteta ambaye ameshindwa kwa mabavu lakini tukajikuta hatuna njia ya kupinga "ushindi" wake kwa vile Katiba inamlinda.

Tatizo la Katiba nyingi katika "Nchi za Dunia ya Tatu" na hususan barani Afrika ni ile tabia hatari ya katiba hizo kutumika kwa mahitaji na maslahi ya watawala walio madarakani.Na kwa vile wengi wa watawala hao ni walafi na waroho wa madaraka,na kwa vile madaraka makubwa waliyonayo yanawapa uhuru wa kufanya lolote wapendalo,katiba hizo huwekwa viraka hapa na pale sio kwa minajili ya ustawi wa taifa husika bali kikundi kidogo cha watawala.

Laiti Katiba ingekuwa inaruhusu ushindi wa Rais kupingwa mahakamani basi ni dhahiri Chadema wangeshafungua kesi.Kuna wanaosema "sasa wakitoka nje ya Bunge ndio inasaidia nini?"Majibu ni mengi ila hapa nitatoa machache tu.Kwanza,ikumbukwe kuwa Chadema ndio chama kikuu cha upinzani bungeni.Pamoja na uchache wa idadi ya wabunge wao ukilinganisha na wale wa CCM,hadhi ya chama kikuu cha upinzani ni kubwa na muhimu ndani na nje ya nchi.Pamoja na mazingira na sheria kandamizi dhidi ya vyama vya upinzani,kwa nchi masikini kama Tanzania kuna kila sababu ya sote kuonekana tumeshikamana hata kama mshikamano huo ni wa kinafiki na unawanufaisha zaidi mafisadi.Ndio maana basi nchi wafadhili zilikuwa zikiwakalia kooni watawala wetu kuhusu upatikanaji wa suluhisho la kudumu huko Zanzibar,ambapo hatimaye CCM kwa shingo upande (na licha ya ngebe za akina Makamba) leo hii tunashuhudia serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar.

Of course,hali ya kutoelewana huko Zanzibar ilikuwa serious sana hasa kutokana na vurugu za uchaguzi zilizopelekea mauaji ya watu kadhaa,ukweli unabaki kuwa msimamo thabiti wa chama kikuu cha upinzani visiwani humo,yaani CUF,kutotambua matokeo ya chaguzi mbalimbali,sambamba na kelele walizopiga kwa jumuiya ya kimataifa ndivyo vilivyopeleka leo hii kuwepo serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwahiyo wanaohoji umuhimu wa wabunge wa Chadema kususia hotuba ya Kikwete wanapaswa kuelewa kuea msimamo imara sambamba na matendo yanayothibitisha msimamo huo yanasaidia kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.Leo pale Dodoma kulikuwa na wawakilishi wa nchi na jumuiya mbalinbali za kimataifa.Vyovyote itavyokuwa,wameguswa na tukio hilo ambalo kwa hakika limetia dola utawala wa Kikwete.Baadhi ya nchi hizo ni wafadhili ambao bila wao basi mambo yanakuwa si mambo.

Lakini jingine la muhimu ni kufikisha ujumbe kwa Kikwete na serikali yake (including vyombo vya dola na Tume ya Uchaguzi) kuwa zama za "ndiyo mzee" zimefika kikomo.Hata kama Katiba inaendelea kuhalalisha sheria dhalimu (kama hiyo inayonyima fursa ya kupinga ushindi wa rais mahakamani) mwanya mdogo wa uhuru wa kidemokrasia kupingana pasipo kupigana unawezesha Chadema kuzalisha harakati mpya za mapambano dhidi ya udhalimu lakini pasipo vurugu au umwagaji damu.Kwa tunaotaka kuona Tanzania yenye kuheshimu na kuzingatia haki na stahili za Watanzania,kitendo cha leo cha Chadema kinafungua ukurasa mpya wa matumaini.Kadhalika,kitendo hicho ni hatua kubwa na muhimu ya kukua kwa demokrasia yetu kutoka vyama vinavyokubali yaishe hata pale penye uthibitisho kuwa vimejumiwa kwenye chaguzi,kwenda kwenye zama ambapo uchakachuaji wa chaguzi unaharamishwa hadharani tena kwenye live tv.Message delivered!

Ni wazi kuwa tukio la leo limemgusa Kikwete na serikali yake kama ambavyo limewagusa Watanzania wengi na jumuiya ya kimataifa.Yayumkinika kuwa inawezekana nguvu kubwa iliyotumika kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita sasa itaelekezwa katika kuihujumu Chadema ili idhoofike na hatimaye kuachana na msimamo wake wa kukataa kumtambua Kikwete.Zitafanyika jitihada za kuwqgombanisha viongozi wa chama hicho kama ilivyokuww kww NCCR-Mageuzi ya Mrema.Kuna uwezekano pia wa Dokta Wilbroad Slaa kuzushiwa zengwe zaidi ya lile ya maisha yake binafsi.Lakini hayo yanaweza kupita pasipo madhara makubwa kwani hata Baba wa Taifa na wenzake walipokuwa wanahangaikia ukombozi wa Tanzania kutoka himaya ya mkoloni walikumbana na vizingiti hivyo.Haya ni mapambano kati ya wenye uchungu na nchi yao dhidi ya wale wanaotaka kuigeuza nchi yetu kuwa "shamba la bibi" na makao makuu ya ufisadi.

Sie Wakristo tunaamini kuwa mwenye haki ataanguka saba mara sabini ( hapa simaanishi kuanguka kama kule kwa Kikwete pale Jangwani) lakini mwishowe atasimama.Kukubali uchakachuaji wa kura kutapelekea matokeo ya ain moja tu: uchakachuaji zaidi.Historia inatufundisha bayana kuwa kukubali kitu kibaya hakusaidii hata chembe kitu hicho kibaya kugeuka kizuri au athari zake kupungua.Wanaoshauri Dkt Slaa na Chadema "wakubali matokeo" hawana tofauti na wanaoweza kusema tuache mapambano dhidi ya malaria au ukimwi kwa vile magonjwa hayo yamekuwepo miaka nenda miaka rudi.

Laiti Nyerere na mashujaa wengine wa mapambano dhidi ya mkoloni wangepatwa na mawazo hayo ya "kukubali yaishe" leo hii tungeendelea kuwa chini ya mkoloni ( I know kuna watakaosema bora mkoloni kuliko fisadi.Mie nasema ukoloni na ufisadi ni mbaya kama ilivyo kwa kansa na ukimwi.Hakuna cha nafuu,wote ni maadui wanaostahili kuangamizwa).Na laiti Nyerere "angekubali yaishe pale Nduli Idi Amini alipotuvamia,basi huends leo tungekuwa sehemu ya Uganda chini ya dikteta Idi Amini au mrithi wake.

Giving up is not an alternative.Mapambano ya kudai haki (kwa amani) lazima yaendelee.Waingereza wana msemo kwamba kukubali kitu pungufu kwa minajili ya bora liende hatimaye hupelekea kupata kilicho pungufu zaidi ya kilichostahili kupatikana.Kadhalika,hatua zote za mabadiliko huanza kwa hatua chache na pengine ndogo lakini zenye impact na hatimaye kutengenrza mazingita mazuri kwa hatua kubwa zenye impact kubwa zaidi na pengine zenye kuweza kuandika historia mpya.Vilevile,actions speak louder than words.Na hiyo imethibitka leo kwani japo Chadema walishatangaza kuwa hawatomtambua Kikwete uzito wa tamko hilo haukuwagusa wengi kulinganisha na tukio la leo la kususia hotuba ya Kikwete.

And by the way,hotuba hiyo ilikuwa na tofauti gani na hotuba lukuki alizotoa wakati wa utawala wake 2005-2010?Hivyo vipaumbele sijui 13 (or were they 19) tulishavisikia kwenye kampeni za 2005 na zikarudufiwa kwenye kampeni za mwaka huu.Kama kuna yeyote aliyechukulia vimpaumbele hivyo seriously all I can say asubiri muda si mtefu atabaini "imekula kwake" as they say in the streets.

KULIKONI UGHAIBUNI: Uamuzi wa Chadema Kususia Hotuba ya Kikwete Bungeni Dodoma
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,277
74,107
Walivyopiga kura kumhakiki Pinda, pendekezo la Kikwete, walikuwa wanahakiki pendekezo la nani ?
 
Nkoboiboi

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
243
63
Nasikia Mkwere anasema waliotoka Bungeni leo watalazimika kumpigia magoti ili awape hela za kuendeleza majimbo yao!!!!
Siamini hilo kama ni kweli - silaha dhaifu!!! Hivi huyu Mchakachuaji hawajui hawa CDM; kwaniCHADEMA ilipokuwa inakua hadi kutoka wabunge 4 hadi 23 aliwapa hela ngapi. Wait and see the creative minds of CHADEMA!!!!!
Naunga mkono hatua ya kutoka mjengoni na nawapongeza wote waliotoka, na hata wale ambao hawakuwepo.
 
MULANGIRA

Member
Oct 10, 2010
74
3
Walivyopiga kura kumhakiki Pinda, pendekezo la Kikwete, walikuwa wanahakiki pendekezo la nani ?

Mbinu halali za kupinga uchakachuaji ni muhimu. Leo wezi wa kura wameaibishwa mbele ya Watanzania na jumuia ya kimataifa wanaanza kulia kama mtoto mdogo. Kwa taarifa ya wengin raisi si baba wala mama yako ni mtu anayechaguliwa kwa utashi wa watu. Katu kamwe mtu asimlinganishe raisi na mzazi yeye ni kiongozi na mtumishi mkuu wa watu. Lakini kama ametwaa cheo hicho kwa wizi hatakiwi kuheshimiwa na wananchi wana kila haki ya kumpinga na kumuabisha. Kikwete na CCM wataaibishwa si tu huku nyumbani pale hata nje ambako nina uhakika Watanzania wenzetu na watu wenye nia njema watajiunga nasi kupambana na utawala huu wa bandia.
 
Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
321
Ndugu Kiranga Heshima sana
leo mara kadhaa nimeoshangazwa jinsi ambavyo umetoa hoja za kitoto juu ya kitendo walichofanya CHADEMA.
Nadhani kukaa kimya ni busara kuliko kukurumuka. Ikiwa chadema ingeshugulika na Pinda isngefikisha ujumbe iliokusudia katika jumuiya ya kimataifa kwa nguvu na uzito wa pekee kama ilivyotokea jana.
Kumbuka aliyetangazwa mshindi na nec si Pinda ila Kikwete na kwa hiyo hapo palikuwa mahali sahihi kabisa kufanya kitendo walichofanya. Ulimwengu umeelewa na nakuhakikishia kuw jambo hili litamsumbua rais wa JMT popote atakapokwenda nadni na nje ya nchi. Wale watoa fedha watamsumbua na maswali ya kero ambayo asingependa kuukulizwa na hatimaye njia itapatikana.
 
Umesema mengi lakini hujajibu swali langu.
 
Hoja za kitoto kwa sababu nahoji sincerity na consistency ya CHADEMA ?

Kukurumuka mambo ya Kalemie au wapi hayo?

Kwa uelewa wako mdogo, unafikiri ninapoongelea habari ya CHADEMA kushiriki uhakiki wa Waziri Mkuu, naongelea habari ya Pinda. No wonder unameza vitu vizima vizima bila kumung'unya.

Kwa kushiriki uhakiki wa Pinda, chaguo la Kikwete, wabunge wa CHADEMA wamemtambua Kikwete kama rais tayari, sasa sijui hizi habari za kutomtambua Kikwete zinaanzia wapi wakati walishamtambua mpaka kupigia kura chaguo lake la Waziri Mkuu.

CHADEMA hawana consistency wala maturity ya kuchukuliwa seriously, nililisema kabla na sasa wanadhihirisha hili.
 
rmb

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
223
6
Jamani hamwoni mabunge ya wenzetu hawaendeshwi endeshwi tu na mtu wapo bungeni kutetea haki za wananchi wao ndo maana wanatwangana hata ngumi ndani ya bunge! lakini Bongo ni ndio mzee mtindo mmoja! Safi sana CHADEMA mwanzo mzuri
 
MULANGIRA

Member
Oct 10, 2010
74
3
Umesema mengi lakini hujajibu swali langu.

Swali lako linaonyesha upeo mfupi wa kufikiria wao wamebuni mbinu za kuiabisha CCM na mbinu hizo ni pamoja na kushiriki katika vikao vya bungeni kwa uchaguzi mkubwa. Kama ambavyo Matiba alikuwa anafanya alikuwa anaingia na kuonekana bungeni kiufundi "technical appearance." Hivyo mkoba wa mbinu za chadema katika kupambana na udhalimu huu ni nyingi na ninakuomba ufunge mkanda.
 
Mzuvendi

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
561
542
Waziri mkuu ameteuliwa na JK. Kwanini basi wasingejitoa? Kukaa ndani na kushiriki katika upigaji kura hata kama kura yenyewe ni ya hapana tayari walishakubali process.
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
396
Whether wapo consistent au la, mimi naunga kwa asilimia 200 kitendo cha chadema kususia hotuba ya jk. Kwa mujibu wa sheria kandamizi zilizopo chadema hawana hatua nzito wanayoweza kuchukua dhidi ya uongozi uliowekwa madarakani kwa wizi zaidi ya hicho walichofanya. Wanaweza kwa mfano kila tukio analokuwepo Kikwete wao wanaondoka basi. Hiyo inatosha kuendelea kupeleka ujumbe kwamba hawamtambui kama raisi wao.
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,277
74,107
Swali lako linaonyesha upeo mfupi wa kufikiria wao wamebuni mbinu za kuiabisha CCM na mbinu hizo ni pamoja na kushiriki katika vikao vya bungeni kwa uchaguzi mkubwa. Kama ambavyo Matiba alikuwa anafanya alikuwa anaingia na kuonekana bungeni kiufundi "technical appearance." Hivyo mkoba wa mbinu za chadema katika kupambana na udhalimu huu ni nyingi na ninakuomba ufunge mkanda.

Upeo mfupi wanao wale wanaofikiri kwamba CCM ina haiba ya aibu, na inaweza kubadilika kwa "kuaibishwa"

Kama hii ndiyo strategy ya CHADEMA then wana safari ndefu sana, na wafuasi wao wajiandae kuona siku Slaa anarudi mstarini kama Seif Sharif Hamad "Ngangari".

Watu kumbe kelele zote hizi ni kushabikia show tu ?
 
monge

Member
Apr 10, 2010
30
0
Unaweza kutukusha taratibu zilizotumia na Mwl pamoja wapambanajia wenzake kudai uhuru kwa wakaloni?
Kama unadhani Chadema wanapoteza wakati,basi subiri uone!!!! siyo muhimu chadema kutumia atartibu ulotumika kenya
ama sehemu nyingine zozote.
 
Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
321
Narudia tena leo Mr. Kiranga unanishanga, ama umeamua kupiga kelele au kwa hiari yako umeamua kutokuelewa. Kama nafuatilia vizuri mchakato tangu uchaguzi hadi sasa naweza kukuthibitishia kuwa cdm ni chama makini na ndiyo maana pamoja na kuwa walikuwa na uwezo wa kuweka watu mitaani kupinga kile kilichokuwa kinafanywa na Kiravu lakini waliamua kutoruhusu mapambano kati ya ffu na raia kufanyika.
Chadema sijawasikia wakidai rais aliyeko wa jmt aliyeko madarakani kujiuzuru lakini pia wako wazi kueleza umma kuwa hawakuridhishwa na yale yalofanywa na tume ya uchaguzi mwaka and hawataki mambo haya yajirudie and therefore kama wanadai iundwe tume huru ichunguze mchakato wa uchaguzi uliopita ili kutengeneza namna nzuri ya kuwa na tume huru kwa siku za usoni.
Na kama haya ndiyo madai yao then ni watu makini na naamini JK na timu yake mambo hayo watayafanyia kazi.
Narudia tena, kwa msingi wa madai hayo hawakuwa na sababu ya kugomea pendekezo la waziri mkuu toka kwa rais. Mzee punguza kukurumuka ili tujenge taifa letu. Tanzania ni yetu wote ccm na wapinzani
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
396
Upunda wetu watanzania ndio uliotufikisha hapa. Jitu linaiba na kuhalalisha wizi wake nyie mnakaa na kusema hewala bwana. Hiyo karne imepita na kama wengi wenu mnadhani CUF nia sawa na CHADEMA basi mnakosea sana. Chadema ni chama makini na kimeshehena wasomi wa field zote. Kila tendo linalofanywa na chadema limechambuliwa kwa umakini mkubwa. Hawakurupuki kama vinavyofanya vyama vingine.
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,531
5,357
Waziri mkuu ameteuliwa na JK. Kwanini basi wasingejitoa? Kukaa ndani na kushiriki katika upigaji kura hata kama kura yenyewe ni ya hapana tayari walishakubali process.
Process iliyofuatwa ni ya bunge. Haikumhusu rais ingawa Pinda ni chaguo la rais. There is a thin line there.
 
Ngolinda

Senior Member
Apr 12, 2010
125
25
Hoja za kitoto kwa sababu nahoji sincerity na consistency ya CHADEMA ?

Kukurumuka mambo ya Kalemie au wapi hayo?

Kwa uelewa wako mdogo, unafikiri ninapoongelea habari ya CHADEMA kushiriki uhakiki wa Waziri Mkuu, naongelea habari ya Pinda. No wonder unameza vitu vizima vizima bila kumung'unya.

Kwa kushiriki uhakiki wa Pinda, chaguo la Kikwete, wabunge wa CHADEMA wamemtambua Kikwete kama rais tayari, sasa sijui hizi habari za kutomtambua Kikwete zinaanzia wapi wakati walishamtambua mpaka kupigia kura chaguo lake la Waziri Mkuu.

CHADEMA hawana consistency wala maturity ya kuchukuliwa seriously, nililisema kabla na sasa wanadhihirisha hili.

Mkuu Kiranga,
Ni kweli unayo sababu ya kutilia shaka Consistency ya CHADEMA ila bado haibadili dhana nzima ya kutomtambua Kikwete kama Rais wa JMT.
Unachoonyesha wewe ni jinsi gani CHADEMA walipaswa kufanya from the beginning ili kuwa consistent. Hilo sina shaka nalo, shaka yangu ni mtazamo na msisitizo wako juu ya jambo hili.

Je, ni kwamba unaona si sahihi CHADEMA kususia hotuma ya Kikwete au ulihitaji kuona wakifanya mambo ambayo ni pre-requisites ya hili?
Kama haja yako ni consistency, basi yamkini umeeleweka...na sasa pengine ni wakati wa kuipongeza CHADEMA walau kwa hatu hii na utoe ushauri nini kifanyike next. Vinginevyo utakuwa kama mtu aliyetumwa akanunue sanda kwa ajili ya kumhifadhi marehemu, lakini yeye akatokomea na fedha ya sanda kusikojulikana.
 
jyfranca

JF-Expert Member
Oct 3, 2010
297
7
Mjumbe wa Iran akiaanza kuzungumza kwenye Umoja wa mataifa, wajumbe wote wa Marekani, Israel na mataifa ya Ulaya wanatoka nje, kuonyesha hawakubaliani nae, na baadae wanarudi. CHADEMA wamefanya sawa kabisa, hii ni njia ya kuonyesha uchaguzi ulikua na tatizo na unaitaji marekebisho, si Maalimu Seif anaikandia tume hapo hapo anaingia ndani ya serikali
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,277
74,107
Mkuu Kiranga,
Ni kweli unayo sababu ya kutilia shaka Consistency ya CHADEMA ila bado haibadili dhana nzima ya kutomtambua Kikwete kama Rais wa JMT.
Unachoonyesha wewe ni jinsi gani CHADEMA walipaswa kufanya from the beginning ili kuwa consistent. Hilo sina shaka nalo, shaka yangu ni mtazamo na msisitizo wako juu ya jambo hili.

Je, ni kwamba unaona si sahihi CHADEMA kususia hotuma ya Kikwete au ulihitaji kuona wakifanya mambo ambayo ni pre-requisites ya hili?
Kama haja yako ni consistency, basi yamkini umeeleweka...na sasa pengine ni wakati wa kuipongeza CHADEMA walau kwa hatu hii na utoe ushauri nini kifanyike next. Vinginevyo utakuwa kama mtu aliyetumwa akanunue sanda kwa ajili ya kumhifadhi marehemu, lakini yeye akatokomea na fedha ya sanda kusikojulikana.

CHADEMA kama kweli wameibiwa kura walitakiwa hata wasile kiapo cha ubunge, kwani bunge linamtambua rais, na rais ni sehemu ya bunge.

Au hata kama wangesema wale kiapo cha ubunge kwa sababu hawawezi kuacha uwakilishi, kazi waliyotumwa na wananchi, kwa sababu ya wizi wa Kikwete, basi wangesusia kupigia kura chaguo la Kikwete, wangeanzisha bonge la zali watu waandamane nchi nzima, wamtoe Kikwete. Wangedai first order of business iwe kubadili sheria za uchaguzi na katiba. Hapo ningewaelewa na hata kuwaunga mkono.

Of course the most sensible thing ni kumtambua rais halafu kumletea mgogoro all the same bungeni, kila siku ma special motion ya kubadili sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba. Na of course Makinda atataka kuyazima, akiyazima tu mnamuwashia hata kwa maandamano barabarani. Hapo nitaona consistency na maturity.

Sio siku wakiamka kulia wanamtambua Kikwete kama rais, wakiamkia kushoto hawamtambui.
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,277
74,107
Process iliyofuatwa ni ya bunge. Haikumhusu rais ingawa Pinda ni chaguo la rais. There is a thin line there.

Process haimhusu rais wakati rais ndiye aliyependekeza jina.

Je Kiranga angepeleka jina pale wangepigia kura?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom