Namkubali sana Mtikila,japo wakati mwingine njaa huwa zinamchanganya akili.
Kweli! Njaa ni janga la Taifa!
Namkubali sana Mtikila,japo wakati mwingine njaa huwa zinamchanganya akili.
Yah jamaa ni mjasiri kweli hao kina slaa mbowe wote hamna kitu.
Mnaonaje watanganyika mkamteua mtikila kuwa ndie baba yenu wa taifa la tanganyika?mkizingatia kuwa nyerere ndie alieiua tanganyika yenu,zanzibar kwanza.
kura ya siri itawatesa CCM lakini tuweke na tulifanye bunge la katiba tukiweka utaifa mbele, mambo ya vyama baadaye
Akichangia ktk semina maalum ya Bunge la Katiba leo, Mch Christopher Mtikila amesema kua nchi hii hakuna mtu jasiri zaidi yake.
Ni katika mapendekezo yaliyowasilishwa na kamati ya bunge juu ya kupigwa kura ya "siri" au kura ya "wazi" ktk maamuzi mbalimbali wakati wa vikao vya bunge maalum la katiba,mch Mtikila akichangia alisema,..........,Mimi sioni kwanini kura iwe ya wazi,mbona wakati tukimchagua Mwenyekiti wa muda wa bunge hili la Katiba tulimchagua kwa kura za siri?
Mnasema kupiga kura za "Uwazi" ni UJASIRI,,mimi sijapata kuona mtu jasiri nchi hii zaidi yangu! ....alimaliza kusema Mch Mtikila.
Huyo ndie Mtikila Mzee wa Tanganyika.
Mtikila ni mnafiki alinikera pale alipokuwa anawapaka akina rOSTAM kuwa ni mafisadi halafu akathibitika kupokea pesa zake milioni 3, hakika nilimuona kichaa