Mtikila: Watanzania tumuunge mkono Dk. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila: Watanzania tumuunge mkono Dk. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MAMA POROJO, Aug 17, 2010.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amekiri kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa ni mpambanaji wa siasa za mageuzi na anastahili kuungwa mkono na Watanzania.

  Mtikila alieleza hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Chacha Wangwe kilichotungwa na Mwanaharakati Deo Meck.

  Alisema akiwa bungeni Dk. Slaa aliweza kupambana na hata kurekebisha yale ambayo serikali kwa makusudi iliyaficha kwa maslahi yake na kuwataka Watanzania kuwapima wagombea kutokana na sifa na vigezo vyao.

  Akizungumzia marehemu Wangwe alisema: “Kifo cha Chacha Wangwe kimetufundisha mengi na tunahitaji kuyaendeleza yale mazuri kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho; ni muhimu sasa tuyafanye kwa maslahi ya taifa letu,” alisema Mtikila.

  Aidha, alisema kitabu hicho kitasaidia kuleta siasa za kweli kwa kufanya yale ambayo marehemu Chacha Wangwe aliyafanya akiwa bungeni kwa maslahi ya Watanzania na kuwatetea wanyonge.

  Kwa upande wake mtunzi wa kitabu hicho, alisema kitabu hicho amekitunga kwa nia ya kukumbuka yale mema aliyoyafanya marehemu Wangwe na sio kumsema mtu kama ilivyodhaniwa na baadhi ya watu.

  “Leo ninazindua kitabu hiki kwa maslahi ya kumbukumbu zetu wala sina chuki na mtu yeyote na wala sijamsema mtu wala taasisi yoyote, Watanzania wakisome wachukue yaliyo mema hasa hasa aliyoyafanya Wangwe,” alisema Deo.
   
 2. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa Tarifa yako mleta Madada , wapenzi na wafuasi wa CHADEMA hata kama kitashinda 99.9% ,kupewa Serekali hilo msahau Dr Wilbrod Slaa atasoma huku anahubiri kila peji katika Bible wakati wa kampeni za Uchaguzi lakini hatopewa Kuongoza Nchi.
   
 3. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM wameishiwa FUNGU?? Au ndo anatafuta njia ya kuja kuvuruga..
  herrrrooooooooo..........nina mawe yangu mfukoni hapa...sina haja ya POLISI
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa si bure kuna kitu aidha kazidiwa kete na mzee wa kiraracha au anawakumbusha CCM kuwa na yeye yupo wasimsahau.
   
 5. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,582
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Mkuu katika hali ya kawaida naweza kusema wewe si MZALENDO kabisa.Nasema hivyo kwa sababu mtu yeyote ambaye kiukweli anaipenda nchi hii na wananchi wake,kwa mara ya kwanza katika hizi awamu mbili za uongozi wa nchi hii tunaweza kusema kabisa kuwa tuna mtu ambaye tunaweza kusema kuwa anafaa.
  Huyu jamaa amepambana na hawa watu mpaka ikafikia wakati wanamtegea vinasa sauti hotelini,wote hilo tunalijua.Naona imefika wakati sasa watanzania tuachane na siasa za kasumba na ushabiki tuweke maslahi ya TAIFA mbele.Hakuna asiye jua kuwa nchi inaliwa na kikundi cha watu wachache tu ambao wapo ndani ya CCM-na hili hata wanaccm wenyewe wanalijua ila mfumo waliojengewa ndiyo unaozuia watu wenye kaliba ya Dr.Slaa walioko ndani ya hicho chama washindwe kukikwamua.Angalia watu kama Selelii alivyochinjwa kisiasa kule Nzega,huo ni mfano mmoja tu.
  Come back back to your senses man ili uone kuwa you need to go hand to hand with people like Dr.Slaa and alike ili tuikomboe nchi kutoka mikononi mwa hawa MANYANG'AU!!!Look at what Makamba did to William Shellukindo kule Bumbuli,yaani hii nchi inakuwa ni ya uongozi wa kurithishana tu.Vita Kawawa,Zamaradi Kawawa,January Makamba na wengine kibao-hivi ubunge wanaweza watoto wa vigogo tu?
  Sikatai wengine wana uwezo,ila wengine mmhh!
  Eee TANZANIA,sasa umefika wakati tuungane ili tumtoe na kumtokomeza huyu COMMON ENEMY kwetu wote ambaye ni UFISADI na mafisadi,period.
  C-chagua
  H-haki
  A-amani
  D-demokrasia
  E-elimu
  M-maendeleo
  A-afya
  That is what we mean when we say CHADEMA!!
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Aisee hii imetulia
   
 7. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  hata mie nimeipenda....chagua,haki,amani,democrasia,elimu,maendeleo na afya ebwana eeee Slaa umeiona hiyo?
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kumbe mtikila zipo? Awe miongoni mwa watakaompigia slaa kampeni
   
 9. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,466
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Rev Mtikila hatabiriki,kumbuka naye ni mgombea uraisi kwa tiketi ya chama chake.
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Chichichieeem mnapata shida sana sasa hivi
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  C-chagua
  H-haki
  A-amani
  D-demokrasia
  E-elimu
  M-maendeleo
  A-afya
  That is what we mean when we say CHADEMA!![/QUOTE]
   
 12. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hilo si kweli kwamba CHADEMA ishinde 99.9% halafu wakunje matokeo. sema watanzania wengi hatujui wapi tulipo sasa na wapi tunaelekea. Ndo maana wengi wetu hatutapiga kura tarehe 31 Oct. Unakuta wasomi tuinaojadili maada hizi tunasubiri watu wapige kura halafu sisi tucomment tu.

  wale waliozoea kupanga foleni watapanga na vijisenti walivyopewa ili kuvumilia watapigia tena CCM na hivyo wanamapinduzi kubaki na
  Kelele zetu 99.9% siyo kura.
  safari yetu ni ndefu jamani CCM hawaibi kura kivile ila wana uwezo wa kujipanga na kuwatafuta watu wa kupiga kura.

  Namkubali sana Mtikila, Is among wapinzai wa kweli kabisa.:confused2:
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  Nashauri yeye awe special kujibu mabomba ya Mrema ambaye atatumiwa na CCM, lakini Mtikila akumbuke kutotia timu Tarime maana yale mawe jamaa bado wanayo.
   
 14. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  tarime mtikila anakaribishwa kama ana sera mura ila kama ni mjungu noo si mmesikia yaliyompata mwera alitimuliwa kufanya mkutano, tarime hatuna njaa ndio maana hatudanganyiki igeni mazuri ya tarime jamani nawaomba
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu tunapiga vita udini hapa
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,649
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  Mawazo ya udini yamepitwa na wakati, tunahitaji kiongozi mwenye uwezo na maono ya kutuondolea kero, awe na dini au la, dini ni yake na mungu wake, tunachojali ni uwezo, na mtu huyo kwa wakati wetu ni Dr Slaa.
   
 17. M

  Mavanza Member

  #17
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wanataka yatokee ya Kenya sawa, safari hii hatukubali ni bora baadhi yetu tutolewe kafara kuliko kuona madaraka yanachukuliwa kwa nguvu.
   
 18. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kumbe mkuu nawewe umo humo eeeh!!!
   
 19. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Ni vuvuzela hilo!!!
   
 20. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mtikila kama Mtikila ni binadamu kama binadamu wengine. kama ameyaona madudu yake kwenye kampeni ya kule Tarime na kujisahihisha basi inapasa kumkaribisha kwa kuwa anapigania mabadiliko ya kweli.

  Waziri mkuu mpya wa uingereza alipohojiwa juu ya makosa yake (na hasa akishutumiwa kuwa aliwahi kuvuta bangi) alijibu kwa kusema kuwa kila binadamu amewahi kufanya makosa ambayo kwa hakika anajuta kwayo.

  Mtikila anajuta na hivyo tumkubali.
   
Loading...