Mtiririko wa Matukio ya Uundwaji wa Serikali ya awamu ya tano: CCM kicheko, UKAWA kilio

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Tunakaribia kufikia tamati ya mchakato wa kupata serikali ya awamu ya tano ambapo mchakato huo utahitimishwa kwa Rais Magufuli kutangaza baraza jipya la Mawaziri. Hata hivyo, ni vema tukajikumbusha wapi tumetokea mpaka tumefikia hapa tulipo. Nitawawekea baadhi ya matukio na jinsi CCM ilivyoibuka kidedea kwenye kila hatua.

1. MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS WA CCM: Lowasa akatwa

Bila shaka mtakubaliana nami kuwa mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM ulivuta hisia za Watanzania wengi. Hata vyama vya upinzani, walikuwa wanyonge kipindi hicho kwa vile hawakuwa na mtu ambaye angeweza kupambana na mgombea yeyote wa CCM. Kati ya majina 42 yaliyojitokeza kugombea, jina la Edward Lowasa ndilo lililoongoza kutangazwa sana kwa vile alikwishavinunua vyombo takriban vyote vya habari isipokuwa Sahara Media na TBC. Hali hiyo ilifanya Watanzania waamini kuwa Mgombea ajaye wa Urais atakuwa Edward Lowasa.

Mkakati wa kumpeleka Lowasa Ikulu uliandaliwa kwa karibu na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang'onda. Kupitia kwake, ndipo mirija ya fedha kutoka kwa wafadhili kama akina Rostam Aziz, Reginald Mengi na Yusuph Manji ikawa inatiririka kwa lengo la kununua makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wa dini.

Naam, CCM ikasimama imara katika kusimamia misingi yake na ilihakikisha kuwa ni yule tu anayeendana na maadili ya chama hicho na taifa ndiye anayeteuliwa kuwa Mgombea Urais. Ndipo alipopatikana John Pombe Joseph Magufuli ambaye hakutarajiwa na Watanzania wengi. Ikawa kilio wa Lowasa na timu yake ya mafisadi na kicheko kwa Wazalendo. Lowasa akakatwa na hakika alikatika vibaya sana. CCM ikashinda mtihani wa kwanza.

2. LOWASA KUHAMIA CHADEMA

Baada ya Lowasa kukatwa CCM, hakika ilikuwa ni majonzi tele kwa Timu ya Mafisadi. Lowasa alijipambanua kuwa yeye ndiye Rais ajaye na kwamba hakuna mtu mwenye jeuri ya kukata jina lake ndani ya CCM. Sasa jina lake limekatwa na ndoto za kwenda Ikulu kupitia CCM zimeyeyuka. Akaona isiwe taabu. Bora ahamie Upinzani huku akinukuu vipande vipande kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM.

Lowasa akatangaza kuachana na CCM na kujiunga na UKAWA kupitia CHADEMA ambapo aliteuliwa kuwa mgombea Urais baada ya kutoa kitita cha shilingi Bilioni 10 kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye kwa wakati huo ndiye aliyekuwa na ushawishi ndani ya UKAWA.

Wakati Lowasa anajiunga UKAWA, alitangaza kuwa anaenda akiwa na kundi kubwa la viongozi na wafuasi wa CCM. Alisema kuwa anaenda UKAWA akiwa na mtaji wa Wabunge 50, Wenyeviti wa Mikoa 15 na Wenyeviti wa wilaya 105. Hata hivyo, kilichotokea kimemshangaza yeye mwenyewe. Ni wenyeviti wawili tu ambao ni Mgana Msindai wa Singida na Hamisi Mgeja wa Shinyanga. Pia wabunge waliomfuata ni watano tu tena wengi wao wamehama baada ya kushindwa ndani ya CCM. hili lilikuwa ni pigo kubwa kwake na CCM ikashinda mtihani wa pili ijapokuwa Lowasa aliendelea kujifariji kuwa ana kundi kubwa la wapiga kura.

3. USHINDI WA CCM KWA NGAZI YA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI

CCM iliingia kwenye uchaguzi Mkuu ikiwa na dhamira ya kuibuka na ushindi. Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana alisimamia vema mpango kazi wa USHINDI hasa katika kusimamisha wagombea wenye sifa na kampeni za kisayansi. UKAWA wakawa wanategemea nyomi ya kwenye mikutano ya kampeni. Pia UKAWA wakawa wanawatumia mapandikizi yao ndani ya CCM kuhakikisha wanakihujumu chama

Kama hiyo haitoshi, Lowasa akaunda kikosi kazi mitandaoni ambacho pamoja na kusambaza propaganda za uongo, kilipewa juumu la kuchakachua matokeo na kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, mikakati ya CCM ilifanikiwa baada ya kuibuka na ushindi kwenye mafiga yote matatu. Aidha, ilikuwa ni pigo kubwa kwa UKAWA kwani kipigo walichokipata kiliwashtua sana. Kilichowaumiza zaidi ni baada ya vijana 191 waliokuwa wanachakachua matokeo kukamatwa ambapo mpaka sasa wanashikiliwa na vyombo vya dola.

4. LOWASA NA UKAWA KUHAMISHIA VITA DODOMA.


Baada ya kichapo walichopata toka CCM, Lowasa na UKAWA wakaendelea kutapatapa. Kwanza waliendelea na msimamo wao kuwa hawatambui ushindi wa Rais Magufuli. Hata hivyo wakaona kuwa biashara hiyo hailipi. Kwa hali hiyo, walihakikisha kuwa wanaingilia michakato ndani ya CCM katika kupata nafasi ya Spika, Naibu Spika na Waziri Mkuu. Pia waliweka mikakati ya kuzuia Rais kutoa Hotuba ya kuzindua Bunge kwa vile waliona kuwa kupitia Hotuba hiyo, hadhi ya CCM itarejea na UKAWA watapotea.

Kuhusu Spika na Naibu Spika, Lowasa alihakikisha kuwa mapandikizi yake kama Emmanuel Nchimbi, Zungu na wengineo wanapenya kwenye mchakato huo, kitita kikubwa cha fedha kilitengwa ili kuwarubuni wabunge wa CCM. Kilichotokea ni kwamba, wabunge walikula fedha hizo na mapandikizi ya Lowasa hayakupitishwa.

Lowasa akaona isiwe tabu, akageukia nafasi ya Naibu Spika. Nako akakwamba kwa vile CCM walishashtukia mchezo wake. Akaanza kusambaza propaganda kupitia wabunge wa UKAWA kuwa Mgombea Unaibu Spika, Tulia Akson ni wa kuletwa na Rais. Matarajio yake ni kuwa Mgombea wa UKAWA, Esther Sakaya angeweza kupata support kubwa kutoka wabunge wa CCM. Kilichotokea ni kichapo tu. CCM ikashinda mtihani mwingine.

Kuhusu uteuzi wa Waziri Mkuu, UKAWA walikuwa na matarajio kuwa Rais Magufuli angeteua watu ambao wana makando kando ili wapate pa kutokea. Wakawa wanahaha huku na kule kuhakikisha kuwa wanapata jina la Waziri Mkuu mapema ili waanze kumchafua hata kabla hajatangazwa na Rais. Rais Magufuli akacheza kama Pele. Uteuzi wa Waziri Mkuu ukawa ni siri yake binafsi. Alihakikisha siri hiyo inatunzwa hadi hatua ya mwisho. Hata barua ya uteuzi aliandika mwenyewe kwa mkono wake. UKAWA wakakwama na CCM ikashinda tena mtihani wa Waziri Mkuu.

Mtihani uliopo kwa sasa ni wa Kukwamisha Hotuba ya Rais Magufuli Bungeni ambapo atahutubia leo majira ya Alasiri. Hata hivyo, hawatafanikiwa. Kwani taarifa za kuaminika zilizopo ni kwamba wabunge wa UKAWA wamekataa maamuzi ya Mbowe na Lowasa ya kuzomea Bungeni. Kwamba, kitendo hicho kitasababisha wananchi wauchukie upinzani kwa kuendesha siasa za kijinga. Wamesema kuwa ni bora wasiingie Bungeni kuliko kufanya mambo ambayo yatawaharibia kisiasa.

Wabunge wanasema kuwa hoja inayotolewa na viongozi wao kuwa wanapinga kitendo cha Rais wa Zanzibar kuingia bungeni haina mantiki kwa vile mpaka sasa Rais wa Zanzibar aliyeapishwa ni Dk Shein tu na hakuna Rais mwingine aliyeapishwa. Pia wanasema kuwa ijapokuwa Viongozi wa UKAWA wanafanya ulaghai wa kumkataa Dr Shein, Maalim Seif Sharif Hamad bado anatambulika kama Makamu wa Kwanza wa Rais na hajaikana nafasi hiyo. Kwa mazingira haya, ni dhahiri kwamba CCM imeshashinda mtihani huu.

Nimalizie kwa kusema kuwa, CCM kwa sasa imeimarika kuliko wakati mwingine. Ka vile imeshinda mitihani yote hii, ni dhahiri kwamba Mungu yu pamoja nasi. UKAWA jipangeni kwa ajili ya 2025.
 
tangu walipo mpokea lowasa ni wazi misingi ya ukawa lazima iyumbe
 
Tunasubiri utekelezaji wa Ilani. Yoyote, CCM ama UKAWA, ingeingia madarakani basi mwisho wa siku tungewapima kwa kukuza uchumi, kupunguza umaskini, huduma bora za kijamii kama elimu, afya, miundombinu, kukua kwa umoja na amani, nk. Nadhani kwa mtu aliyeenda shule na akaelimika basi atakipima chama cha siasa kilichoshika dola kwa kuzingatia mambo niliyoyabainisha na mengine yanayofanana na hayo.

Ni mapema sana kutoa hitimisho juu ya mafanikio ya Serikali ya Viwanda ya Magufuli. Ni mtazamo wangu.
 
Chadema duh.... Tumepoteza misingi ya chama chetu... nadhani wabunge wetu ni mda wakurudisha hadhi yetu..
tumekua watu wazur wa kubisha kwa hoja... tuachane na makelele sisi watu wenu tunakuwa hatuwaelewi...
Tuachane na watu wa kuje turudi kwenye misingi yetu..
 
CCM ni mfano wa dhahabu,kwa sasa dhahabu hii inang'aa kuliko wakati wowote kwa kuwa imepitia moto mkali zaidi.WEMBE KUPITA ULE UNAENDELEA KUNYOA.
 
mada nyingine ni kama kurudi nyuma, zinafaa kuwekwa kwenye jukwaa la historia.... tuongelee yajayo na maendeleo ya watanzania kwa ujumla, nini kitawakwamua watu walio maskini na kuwapa na maisha bora, kuinua elimu na huduma za afya, kuendeleza mada za 'kukatwa' lowasa ni kuishiwa ki mawazo....
 
kupigana na mtu uliemfunga kamba then unajisifia ni vchekesho tu kama watetezi wa mita 200 ndo leo wanakuwa promoted
 
Chadema duh.... Tumepoteza misingi ya chama chetu... nadhani wabunge wetu ni mda wakurudisha hadhi yetu..
tumekua watu wazur wa kubisha kwa hoja... tuachane na makelele sisi watu wenu tunakuwa hatuwaelewi...
Tuachane na watu wa kuje turudi kwenye misingi yetu..
Wewe ni moja ya mazombie wa ccm Mliozoea kuburuzwa
 

Kuhusu uteuzi wa Waziri Mkuu, UKAWA walikuwa na matarajio kuwa Rais Magufuli angeteua watu ambao wana makando kando ili wapate pa kutokea. Wakawa wanahaha huku na kule kuhakikisha kuwa wanapata jina la Waziri Mkuu mapema ili waanze kumchafua hata kabla hajatangazwa na Rais. Rais Magufuli akacheza kama Pele. Uteuzi wa Waziri Mkuu ukawa ni siri yake binafsi. Alihakikisha siri hiyo inatunzwa hadi hatua ya mwisho. Hata barua ya uteuzi aliandika mwenyewe kwa mkono wake. UKAWA wakakwama na CCM ikashinda tena mtihani wa Waziri Mkuu.

Chifu, sijui wewe unaegemea upande upi. Lakini kwa ulichoandika ni dhahiri upo upande wa CCM.

Leo hii unasema Kassim Majaliwa hana makando kando, wakati wabunge wa CCM walimwona mzigo hapa juzi juzi!!??

Wabunge wa CCM wawakalia kooni mawaziri mizigo - Kitaifa | Mwananchi

Pili, hilo la siri si gazeti la Nipashe liliandika kuhusu uteuzi wa Kassim Majaliwa kabla ama?

Home
 
GAMBA HILI LIMETUMWA KULETA PROPAGANDA ZA KIJINGA, MODE MPE BAN YA KUDUMU HUYU MLETA MADA , ni mchochezi na hamna kitu kichwani
 
mada nyingine ni kama kurudi nyuma, zinafaa kuwekwa kwenye jukwaa la historia.... tuongelee yajayo na maendeleo ya watanzania kwa ujumla, nini kitawakwamua watu walio maskini na kuwapa na maisha bora, kuinua elimu na huduma za afya, kuendeleza mada za 'kukatwa' lowasa ni kuishiwa ki mawazo....
Mkuu, kabla hatujaenda mbele, ni vema tukajikumbusha nyuma. Na kwa vile kuna tukio ambalo halijatokea, ni vema tukapata muda wa mjadala. Je UKAWA watafanikiwa kukwamisha hotuba ya Rais?
 
Back
Top Bottom