MTIZAMO: CCM Inadondoka... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MTIZAMO: CCM Inadondoka...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wamapalala, Jun 6, 2012.

 1. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  Hapana; wazungu wanasema, "hold on, CCM still alive and kicking".

  Katika nchi zenye demokrasia, chaguzi zozote zile (ubunge, serikali za mitaa, congress, senate, nk) kipindi cha kati (midterm) huwa ni mwiba mkali kwa chama na serikali iliyoko madarakani. kwa ujumla, utendaji wake kwa kipindi hiki huwa unakabiliwa na changamoto nyingi na ngumu.

  Ni katika kipindi hiki, utekelezaji wa ilani ya uchaguzi huwa bado haujakamilika, ni muda ambao pia chama na serikali yake hugundua kama kuna baadhi ya ahadi hazitekelezeki, vilevile ni muda ambao chama na serikali hukumbwa na kashfa za hapa na pale zinazowafanya wananchi waanze kuwa na wasiwasi au kukata tamaa na utekelezaji wa yale chama kiliwaahidi kwenye ilani ya uchaguzi.

  Na hapo ndipo ombwi linapotokea kati ya chama, serikali na wananchi. Kwa wana siasa na vyama vya upinzani ambavyo ni makini, huu ndiyo muda wa mavuno kisiasa. "Step in and fill the vacuum" kwa sababu katika kipindi hiki, chama na serikali tawala hupoteza nguvu ya hoja katika ulingo wa kisiasa kwa vile wananchi walichokuwa wanakitegemea hawajakipata (ahadi) na hata kama watakuwa wamekipata kitakuwa hakijakamilika kwa vile utekelezani wa ilani ya uchaguzi huwa ni katika kipindi kizima cha utawala kisheria kwa mujibu wa katiba(miaka mitano).

  Chama makini kama CHADEMA (samahani kwa kutogusia vyama vingine) wameliona hili na wanajitahidi katika uhamasishaji na uvunaji kisiasa (M4C) lakini changamoto na tatizo kubwa linalokikabili chama ni utegemezi wa watu mashuhuri wachache katika uhai wake kijamii. Chama kinaonekana kuwa hai pale wanapokuepo na wakiondoka kinalala(domant) au pia kinaondoka.

  CHADEMA wameweza kupambana kihoja kwa mafanikio katika ulingo wa siasa katika chaguzi ndogo na katika mikutano inayoendelea (m4c) lakini siyo jambo la ajabu kufanikiwa kama wanavyopenda jamii eamini. Sababu kuu za mafanikio nimezielezea hapo juu. Kazi kubwa katika siasa ni ujumbe kukubalika na Natumaini hata wataalamu wa mambo ya siasa watakubaliana nami.

  Ninapatwa na wasiwasi pale uvunaji wa kisiasa utakuwa ni kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu kwa nchi nzima. Ninasema hivi kwa sababu, kwanza, watu muhimu au maarufu ndani ya chama watahitajika kwenye majimbo yao ya uchaguzi , pili, muda ni mfupi wa kampeni katika uchaguzi mkuu ambazo zinachukua kama miezi miwili na tatu, upatikanaji wa nyenzo(pesa, usafiri).

  Chama hai si kile tu chenye nyenzo bali pia lazima kiwe na mizizi hai na matawi hai kwa maana lazima kiwe na jumuiya na wanachama hai kuanzia kaya mpaka taifa. Na kwa hili CCM inakuwa na mafanikio(advantage), kuna wengine watapinga lakini kwa aliye makini, kwa hili halina ubishi na imekuwa hivyo kwa vile kilishika hatamu (one party), kikajiimarisha kabla ya kuruhusu ushindani wa vyama vingi na hakikurudisha hizo nyenzo kwa wananchi wake.

  Nakubaliana pale Mwalimu Nyerere na wachunguzi wa maswala ya kisiasa wanaposema adui mkuu wa CCM ni CCM yenyewe na siyo vyama vya upinzani. CCM itaondolewa madarakani na wana CCM. Mitafaruku ndani ya CCM na Utendaji mbovu wa serikalini ndiyo adui wa uhai wa CCM. Adui mkuu wa vyama vya upinzani ni CCM na pia viongozi maarufu wakorofi ndani ya chama. Marumbano ya hivi karibuni ndani ya CUF (Maarim Seif na Hamad) na CHEDEMA(Shibuda na BAVICHA) huku pande moja ikiishutumu pande nyingine kuwa imepandikizwa na CCM ni ishara tosha .

  Changamoto kubwa na ngumu itakayovikabili vyama ya siasa (CHADEMA, CUF) ni katika uchaguzi wa mgombea urais kwa sababu vitaenda katika uchaguzi mkuu ujao vikiwa na matumaini hasa ya mgombea wake kushinda uchaguzi tofauti na mwaka 1995-2010 . Misuguano ya nani atapeperusha bendela ya kiti cha Urais itavifanya vyama hivi kumegeka au kushikamana lakini kuna uwezekano mkubwa wa vyama hivi kupata misukosuko mikubwa au kumegeka kwa vile itakuwa ni kwa mara ya kwanza kupatwa na changamoto hii kubwa wakati CCM waliisha ipitia katika awamu mbili za uchaguzi.

  Katika siasa, wiki moja ni ndefu, safari ni ndefu zaidi katika miaka miwili na nusu. Wanaodiriki kusema CCM imekwisha huku akichukua mifano ya vyama vingine vilivyokuwa vikongwe katika Nchi za Kenya (KANU), zambia (UNIP) wakati mazingira ya kisiasa ni tofauti wanajiliwaza au wanaota ndoto za mchana lakini iwapo CHADEMA kwa Tanzania bara na CUF kwa Tanzania visiwani watashikamana kisiasa na kujinasua na changamoto nzito ya uchaguzi wa wagombea hasa kiti cha urais na kuendelea na kasi waliyonayo kwa sasa wakati baadhi ya watendaji ndani ya CCM wakiendelea na utendaji wa kimazoea. Kuna uwezakano mkubwa Tanzania ikaingia mwaka 2016 ikiwa kwenye mabadiriko makubwa ya kisiasa ambayo hayajawahi kutokea katika historia nchini.

  Kwa jinsi ishara zinavyoonyesha, kwa sasa hakuna lisilowezekana katika medani ya kisiasa nchini wakati huohuo, waswahili anasema, usione simba kanyeshewa ukadhani ni paka.
   
 2. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  HIVI KWANINI MSIENDE STRAIGHT NA MADA ZENU MPAKA MUANDIKE MAFUMBO. HEADING IKO VILE! CONTENT IKO HIVI.

  KWANINI MAFUMBO. AU NI KUTAFUTA POWER OF REPLY!. by the way CCM kwisney. Inaekelea wewe unakaa mafichoni.

  Fuatalilia kwa karibu uchaguzi wao ndo utajua uimara wa CCM
   
 3. m

  mumburya JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 268
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 45
  Inawezekana hapa kaandika TUNU PINDA
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  mkuu mbona sijaona hoja yako hapa? 1+1=5
   
 5. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kigumu chama cha magamba.......Ziendelee kudumaa kasi na nguvu zao.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Endeleeni kuvaa kitambaa cheusi ,kila mtu anasababu zake za kung'ang'ania kubaki madarakani,mungejua utamu wa utawala mungetekeleza basi ile kitu roho ya wananchi inapenda,maisha magumu, magumu,tabaka la walio nacho na sio linapanuka mithili ya moto wa mabua,uvunaji wa rasilimali usio na tija ,kushindwa kwa sera zote za ustawi na maendeleo kwa jamii kwa mfano sera ya elimu ya sekondari na vyuo vikuu,afya,maji,mazingira,ujenzi wa majengo,kilimo kwanza,madini bado unaanzisha propaganda za kichina kwamba eti CCm itafanya vizuri,kitu gani itafanya vizuri ambacho wameshindwa kwa miaka hamsini,ahadi 170 za 2010 za Kikwete hata asilimia moja haijatekelezwa,samahani napenda kukwambia kwamba sisi watanzania hatutaendelea kuwa madondocha kamwe tumieni lugha zozote tamu za kulainisha lakini watanzania tutawaambia kuwa tumewafahamu kwa miaka hamsini nyie ni waongo,wavivu wa kufikiri na ubunifu,wezi,wabadhirifu,wafuja nchi na wadumazi wa maendeleo na ustawi wa nchi yetu munataka kutuaminisha kwamba wananchi hawaamui wenyewe kuichukia CCM imekula kwenu
   
 7. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hata mimi naamini CHADEMA wanachukua. Na I call upon/ naomba Watanzania wote tuungane kuhakikisha tunaiunga mkono CHADEMA. Ndo chama pekee kwasasa kina huo uwezo. Jamani Afrika yote wamefanya mabadiliko bado sisi tu. Zimbabwe hawana uhuru kama sisi. Je sisi tatizo nini?
   
 8. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi pia nimepata 0+0=1
   
 9. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  mumburya-----Mimi siyo mfuasi au mpenzi wa chama chochote cha kisiasa. Huu ni mtizamo wangu nje ya upenzi na ukeleketwa kisiasa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145


  MTENGETI----------Hakuna mafumbo yoyote katika thread, kama ukiisoma kwa macho mawili nafikili utaelewa vizuri. Kama kwa mtazamo wangu unakufanya uwe na jumuisho la kuwa ninakaa mafichoni hilo sina nguvu ya kukuzuia. Huu ni mtazamo wangu nje ya ushabiki na upenzi wa vyama ya kisiasa.
   
 11. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145

  POMPO-------jaribu kusoma kwa macho mawili ndipo utagundua kama hoja yangu ni well balanced and 1 + 1 = 2
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Ngoja na mimi nitoe Kastory Kangu
  Ninafanya partial quotation ya movie moja niliiangalia miaka mingi huko nyuma, ama ilikuwa ikiitwa Burton au the main character aliitwa burton.

  Burton alizaliwa akiwa mzee kikongwe, akaanza kukua kuelekea udogo, kwa hiyo kutokana na umri wake tangu areport hapa duniani alilazimika kucheza na watoto wadogo, ni mkasa ambao unahitaji roho ya ajabu kuweza kucheka, sababu ni mkasa wa kusikitisha, hasa ilipofikia kipindi burton na yeye alipoanza kutongoza vibinti kama vijana wenzake, ilikuwa mbaya sana. Hakuna binti alimkibali, sababu he looked very old for them, baadhi ya wazazi waliwakaza watoto wao kucheza na burton sababu waliona kama atawafundisha tabia mbaya kutokana na umri wake. Wakati marafiki zake wanamiaka kumi, burton alionekana anamiaka kati ya sitini mpaka sabini.Kwa kifupi Burton dead out of frustration kama sikosei

  Hivi ndio ilivyo CCM. Kabla ya CCM kuwapo, mfumo wa vyama vingi ulikuwapo, CCM ikazaliwa na kufanywa chama pekee cha siasa nchini (the old way). hivi sasa inapambana na vyama vichanga, Am told CHADEMA is about 21 Years old. CCM inaonekana kuwa between its 70s au 80s very old,tired and irrelevant. Imejikuta katika very frustrating situation, new and hash environment.

  Hivyo, ndugu yangu Ng'wamalala hiki chama hata kikiachwa chenyewe kwenye ulingo wa siasa kitapoteza maisha kwa mshangao.

  Kwa sababu kimeshindwa kuwa na mfumo realistic wa kuendana na mazingira (ambayo hakikuwahi kujua kama yatabadirika kiasi hiki) kama wanavyozeeka kwa umri waasisi wake wa binaadamu ndiyo kinavyozeeka. Kumbuka itikadi zake sio tu zimezeeka, ziliisha kufa na kuzikwa.
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,006
  Likes Received: 2,658
  Trophy Points: 280
  Kichwa cha habari na kilichomo havifanani sijui ulikusudia nini?
   
 14. M

  Melubo Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kipengele hiki kimenigusa na naunga mkono.."Mitafaruku ndani ya CCM na Utendaji mbovu wa serikalini ndiyo adui wa uhai wa CCM"
   
Loading...