Mtikila: Hakuna mtu jasiri nchi hii zaidi yangu!

Mtikila: Hakuna mtu jasiri nchi hii zaidi yangu!

Joined
Feb 20, 2014
Posts
87
Reaction score
35
Akichangia ktk semina maalum ya Bunge la Katiba leo, Mch Christopher Mtikila amesema kua nchi hii hakuna mtu jasiri zaidi yake.

Ni katika mapendekezo yaliyowasilishwa na kamati ya bunge juu ya kupigwa kura ya "siri" au kura ya "wazi" ktk maamuzi mbalimbali wakati wa vikao vya bunge maalum la katiba,mch Mtikila akichangia alisema,..........,Mimi sioni kwanini kura iwe ya wazi,mbona wakati tukimchagua Mwenyekiti wa muda wa bunge hili la Katiba tulimchagua kwa kura za siri?
Mnasema kupiga kura za "Uwazi" ni UJASIRI,,mimi sijapata kuona mtu jasiri nchi hii zaidi yangu! ....alimaliza kusema Mch Mtikila.

Huyo ndie Mtikila Mzee wa Tanganyika.
 
Yah jamaa ni mjasiri kweli hao kina slaa mbowe wote hamna kitu.
 
Kura lazima inapaswa kuwa ya siri, au ccm inataka kutumia nafasi hiyo kuwaburaza wa bunge wake pamoja na wajumbe walio pewa shavu na mkuu wakaya.....wanataka kuwajengea nidhamu ya woga hapo
 
kura ya siri itawatesa CCM lakini tuweke na tulifanye bunge la katiba tukiweka utaifa mbele, mambo ya vyama baadaye
 
Semeni yoote kura ya siri itatufikisha tunapotaka kwenda

Mimi binafsi pia ni muumini wa kura ya Siri! Kupiga kura ya Uwazi ni njia ya kudhibiti baadhi ya Wabunge wenye mawazo tofauti na msimamo wa chama!
Inaaminika kwamba kuna mgawanyiko mkubwa sana ndani ya wabunge wa bunge maalum la katiba kwa upande wa chama fulani,ndio maana inapendekezwa kura iwe ya Uwazi ili kuwadhibiti na kuwatisha wabunge wao.
 
Akichangia ktk semina maalum ya Bunge la Katiba leo, Mch Christopher Mtikila amesema kua nchi hii hakuna mtu jasiri zaidi yake.

Ni katika mapendekezo yaliyowasilishwa na kamati ya bunge juu ya kupigwa kura ya "siri" au kura ya "wazi" ktk maamuzi mbalimbali wakati wa vikao vya bunge maalum la katiba,mch Mtikila akichangia alisema,..........,Mimi sioni kwanini kura iwe ya wazi,mbona wakati tukimchagua Mwenyekiti wa muda wa bunge hili la Katiba tulimchagua kwa kura za siri?
Mnasema kupiga kura za "Uwazi" ni UJASIRI,,mimi sijapata kuona mtu jasiri nchi hii zaidi yangu! ....alimaliza kusema Mch Mtikila.

Huyo ndie Mtikila Mzee wa Tanganyika.

Ni jasiri maana hakuna anayeweza diriki kutoa maoni yasiyo ya kujikomba kumsema rais!
 
nakukubali sana mch mtikila 2ngekuwa na wachungaji kumi kama wewe!!!
 
Wakati nasoma Shahada ya kwanza UDSM,walimu wangu mbalimbali walikuwa wakimuita Mchungaji Mtikila 'Baba wa Sheria' Tanzania. Nakubaliana nao. Ni mtu jasiri mno;kuliko yeyote ninayemfahamu.Ni ujasiri wa kupigania mabadiliko na kuzia kuharibiwa kwa Katiba na Sheria nchini
 
Mnaonaje watanganyika mkamteua mtikila kuwa ndie baba yenu wa taifa la tanganyika?mkizingatia kuwa nyerere ndie alieiua tanganyika yenu,zanzibar kwanza.
 
Namkubali sana Mtikila,japo wakati mwingine njaa huwa zinamchanganya akili.
 
Inakuwaje ajisifu mwenyewe, badala ya kusifiwa? Hapo kuna walakini! Majasiri ni wale watu wa Tarime waliompopoa mawe alipowapelekea longolongo za kipuuzi!
 
Wakati nasoma Shahada ya kwanza UDSM,walimu wangu mbalimbali walikuwa wakimuita Mchungaji Mtikila 'Baba wa Sheria' Tanzania. Nakubaliana nao. Ni mtu jasiri mno;kuliko yeyote ninayemfahamu.Ni ujasiri wa kupigania mabadiliko na kuzia kuharibiwa kwa Katiba na Sheria nchini

Wabongo kwa kujimegemea kila kwenye Fursa hamjambo! Namie namkumbuka sana Mwl wangu Dkt Sherwan wakati nafanya Research yangu ya MBA (Esami) aliwatahadharisha juu ya watu wanaojisifu wenyewe hata kama kweli hizo sifa wanazo. Egoism Principle.
 
Back
Top Bottom